Yono Auction Mart yafungiwa, Merry chrismass

2015ready

JF-Expert Member
Feb 15, 2011
372
130
Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki(pichani) ameiagiza Halmashauri ya jiji hilo kuchukua hatua za haraka, kuziondoa kampuni zote udalali zinazokamata magari yanayovunja sheria za maegesho jijini humo.

Kauli hiyo ya Sadiki inakuja wakati kuna ongezeko la malalamiko ya wamiliki wa magari kuhusu kampuni hizo kuendesha vitendo vya unyanyasaji, udhalilishaji, ukatili na usumbufu hasa kwa wanawake huku kiongozi huyo akisema yamejaa ofisini kwake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini humo, Sadiki alizitaja kampuni hizo kuwa ni Mwamkinga Auction Mart, Yono Auction Mart & Co Ltd na Tambaza Auction Mart & General Court Broker of the Tribunal.

“Utendaji wa kampuni hizi umeendelea kuwa kero kwa watumiaji wa barabara licha ya viongozi wa kampuni hizo kupewa maelekezo ya kuboresha huduma zao...Malalamiko niliyoyapokea ni mengi, hatuwezi kuvumilia yaendelee,” alisema Sadiki.

Alizitaja baadhi ya kero hizo kuwa ni kukamata magari kwenye nyumba za watu, kuwalazimisha wamiliki wa magari kuvutwa wakati gari linaweza kutembea lenyewe, kufukuza magari yanayodaiwa kuegeshwa vibaya na kusababisha ajali pamoja na kutoza faini viwango tofauti na vilivyoainishwa na halmashauri ya jiji.

“Unakuta magari mazuri na mazima yanavutwa na magari mabovu na kusababisha gari zima kuharibika. Lakini mbaya zaidi, faini halali ni Sh50,000 , wao wanatoza kuanzisha Sh200,000 hadi Sh500,000 . Hii ni kero ambayo hakuna mtu anayekubali.

Hata hivyo, kukamata magari kwa kuvizia mtu akiwa labda amepaki ananunua dawa au hata kushusha mgonjwa, wizi wa vifaa vya magari kwa baadhi ya magari yanayokamatwa... “Mtu anakamatiwa Kimara au Mwenge lakini anavutwa kupelekwa katika yadi yao Pugu au Kurasini, hii haivumiliki,” alisema Sadiki .

Aliongeza: “Wafanyakazi wa kampuni hizo wengi hawana weledi na wanafikiri mtu akishakuwa ‘baunsa’ anafaa na kwamba sehemu kubwa wamekuwa wakiwanyanyasa watu na kuwadhalilisha wanawake ambao hawawezi kupambana nao.”

Sadiki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Dar es Salaam alisema kuwa Halmashauri za Ilala, Kinondoni na Temeke zitachukua nafasi ya kampuni hizo hadi utaratibu mwingine utakapofuata.

“Nazishauri Halmashauri za Ilala, Temeke na Kinondoni kuigia mkataba na Kampuni ya Ulinzi ya Suma JKT ambao vijana wake wanaandaliwa kwa weledi na kufuata sheria za kijeshi na kuachana na wanaookotwa wasikokujua,” alisema.

Huku akisisitiza Sadiki alisema: “Ninawaomba radhi sana wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwa matatizo yaliyokuwa wakiwakuta kutokana na kampuni hizo kuendesha mambo wanavyojua wao, licha ya kuwakemea mara tatu.”
 
Safi sana..........wapite mikoa yote........
halafu niulize.......FAIDA YAO NI NINI........?.........
 
Hizi kampuni ***** zao.kuna siku walinivizia pale kariakoo,nilichowafanya kila mtu alinipa pongezi.Bado wale wa Arusha nawalia timing nikienda kuhesabiwa
 
Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki(pichani) ameiagiza Halmashauri ya jiji hilo kuchukua hatua za haraka, kuziondoa kampuni zote udalali zinazokamata magari yanayovunja sheria za maegesho jijini humo.

Kauli hiyo ya Sadiki inakuja wakati kuna ongezeko la malalamiko ya wamiliki wa magari kuhusu kampuni hizo kuendesha vitendo vya unyanyasaji, udhalilishaji, ukatili na usumbufu hasa kwa wanawake huku kiongozi huyo akisema yamejaa ofisini kwake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini humo, Sadiki alizitaja kampuni hizo kuwa ni Mwamkinga Auction Mart, Yono Auction Mart & Co Ltd na Tambaza Auction Mart & General Court Broker of the Tribunal.

