Kamawewe
JF-Expert Member
- Jan 16, 2013
- 531
- 500
Nina ndugu wa karibu wamekosa mikopo pamoja na umasikini na kufaulu kwao. Inauma sana huyu mama Mungu anamuona. Tuliwakebehi BAKWATA walipomkataa lakini sasa watu wengi zaidi wanaona uchungu wa kutengwa, kunyanyasa na kutosaidiwa na serikali. Ninamuomba Mungu niendelee kuwa mzalendo kwa nchi yangu.Wakati ndugu zetu waislam wanamkataa huyo bi Joyce Ndalichako pale baraza la mitihani (Siwezi kum-adress kama profesa kwa jinsi anavyotenda), nilidhani kuna chembe za udini (Naoimba nikiri hivyo), lakini sasa nimetambua waislamu wale walikuwa sahihi sana na waliona vitu ambavyo wengine tulikuwa hatujaviona au kupofushwa na hoja ya udini!