Yona atoswe baharini ili merikebu isizame

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
735
1,464
Anaandika; Robert Heriel.

Moja ya Visa maarufu kwenye Magombo ya kale ya Kiyahudi ni pamoja na Kisa cha Nabii mdogo aitwaye Yona. Kwa Waislam hujulikana kama Nabii Yunus.

Kwa faida ya wasiomjua Yona. Yona ni Nabii mdogo aliyeishi Kaskazini mwa nchi ya Israel. Baba yake aliitwa Amitai. Yona ambaye ndiye Yunus aliagizwa kwenda Mji Mkubwa wa Ninawi akapige kelele na kuwaonya juu ya maovu yao. Lakini Yona alikaidi, Hakuenda Ninawi bali alifunga Safari ya kwenda Tarshishi kujiepusha na Uso wa Mungu. Usafiri pekee aliokuwa akiutegemea ulikuwa ni Usafiri wa Majini kwa kutumia Merikebu. Hapo ndipo Kiini cha mada yetu kilipo.

Yona alipanda Merikebu na safari ya Tarshishi ilianza. Wakiwa njiani mara upepo mkali na Mawimbi yakaanza kuisuka suka merikebu. Wakati huo Yona alitafuta chimbo akajificha huko na kulala kabisa fofofo. Hahaahaha!! Yona Bhana anachekesha kweli.

Wenzake wanahangaika kupambana na dhoruba ya baharini. Yona anakoroma. Ilifikia hatua wakaamua kupunguza Mizigo kusudi Merikebu/Meli isizame lakini haikufua Dafu. Kumbuka Merikebu hii ilipandwa na watu mbalimbali wakiwemo Wafanyabiashara waliobeba mizigo yao ya biashara kwenda kuiuza mji wa Tarshishi.

Embu fikiria wewe ndiye Mfanyabiashara upo ndani ya Merikebu unaambiwa utupe mizigo yako ili meli isizame. Looh! Hakika inaumiza sana. Pia walikuwepo Abiria wengine huenda ni Waalimu, Matabibu, Waandishi wa Habari na wengineo. Wote sasa kila mmoja anaambiwa atupe mzigo wake baharini. Hahaha! Yaani kama ni Mwalimu ataambiwa atupe Mtaala, Muongozo, na Vitabu. Kama ni Mwanasheria au hakimu ataambiwa atupe mavitabu ya sheria, na Katiba. Waandishi nao wataambiwa tupeni Makamera yenu na magazeti yenu majini huko ili meli isizame.

Na kama ni Wachungaji na mashehe waliambiwa tupeni Biblia na Quran ili meli itulie. Looh! Yona yeye kalala.

Watu wakamkumbuka Yona. Ati mbona Yona kalala huko chimbo wakati sisi tupo katika hali ngumu hivi. Jamani Yona aamshwe. Yona akaamshwa.

Hahaha! Yona kuamshwa ati anapikicha macho na kupiga Miayo. Looh! Yona kweli umevurugwa.
Yaani unapiga miayo wenzako wapo hai hai roho mkononi. Khaah!!.

Kumbuka wasafiri hawa hawajuani. Mara paap! Wakampiga Maswali muhimu; Moja, Kazi yako ni kazi gani? mbili, Umetoka wapi? Tatu, Nchi yako ni nchi Ipi
?. Mwisho, Kabila lako ni lipi?. Yona akabung'aa akajua hapa dili limesanukiwa. Akawajibu.

Sasa wakamtambua. Wakamuogopa. Wakamuuliza kwa hadhari na kwa hofu. ''TUKUTENDE NINI BAHARI ITULIE?''
Akawajibu, ''NIKAMATENI, MNITUPE BAHARINI, NAYO BAHARI ITATULIA. akamalizia huku akipiga pikicha macho akiyatazama mawimbi, akasema; Kwa ajili yangu najua ndio maana tufani hii imewapata. Looh!

Napiga picha nami nimo ndani ya Merikebu. Huenda mimi ni Mfanyabiashara na tayari mizigo yangu imetupwa baharini. Alafu punde Anakuja mtu anasema kuwa hasara niliyoipata ni kwa sababu yake. Embu na wewe nisaidie kupiga picha hapo alafu utaelewa Wale wasafiri muda ule walikuwa wanamtazamaje Yona.

Kitu pekee kinachokuja kwenye akili yangu ni kuwa, tayari Yona anajua yeye ni chanzo cha ile Tufani. Pia Wasafiri wenzake nao wameshamjua Yona ndio chanzo cha wao kupatwa na Mabaya yale. Chanzo cha wao kutupa mizigo yao. Biashara zao. Nguo zao. Zawadi zao. Na kila aina ya mizigo. Lakini nilichokigundua ni kuwa Yona hana Ujasiri wa Kujitupa mwenyewe Baharini. Anaomba Msaada wa Kutupwa na Wasafiri wenzake.

Hii inaniambia yakuwa Watu kama wakina Yona kamwe usisubiri ajitupe mwenyewe Baharini kwani hawawezi kufanya hivyo. Watu kama kina Yona ni kuwatosa tuu Baharini.

Basi Wakamtupa Yona Baharini na muda ule ule Bahari ikatulie. Kumbe wangejua muda mrefu kuwa chanzo cha maswahibu na Mabaya yote ni Yona wasingetupa Mizigo yao. Wasingetupa Nguo zao. Biashara zao. Kamera zao wasingezitupa. Vitabu vyao na mizigo mingine. Wangemtupa tuu huyo Yona.