"Utendaji wa kampuni hizi umeendelea kuwa kero kwa watumiaji wa barabara licha ya viongozi wa kampuni hizo kupewa maelekezo ya kuboresha huduma zao...Malalamiko niliyoyapokea ni mengi, hatuwezi kuvumilia yaendelee," alisema Sadiki.

Alizitaja baadhi ya kero hizo kuwa ni kukamata magari kwenye nyumba za watu, kuwalazimisha wamiliki wa magari kuvutwa wakati gari linaweza kutembea lenyewe, kufukuza magari yanayodaiwa kuegeshwa vibaya na kusababisha ajali pamoja na kutoza faini viwango tofauti na vilivyoainishwa na halmashauri ya jiji.

"Unakuta magari mazuri na mazima yanavutwa na magari mabovu na kusababisha gari zima kuharibika. Lakini mbaya zaidi, faini halali ni Sh50,000 , wao wanatoza kuanzisha Sh200,000 hadi Sh500,000 . Hii ni kero ambayo hakuna mtu anayekubali.

Hata hivyo, kukamata magari kwa kuvizia mtu akiwa labda amepaki ananunua dawa au hata kushusha mgonjwa, wizi wa vifaa vya magari kwa baadhi ya magari yanayokamatwa... "Mtu anakamatiwa Kimara au Mwenge lakini anavutwa kupelekwa katika yadi yao Pugu au Kurasini, hii haivumiliki," alisema Sadiki .

Aliongeza: "Wafanyakazi wa kampuni hizo wengi hawana weledi na wanafikiri mtu akishakuwa ‘baunsa' anafaa na kwamba sehemu kubwa wamekuwa wakiwanyanyasa watu na kuwadhalilisha wanawake ambao hawawezi kupambana nao."

Sadiki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Dar es Salaam alisema kuwa Halmashauri za Ilala, Kinondoni na Temeke zitachukua nafasi ya kampuni hizo hadi utaratibu mwingine utakapofuata.

"Nazishauri Halmashauri za Ilala, Temeke na Kinondoni kuigia mkataba na Kampuni ya Ulinzi ya Suma JKT ambao vijana wake wanaandaliwa kwa weledi na kufuata sheria za kijeshi na kuachana na wanaookotwa wasikokujua," alisema.

Huku akisisitiza Sadiki alisema: "Ninawaomba radhi sana wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwa matatizo yaliyokuwa wakiwakuta kutokana na kampuni hizo kuendesha mambo wanavyojua wao, licha ya kuwakemea mara tatu."
Umeripoti Vizuri ila unaonekana kuwa na Chuki na YONO
Maoni yangu kwa RC:
1.Suala la rushwa lipo sehemu zote , Polisi wamefundishwa Vizuri sana lakini angalia wanavyokamata magari hovyo na kuchukua Rushwa . Hata hao SUM JKT nao watapokea Rushwa tu??. RC Serikali unayoingoza nayo imepkea rushwa Escrow Mkuu wa nchi anasua sua kuchukua maamzi.
2.Wanamgambo wa Jiji ambao walikuwa Chini yako nao wamekuwa wanapokea Rushwa sasa tatizo hili litaisha ???
Wananchi wana angamia
 
Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki(pichani) ameiagiza Halmashauri ya jiji hilo kuchukua hatua za haraka, kuziondoa kampuni zote udalali zinazokamata magari yanayovunja sheria za maegesho jijini humo.

Kauli hiyo ya Sadiki inakuja wakati kuna ongezeko la malalamiko ya wamiliki wa magari kuhusu kampuni hizo kuendesha vitendo vya unyanyasaji, udhalilishaji, ukatili na usumbufu hasa kwa wanawake huku kiongozi huyo akisema yamejaa ofisini kwake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini humo, Sadiki alizitaja kampuni hizo kuwa ni Mwamkinga Auction Mart, Yono Auction Mart & Co Ltd na Tambaza Auction Mart & General Court Broker of the Tribunal.

