G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Hivi umewahi kujiuliza kuwa ikiwa mwanao au ndugu yako wa kawaida anayesomeshwa chuo kikuu na serikali walau kwa "kamkopo" ka asilimia kadhaa na kupewa hela ya kujikimu kisha akasitishiwa ghafla hayo yote na wakati huohuo ukiwa haujajipanga na huyo ndugu/mwanao anatokea katika familia ya kawaida kabisa?
Basi pale ghafla utakapojikuta ukitakiwa kumpa siyo chini ya Tshs. Elfu hamsini tu kila wiki na ukitakiwa kuandaa ada ya siyo chini ya Tshs. 1.5 million kwa kila mwaka wa masomo kwa muda uliobaki ambao amesitishiwa hiyo huduma muhimu na serikali ndipo utakapojua hasa ni nini maana ya kujikuta ukiwajibika ili fulani aende.
Zaidi ya yote utakuta enzi za kampeni ulikuwa ukitoka jasho mpaka masikioni wakati ukiimba "CCM mbele kwa mbele" mbaya zaidi ulikuwa mbishiiii hutaki kusikia wala kuambiwa kwa Magufuli!
Usitake kujifanya kujipa moyo eti serikali itakuwa sikivu na kuwa makini katika swala hilo. Ukiwa unajipa moyo kuhusu hilo ukumbuke yule mwanao wa UDOM aliyepata Div. Two na sasa umempeleka Kleruu kusomea upya certificate ya ualimu daraja la kwanza baada ya muda kupotea na matumaini kuanza upya. Pia wakati ukijipa moyo kuhusu hilo ujiulize ni mangapi ambayo serikali hii imeyaingilia na kuyafanya kwa usahihi (Sakata la sukari? Makodi? UDOM? Lipo lingine? )
Ni hivi: Karibia nusu ya wanafunzi wote wanaoendelea na masomo yao ya elimu ya juu watasitishiwa kupewa mikopo na hela ya kujikimu kutoka serikalini baada ya serikali kutoa siku nne tu kwa vyuo vyote nchini kupeleka taarifa zote za wanafunzi wao wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ili kuanza uhakiki rasmi ili kuwachuja rasmi wale wanaoitwa "wasiostahili kusomeshwa na serikali ambao waliingia kwa bahati mbaya"