Kleptomaniacs
Member
- Apr 23, 2008
- 86
- 2
Nimeona ni vyema niliweke hili la huyu bwana Yona hapa JF, ni kwamba kumekuwa na taarifa mbalimbali zenye utata kuhusu kukamatwa kwa bwana Yona Fares Maro na polisi, kwa mujibu wa email iliyotumwa katika address ya wanazuoni ambao ni mtandao ama group email aliyokuwa akichangia mara kwa mara alikamatwa Jnne na taarifa hiyo ilitumwa kupitia simu yake kwa mmoja wa rafiki zake ambaye pia ni mwanachama wa kundi hilo la wanazuoni! kwa mujibu wa maelezo ambayo bila shaka si vibaya nikaya ambatanisha hapa yanasomeka kama ifuatavyo;
''Ndg wanazuoni
Habari zilizonifikia Muda mfupi uliopita zinasema kuwa Mwanazuoni Yona Maro amekamatwa na polisi tangu jumanne usiku.Kwa bahati mbaya text message iliyonifikia haijasema mahali aliko wala sababu za kukamatwa kwake.Ujumbe huo umenifikia kutoka kwa moja ya namba ambayo huwa natumia kuwasiliana na Yona.Nimejaribu mara kadhaa kupiga namba hiyo ili kuweza kupata undani wa swala hilo bila mafanikio.
Kwa wale waliokaribu sana na Yona kama wanaaltenative number ni vizuri kujaribu kumtafuta ili kuona namna ya kumsaidia.Pia wale walio Dar wanaweza kwa nafasi yao kujaribu kufatilia swala hili kwa ukaribu zaidi
.
Nawatakia kazi njema.'' ( wanazuoni@yahoogroups.com)
Leo hii pia ndugu yake aliyepewa jukumu la kutafuta ukweli katika vituo vya polisi ametuma email nyingine juu ya jitihada za kumtafuta katika vituo tofauti vya polisi kutokuzaa matunda email hiyo inasomeka kama ifuatavyo;
''Wanazuoni,naandika kuwasilisha hatua ambayo nimefikia katika kumtafuta Yona,ninasikitika kuwataarifu kuwa pamoja na jitihada hizi bado hazijazaa matunda.
Nimewasiliana na Central Police wanasema wao hawana majina ya waliotiwa mbaroni lakini hata hivyo nimejaribu pia Oysterbay ambako nako sijapata jibu la uhakika.
Bado naendelea kusubiria feedback toka katika vyanzo mbali mbali ili tuwezejua huyu mwenzetu yuko wapi bila KUJALI AIDHA KATIWA NGUVUNI KWA MAKOSA BINAFSI ama ni kutokana na HARAKATI ZAKE.''
Kwasasa kuna kampeni inayoendelea inaitwa FREE YONA, sasa si vibaya kama kampeni hiyo ikiletwa hapa JF ambako pia bwana Yona amekuwa mchangiaji mkubwa katika kuendeleza hiyo kampeni ya FREE YONA. Wale wenye taarifa za ziada kuhusu huyu bwana wanaweza kuchangia hapa ama namna ya kumpata maana ndio hivyo tena polisi wanadai hawajamkamata kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari.
Nawasilisha.