“Utendaji wa kampuni hizi umeendelea kuwa kero kwa watumiaji wa barabara licha ya viongozi wa kampuni hizo kupewa maelekezo ya kuboresha huduma zao...Malalamiko niliyoyapokea ni mengi, hatuwezi kuvumilia yaendelee,” alisema Sadiki.Aliongeza: “Wafanyakazi wa kampuni hizo wengi hawana weledi na wanafikiri mtu akishakuwa ‘baunsa’ anafaa na kwamba sehemu kubwa wamekuwa wakiwanyanyasa watu na kuwadhalilisha wanawake ambao hawawezi kupambana nao.”

“Nazishauri Halmashauri za Ilala, Temeke na Kinondoni kuigia mkataba na Kampuni ya Ulinzi ya Suma JKT ambao vijana wake wanaandaliwa kwa weledi na kufuata sheria za kijeshi na kuachana na wanaookotwa wasikokujua,” alisema.Kabla hajabeteka na hao Suma JKT akafanye kwanza utafiti na hasa sehemu ndogo tu pale FERI KWENYE PANTONI,VIJANA HAO HAWANA TOFAUTI NA HIZO KAMPUNI.
Hao vijana wamegeuka kuwa kila kitu-Polisi,Trafiki,mabaunsa-(Unyanyasaji)

Matatizo hayo yanapanuka kwa sababu ya Rushwa ndani ya Polisi ,Mahakama na Halmashauri zinazotakiwa kusimamia hayo Makampuni.

Namshauri Mkuu wa Mkoa kama Kiranja wa hizi hamashauri katika ofisi yake na hata kwa kupitia Sekretarieti yake au kuwa na ofisa ndani ya Ofisi yake moja moja anayeshughukia Malalamiko na kuwe mfumo rasmi wa kupokea taarifa hasa kutumia ;simu ,e-mail adress ,whataps,facebook acc ambayo wakaazi /wananchi wanaweza kufikisha Malalamiko yao na yeye kuyashughulikia kwa kuwajibisha watendaji husika itakapodhihirika .
 
Umeripoti Vizuri ila unaonekana kuwa na Chuki na YONO
Maoni yangu kwa RC:
1.Suala la rushwa lipo sehemu zote , Polisi wamefundishwa Vizuri sana lakini angalia wanavyokamata magari hovyo na kuchukua Rushwa . Hata hao SUM JKT nao watapokea Rushwa tu??. RC Serikali unayoingoza nayo imepkea rushwa Escrow Mkuu wa nchi anasua sua kuchukua maamzi.
2.Wanamgambo wa Jiji ambao walikuwa Chini yako nao wamekuwa wanapokea Rushwa sasa tatizo hili litaisha ???
Wananchi wana angamia

Wacha wale Wengine sasa Yono wamekula sana wamewatesa sana watu, kila Mtu anakula kwa wakati wake.
 
Hao ni wanyanyasaji balaa hasa ndg zetu wa bodaboda, receipt ndo geti pass
 
Umeripoti Vizuri ila unaonekana kuwa na Chuki na YONO
Maoni yangu kwa RC:
1.Suala la rushwa lipo sehemu zote , Polisi wamefundishwa Vizuri sana lakini angalia wanavyokamata magari hovyo na kuchukua Rushwa . Hata hao SUM JKT nao watapokea Rushwa tu??. RC Serikali unayoingoza nayo imepkea rushwa Escrow Mkuu wa nchi anasua sua kuchukua maamzi.
2.Wanamgambo wa Jiji ambao walikuwa Chini yako nao wamekuwa wanapokea Rushwa sasa tatizo hili litaisha ???
Wananchi wana angamia
vipi mkuu na wewe ndio walewale nini?
 
https://jamii.app/JFUserGuide these dogs hawa mbwa wametesa sana watu hapa mjini ni ningekuwa mchawi ningeshawapiga vipapai wote wanasumbua sana watu
 
Tutapumua kidogo lakini suala la rushwa kusema kweli limezidi hii nchi na hadi sasa sielewi kwanini watu hawaoni jinsi TAKUKURU wanavyo under perform.
 
