Yona agombana na Wamarekani

PELE

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
229
12
Mwandishi Wetu
Machi 24, 2010


bul2.gif
Yumo Balozi wa zamani wa Marekani Charles Stith
bul2.gif
Ni kuhusu mradi wa nyumba Kunduchi, Dar


FAMILIA ya aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini katika Serikali ya Awamu ya Tatu, Daniel Yona, iko katika mvutano unaomhusisha aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini, Mchungaji Charles Stith. Katika mvutano huo, Serikali ya Tanzania imeshtuka dakika za mwisho, ikishangaa na kuahidi kuchukua hatua stahili, Raia Mwema imebaini.

Mvutano huo unahusisha moja kwa moja kundi la wawekezaji wa Marekani waliokuwa tayari kuwekeza mamilioni ya dola nchini katika mradi wa ujenzi wa nyumba nafuu, kwa makubaliano mahsusi na kampuni ya Yona.

Yona, ambaye kwa sasa anashitakiwa katika Mahakama ya Kisutu kwa tuhuma za kutumia vibaya madaraka alipokuwa Waziri, amejikuta katika mvutano baada ya kutaka kujitoa katika makubaliano ya uuzaji wa eneo kwa kampuni ya Kimarekani ya Enterprises Homes Tanzania Ltd (EHTL).


Kampuni ya Yona inayoitwa Devconsult International Ltd iliingia mkataba na Enterprises Homes Tanzania Ltd kuuza ardhi yenye hati namba (Plot No). 384, Block ‘A’ Kunduchi kwa bei ya Dola za Marekani 650,000 (zaidi ya Sh milioni 650).


Lengo la EHTL kwa kushirikisha wadau wengine ni kufanikisha ujenzi wa awali wa nyumba 45 za gharama nafuu, ambazo ni sehemu ya ujenzi wa nyumba nafuu mpya 5,000 utakaokamilika mwaka 2012.

Mradi huo wa aina yake unalenga kusaidia ndoto ya Serikali kuwapatia wananchi makazi bora ya gharama nafuu, lakini habari zinasema kampuni iliyokusudia kununua ardhi hiyo kwa familia ya Yona, ilishindwa kutimiza masharti ya mkataba wa awali ikiwa ni pamoja na kulipa fedha kabla ya kukabidhiwa eneo husika.


Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, mfadhili wa mradi huo kupitia EHTL ni kampuni binafsi ya Marekani, Overseas Private Investment Corporation (OPIC), pamoja na taasisi nyingine za fedha zikiwamo Benki ya Eurafrican Bank na taasisi ya mikopo Ghana.


Kila nyumba ilipangwa kugharimu dola za Marekani 100,000 (zaidi ya Sh milioni 100) au pungufu ya kiwango hicho. Mkataba wa mkopo wa kuuziwa nyumba hiyo kwa mlalahoi wa Tanzania utadumu kwa miaka 15.

Hata hivyo, hivi karibuni Devconsult iliamua kujitoa katika mpango huo na hivyo kuhatarisha malengo yaliyokusudiwa, baada ya kampuni hiyo ya kina Yona kushindwa kuwashawishi wawekezaji hao kulipa fedha husika kwa mujibu wa mkataba.


Lakini pamoja na kitisho hicho, Wawekezaji wa Marekani wenye malengo hayo bado hawajakata tamaa isipokuwa wamekuwa wakifanya kampeni wakidai kwamba ni vigumu kuendesha shughuli za kiuwekezaji nchini Tanzania bila kueleza ukweli kwamba walishindwa kulipa fedha kwa wakati kama walivyokubaliana katika mkataba.


Taarifa kutoka kwa wawekezaji hao zinabainisha kuwa wana matumaini familia ya Yona itarejea katika mpango huo ili hatimaye kuufanikisha, huku kukiwa na taarifa za suala hilo sasa huenda likaingia katika mkondo wa kimahakama.

Habari zaidi zinasema kwamba mbali ya kuwa familia ya Yona kutaka kuuza eneo hilo, mmoja wa wanafamilia naye aliingizwa katika kampuni hiyo ya Wamarekani kama mwana hisa kwa nia ya kufanikisha malengo ya ujenzi wa nyumba hizo huku kukiwa na watu wengine maarufu nyuma yao.


Wakati mvutano huo ukiendelea, takwimu nchini hasa za Benki Kuu zinabainisha kuwa mahitaji ya nyumba bora Tanzania yemefikia nyumba milioni 2.


Dar es Salaam pekee, wastani wa mahitaji ya viwanja kwa ajili ya ujenzi ni 20,000 lakini uwezo wa utoaji kwa mwaka ni 700, na hivyo takriban asilimia 97 ya mahitaji hayatekelezwi.