Najifunza katika kisa hiki kuwa Endapo Yona akitoswa Baharini basi bahari inatulia. Ukiona umemtupa Mtu lakini bado majanga yanaendelea ujue umemtupa asiye sahihi.

Huu ni wakati wa Kumtupa Yona baharini. Yona anagharimu wafanyabiashara kutupa biashara zao baharini. Yona anagharimu watu kutupa mitaji yao baharini. Yona akitupwa Baharini Biashara haitatupwa baharini. Watu hawatatupa mitaji majini.

Huwezi Safiri na Yona kwenye merikebu alafu biashara yako ikakaa poa. Ukimuonea huruma Yona basi kubali na usilalamike Uonapo biashara yako ikitupwa baharini.

Huu ni wakati wa Kumtosa Yona Baharini Vinginevyo Wakulima waliomo Kwenye Merikebu watazidi kutupa mazao yao na mbegu zao baharini. Mkulima huwezi safiri pamoja na Yona kwenye Merikebu alafu mazao yako yakabaki salama. Lazima yatupwe baharini. lazima mbegu zitupe baharini. looh! Yona bhana.

Wakati ni sasa wa Kumtupa Yona Baharini ili Ndoa yako ibaki salama. Ili wewe Binti uolewe na kijana uoe lazima Yona atoswe baharini. Vinginevyo Mahari na Zawadi ulizobeba kwenda ukweni zitupwe baharini. Mtaji na faida ya biashara yako ulioubeba kurudi nyumbani utupwe baharini. Je Mkeo atakuelewa ukifika? Ati umwambie Faida na mshahara wote niliutupa baharini kwa sababu ya Yona. Mkeo au mumeo atakuelewa. Tupa Yona Baharini acha kuvunja ndoa kisa Yona.

Yona yeye haoni tufani kwani kalala huko chimboni. Wewe upo juu ya Merikebu unamtolea Maji yanayoingia kwenye Merikebu. Unapandisha na kuliweka vizuri Tanga ili likabiliane vizuri na upepo. Yeye Yona kambonji. Haha! Nacheka kama mazuri.

Kijana unahangaika kutafuta kazi ya kuajiriwa au kujiajiri huko ndiko kutoa maji kwenye Merikebu. Unajua hayo maji unayoyatoa yasingeingia kama sio Yona. Yona ndiye kaleta tufani iliyoingiza maji ndani ya Merikebu ona sasa inazama. Yeye kalala kazi kupiga miayo na kukoroma tuu. Tena anakoroma kama simba. Yeye kutoa Maji hataki wakati yeye ndiye chanzo cha tufani. Looh! Embu mtoseni Yona Baharini msimkawize atazidi kuleta madhara.

Unajua Yona ni kweli alitumwa na Mungu lakini alichokosea ni Kupanda Merikebu yenu wakati yeye haelekei ninyi mnakoelekea. Yeye aliagizwa kwenda Ninawi alafu akapanda Merikebu yenu iendayo Tarshishi. Kwani ndiko alikotumwa.

Sasa Matokeo yake ndio hayo Sasa. Utaona watu wanakufa bila sababu kisa ni Yona. Wanavamiwa na Kutekwa kisa ni Yona. Yona Hicho sicho ulichoagizwa na Mungu. Na kwa vile unakimbia Uso wa Mungu basi Lazima utoswe Baharini.

Hata katika Taifa wapo wakina Yona wengi. Sifa za Yona zinajulikana. Ukiona mtu anatoswa baharini kwenye taifa na bahari haitulii ujue huyo hakuwa Yona. Yona bado yupo Merikebuni. Ukiona mtu kauawa au kafungwa au katekwa lakini Bahari haitulii ujue huyo hakuwa Yona. Yona bado yupo kwenye Merikebu. Yona amelala anakoroma kama simba. Tena ukimuamsha atapiga miayo sura yake akiwa ameikunja na macho yakiwa mekundu.

Yona ukimuuliza yeye ni nani. Atakujibu na lazima utaogopa kwa kuwa wasifu wake si haba. Lakini Usimuogope mtose Baharini uone kama Bahari haitatulia.

Wakati ni Sasa. Yona atoswe Baharini Merikebu ipate kutulia. Wasafiri roho zao zipumzike. Looh!

Kumbuka kamwe Usidhani kuwa Yona atajitosa mwenyewe Baharini. Yona hatofanya hivyo asilani. Mkamateni, mumtupe Baharini, Nayo bahari itatulia.

Taikon Nimemaliza mwenye maswali aweza kuuliza. Ila Majibu yangu yanaweza kumtatiza.

Robert Heriel
Taikon Wa Fasihi.
 
Yona ana jenga chato huku Sehemu kubwa ya wananchi wa taifa lake wakiwa Wanaishi katika mazingira haya

huwezi%2Bkujua.JPG
hospitali.jpeg
18_Children%252520Jinja%252520suburb.jpeg
 
Yona yona akaangamiza watu wa kila aina jamani.Nani awe wakwanza kumshika mguu Yona ili kumzamisha bahari?? Makundi yote yanatamani iwe hivi, shida ni shujaa nani ajivue huruma na uwoga kama aliyonao Yona aliyehukumiwa pasipo makosa kwa lengo la kuondoa hii tufani ya bahari ili iwe shwari kwa lazima na sio kudra na uwezo wa mwenyezi mungu??. Kama waliomteua na kumtuma kazi hii hawaoni madhila ya shida wazipatazo walio kwenye Merikebu!! basi ni wakati wa wao kuomba merikebu izame ili wafe wote na Yona.
 
64 Reactions
Reply
Back
Top Bottom