Hizi kampuni ***** zao.kuna siku walinivizia pale kariakoo,nilichowafanya kila mtu alinipa pongezi.Bado wale wa Arusha nawalia timing nikienda kuhesabiwa
mkuu uliwafanyaje?!au uliwalipa hela pale pale kuonesha jeuri ya fedha!
 
dar es salaam. Mkuu wa mkoa wa dar es salaam, said meck sadiki(pichani) ameiagiza halmashauri ya jiji hilo kuchukua hatua za haraka, kuziondoa kampuni zote udalali zinazokamata magari yanayovunja sheria za maegesho jijini humo.

Kauli hiyo ya sadiki inakuja wakati kuna ongezeko la malalamiko ya wamiliki wa magari kuhusu kampuni hizo kuendesha vitendo vya unyanyasaji, udhalilishaji, ukatili na usumbufu hasa kwa wanawake huku kiongozi huyo akisema yamejaa ofisini kwake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini humo, sadiki alizitaja kampuni hizo kuwa ni mwamkinga auction mart, yono auction mart & co ltd na tambaza auction mart & general court broker of the tribunal.

"utendaji wa kampuni hizi umeendelea kuwa kero kwa watumiaji wa barabara licha ya viongozi wa kampuni hizo kupewa maelekezo ya kuboresha huduma zao...malalamiko niliyoyapokea ni mengi, hatuwezi kuvumilia yaendelee," alisema sadiki.

Alizitaja baadhi ya kero hizo kuwa ni kukamata magari kwenye nyumba za watu, kuwalazimisha wamiliki wa magari kuvutwa wakati gari linaweza kutembea lenyewe, kufukuza magari yanayodaiwa kuegeshwa vibaya na kusababisha ajali pamoja na kutoza faini viwango tofauti na vilivyoainishwa na halmashauri ya jiji.

"unakuta magari mazuri na mazima yanavutwa na magari mabovu na kusababisha gari zima kuharibika. Lakini mbaya zaidi, faini halali ni sh50,000 , wao wanatoza kuanzisha sh200,000 hadi sh500,000 . Hii ni kero ambayo hakuna mtu anayekubali.

Hata hivyo, kukamata magari kwa kuvizia mtu akiwa labda amepaki ananunua dawa au hata kushusha mgonjwa, wizi wa vifaa vya magari kwa baadhi ya magari yanayokamatwa... "mtu anakamatiwa kimara au mwenge lakini anavutwa kupelekwa katika yadi yao pugu au kurasini, hii haivumiliki," alisema sadiki .

Aliongeza: "wafanyakazi wa kampuni hizo wengi hawana weledi na wanafikiri mtu akishakuwa ‘baunsa' anafaa na kwamba sehemu kubwa wamekuwa wakiwanyanyasa watu na kuwadhalilisha wanawake ambao hawawezi kupambana nao."

sadiki ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa dar es salaam alisema kuwa halmashauri za ilala, kinondoni na temeke zitachukua nafasi ya kampuni hizo hadi utaratibu mwingine utakapofuata.

"nazishauri halmashauri za ilala, temeke na kinondoni kuigia mkataba na kampuni ya ulinzi ya suma jkt ambao vijana wake wanaandaliwa kwa weledi na kufuata sheria za kijeshi na kuachana na wanaookotwa wasikokujua," alisema.

Huku akisisitiza sadiki alisema: "ninawaomba radhi sana wakazi wa jiji la dar es salaam kwa matatizo yaliyokuwa wakiwakuta kutokana na kampuni hizo kuendesha mambo wanavyojua wao, licha ya kuwakemea mara tatu."

samahani kuandika hivi kwa maandishi makubwa

huyu mkuu wa mkoa ni mnafiki mkuu..... Miezi mitatu iliopita alinukuliwa akitangaza wazi akutakuwa na wahuni wa tambaza watakaokamata pik pik na magari akisema mikataba yao batili imeisha muda

nilitamani kuona kama mkuu wa mkoa yuko dar na si singida anaingiaje mjini bila kuona wale wahuni wa tambaza wakisukuma watu na pik pi k zao...leo nimekuta pale vingunguti wanamsumbua mtu kaweka pembe tatu gari imearibika ati walete break down kama si jamaa kupiga kelele wanataka kumuibia na wamefukuzwa wasiendelee na watu walipoona tu watu wamejaa wakakimbia

mbaya kuna polisi ndani so sad
 
Kuna siku ningepata kesi ya mauaji kisa hawa mbwa wanyanyasaji sn!!!big up mecky
 
Back
Top Bottom