Kuhusika kwa Balozi Charles Stith


stith_1.jpg

Balozi Charles Stith

Balozi Stith, ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti na Kumbukumbu za marais wa Afrika (APARC), kilichoko katika Chuo Kikuu cha Boston, Marekani ndiye Mwenyekiti wa Enterprises Homes Tanzania Ltd.

Balozi huyo wa zamani wa Marekani nchini, wakati wa utawala wa Rais Bill Clinton, amewahi kuuelezea mradi huo kuwa ni ukombozi kwa Watanzania wenye uwezo mdogo kiuchumi kumiliki makazi.

“Suala hili la mkopo nafuu wa nyumba utawanufaisha Watanzania wengi na kujiona ni wadau wa kweli katika maendeleo ya nchi yao.

“Hiki tunachofanya ni mapinduzi makubwa katika umiliki wa makazi katika hii nchi (Tanzania),” anasema Balozi Stith akizungumzia mradi huo.

Shirika la Overseas Private Investment la Marekani (OPPIC) ambalo ndilo mfadhili wa mradi huo ni wakala wa Serikali ya Marekani ulioanzishwa kwa lengo la kukusanya na kuwezesha mitaji na maarifa kutoka nchini Marekani kuwekezwa kwa kushirikisha wadau wengine katika nchi mbalimbali duniani.

Msimamo wa kigogo wa EHTL

Akizungumzia sakata hili, mmoja wa viongozi wa kampuni ya Enterprises Homes Tanzania Ltd (EHTL), Kyle McKinney anasema hakuna sababu za kujitoa au kusitisha mpango huo kwa kuwa umefikia hatua za mwisho na tayari wafadhili kadhaa wameridhia kusaidia.

Kwa mujibu wa McKinney, wakati Benjamin Mkapa (akiwa Rais) alifika Marekani Septemba 1999 na kuipigia debe Tanzania kama moja ya nchi nzuri za kuwekeza katika Afrika, akitaka wawekezaji wa kigeni wakiwamo Wamarekani kuwekeza Tanzania.

“Pamoja na kikwazo hiki bado tuna nia ya kuendelea na mradi lakini kama Bw. Yona (Daniel) na kampuni yake watatii masharti ya mkataba na kukubali kubadilisha hati ya umiliki katika Wizara ya Ardhi,” anasema McKinney.

Mkono wa Daniel Yona

Waziri huyu wa zamani wa Nishati na Madini, Yona anahusika moja kwa moja na barua yake ya Desemba 8, mwaka 2009 inathibitisha.

Katika barua hiyo Daniel Yona, anamweleza Sadock Maggai wa kampuni ya uwakili ya IMMMA (IMMMA advocates) ambaye kwa wakati huo alikuwa mwakilishi wa EHTL, kwamba; makubaliano (uuzaji ploti ya Oktoba 23, 2006) kati ya kampuni mbili (Devconsult International Ltd na Enterprises Homes Tanzania Ltd) yamesitishwa na kampuni ya Devconsult.

Yona katika barua hiyo anasema; “makubaliano yamesitishwa na kwa hivyo anaomba kurejeshewa nyaraka zote kutoka Enterprises Homes Tanzania Ltd-EHTL.

Lakini katika majibu yake kwa barua hiyo ya Yona, Maggai ambaye ni wakili alifafanua kuwa EHTL haiko tayari kurejesha nyaraka yoyote ambazo ndiyo msingi wa makubaliano kati ya kampuni hizo na kwa maana hiyo, kuna mkataba wa kisheria kati ya kampuni hizo mbili.

Taarifa zaidi zinabainisha kuwa baadaye Wakili Maggai alijitoa katika jukumu la kumwakilisha mteja wake (EHTL) kwa madai ya kuwapo kwa mgongano wa maslahi kati yake na Yona (familia).

yona_1.jpg


Waziri wa Nishati na Madini katika Serikali ya Awamu ya Tatu, Daniel Yona

Alipoulizwa kuhusu mvutano huo, Daniel Yona alikataa kuzungumza kwa kina akiishia kuweka bayana kuwa uamuzi wa kusitisha makubaliano kati ya kampuni hizo mbili umefanywa na watoto wake na si yeye.

Hata hivyo, mawasiliano mbalimbali yanabainisha kuwapo kwa utata ikidhihirika kuwa Yona ndiye amekuwa akitoa baraka zote katika kusitisha mkataba huo kupitia wanawe.

Kiini cha mvutano chaanzia BoT

Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha kuaminika nchini, uamuzi wa kusitisha makubaliano yaliyofikiwa umetokana na sababu kuu mbili.

Kwanza, ni mtihani wa kisheria (kesi yake mahakamani) ambao Yona kwa sasa anapambana nao na pili, mapendekezo mapya mradi wa ujenzi wa nyumba wa Benki Kuu, ambao utahusisha takriban dola za Marekani milioni 40 (zaidi ya Sh bilioni 40).

Kampuni na taasisi binafsi za Tanzania zinatarajiwa kunufaika na fungu hilo la fedha na hasa zinazojihusisha na masuala ujenzi.

Chanzo cha kuaminika cha habari, kinafichua siri kubwa ya maandalizi ya ulaji inayohusisha maofisa kadhaa wa Benki Kuu.

Maofisa hao wamejipanga kuandaa washirika wao kibiashara kuanzisha au kutafuta kampuni za masuala ya ujenzi na ardhi, kwa ajili ya kujichotea mabilioni hayo. Mradi huo unaohusisha BoT ulitangazwa rasmi Novemba 14, mwaka 2009.

EHTL yatoa notisi

Tayari EHTL imetoa notisi kwa kushirikiana na OPIC katika kukabili kile kilichoelezwa kuwa “kitisho kutoka kwa Serikali ya Tanzania-Wizara ya Ardhi kuzuia mchakato wa utoaji hati kwa jina la Enterprise Homes Tanzania Limited kwa mujibu wa nyaraka haraka halali zenye sahihi husika.”

Waziri Chiligati ashangaa

Katika maelezo yake kuhusu sakata hili, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati alisema hakuwa na taarifa zozote kuhusu kuwapo kwa mradi huo lakini akiahidi kuwa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete itahakikisha mradi huo unakwamuliwa.
 
Mmoja kati ya wanahisa wa hiyo kampuni ni mtoto wa Daniel Yona, ajulikanaye kama Daniel Yona, Jr
 
I think Tanzania needs some sort of catharsis - physical, verbal, psychological, judicial and all other sorts possible- to get rid of these double-dealing government officials once and for all and start afresh.
 
Uchina huyu Yona na wengine morons wangeshanyongwa.Simple as that!

Nakubaliana nawe kabis; Tanzania tunahitaji a "progressive dictator" ..... kuna wakati hutakiwi kufuata sheria au utaratibu .... kuna watu inabidi wa-face firing squad pale Mnazi Mmoja, saa saba mchana.
 
Ni lini watu watakuwa na kukinai katika msamiati wao?

1. Fursa zinazojitokeza..wa kwanza kujua ni viongozi wetu... ina maana hutumia nafasi zao kwa manufaa yao tu?.... huu nao sio matumizi mabaya ya madaraka?
2. Ina maana viongozi ndio wateule wa kula keki ya taifa wao peke yao tu?
Kila fursa... utaona ni kiongozi, akichomekea huko watu wake( ndugu hasa)

Tufike mahali tuwe na moyo wa kutosheka.... viongozi wana mishahara mikubwa, marupurupu, pension za uhakika.... na bado wanadaka kila kinachoingia... waone haya na wamuogope Mungu!
 
Ubinafsi na ufisadi vimemponza kama wanavyoliponza Taifa zima kwa ubinafsi na ufisadi wao....Ukweli ni kwamba international contracts are always very easy to get in BUT almost IMPOSSIBLE to get out,kazi anayo,bado na mashtaka yetu sisi wananchi,mwisho wa mafisadi slowly but surely uko karibu!
 
Tufike mahali tuwe na moyo wa kutosheka.... viongozi wana mishahara mikubwa, marupurupu, pension za uhakika.... na bado wanadaka kila kinachoingia... waone haya na wamuogope Mungu!

dada watu wanalipizia walichokosa kufanya wakati wa Nyerere. Miaka 20 ya kutoruhusiwa lazima ilipizwe sasa.
 
Yale yale ni sawa na kina Ridhiwani Kikwete jinsi wanavyojitajirisha na makampuni ya kuchimba dhahabu. Tufike mahali tuwasulubishe hawa mafisadi.
 
dada watu wanalipizia walichokosa kufanya wakati wa Nyerere. Miaka 20 ya kutoruhusiwa lazima ilipizwe sasa.

Ndugu yangu.....

Mwisho wa ubaya ni aibu siku zote....
Hata kama ni kulipiza..hizo mali zinazotokana na ujanja tu na siyo hard work sijui kama zinakuletea heshima!
One lesson coming out of this is.....kuna umuhimu wa kupeana zamu..hasa nafasi za juu na kati..siyo watu hao hao tu toka uhuru hadi leo wanafia ofisini kisa kuendelea kupeana ulaji tu hata baada ya kustaafu.

Watanzania wapo wengi sana wenye elimu, akili, maarifa, busara, experience, na uchaji wa Mungu..lakini kama hauko kwenye mitandao ya wenye kugawa nafasi ..utaishia kushangaa tu kama tunavyoshangaa hapa.
 
Ingawaje napinga ufisadi kwa nguvu zote, hapa ukiangalia haki na sheria nadhani kina Yona hawana makosa.

Walikubali kuuza ardhi miaka ya nyuma kwa $650,000, lakini hiyo kampuni ya Balozi ilishindwa kulipa, 3 yrs later wanataka kuanza mradi kwa bei ya ardhi ya 2006, hapo si haki.

Also inaelekea kina Yona wamepata idea au deal nzuri zaidi, kwa hiyo hapa issue ni Mahakamani tu kuangalia masharti ya mkataba ule wa 2006 na kama balozi na kampuni yao walishindwa kulipa, basi mkataba uwe batili na kina Yona wafanye chochote na ardhi yao.

Mambo ya kisiasa hayahusiki kabisa hapo ooh sijui wamarekani sijui yona, No sheria ifuate mkondo wake sababu hii ni personal business agreement na kina chiligati kama wanataka kusaidia watu watoe viwanja vya serikali na sio kuleta maneno mengi.
 
Ingawaje napinga ufisadi kwa nguvu zote, hapa ukiangalia haki na sheria nadhani kina Yona hawana makosa.

Walikubali kuuza ardhi miaka ya nyuma kwa $650,000, lakini hiyo kampuni ya Balozi ilishindwa kulipa, 3 yrs later wanataka kuanza mradi kwa bei ya ardhi ya 2006, hapo si haki.

Also inaelekea kina Yona wamepata idea au deal nzuri zaidi, kwa hiyo hapa issue ni Mahakamani tu kuangalia masharti ya mkataba ule wa 2006 na kama balozi na kampuni yao walishindwa kulipa, basi mkataba uwe batili na kina Yona wafanye chochote na ardhi yao.

Mambo ya kisiasa hayahusiki kabisa hapo ooh sijui wamarekani sijui yona, No sheria ifuate mkondo wake sababu hii ni personal business agreement na kina chiligati kama wanataka kusaidia watu watoe viwanja vya serikali na sio kuleta maneno mengi.

Swali la kujiuliza hata kama ni kwa kuangalia sheria.... ardhi kisheria ni mali ya nani? Mfumo wa sheria za ardhi ulivyo ni kuwa Land is held by the President in trust on behalf of us citizens. What we get is just the Right to occupy it for a number of years..ndio maana kuna leases za 33, 66 and 99 yrs ..ofcourse can be renewed thereafter. Huwezi kuhodhi ardhi which most probably wameitwaa bure kutokana na nafasi zao ili tu u speculate na kuja kuuza kwa mabilioni! 650,000 DOLLARS isnt peanuts eti!..

Sheria inataka upate compensation for unexhausted improvements that you made on the land...most probably hajaweka chochote kwenye hiyo ardhi..sasa anakuwa compensated for what?
Ni wananchi wangapi hawana ardhi hata ya kulima kabustani?
Consider this before defending a cause.
 
Swali la kujiuliza hata kama ni kwa kuangalia sheria.... ardhi kisheria ni mali ya nani? Mfumo wa sheria za ardhi ulivyo ni kuwa Land is held by the President in trust on behalf of us citizens. What we get is just the Right to occupy it for a number of years..ndio maana kuna leases za 33, 66 and 99 yrs ..ofcourse can be renewed thereafter. Huwezi kuhodhi ardhi which most probably wameitwaa bure kutokana na nafasi zao ili tu u speculate na kuja kuuza kwa mabilioni! 650,000 DOLLARS isnt peanuts eti!..

Sheria inataka upate compensation for unexhausted improvements that you made on the land...most probably hajaweka chochote kwenye hiyo ardhi..sasa anakuwa compensated for what?
Ni wananchi wangapi hawana ardhi hata ya kulima kabustani?
Consider this before defending a cause.

Yesu na maria, nkiki?? Yaani sasa unakuja as if huo mradi wa kina Stith una public interest?? Kwani wanajenga hospitali au airport au barabara?? Hii ni personal deal btn 2 companies, usiingize mambo ya public interest sababu hakuna public interest hata moja humo ndani. Kampuni ya kina Stith ni kampuni inayotafuta profit ya hali ya juu na sio NGO kama ambavyo kampuni ya Yona ilivyo also sio NGO, wote ni wafanya biashara na serikali haihusiki hata kidogo kuingilia, sehemu ya kwenda ni mahakamani ONLY.
 
Moelex wenye tatizo ni kina Yona.. ili kukamilisha dili walitakiwa waende ardhi kutransfer certificate of occupancy.. lakini wao wakataka fedha zaidi. Matokeo yake ndiyo haya sasa.
 
WoS,

Nikimiambienit kuwa Watanzania i wavivu na wajanja wajanja mnasema si mzalendo!

Nimekuwa napiga ndoma na baragumu kwa karibu miaka 10 na ushehe kuwa Siasa na Uanasiasa ndio mfumo mpya wa Ujasirimali au wenyewe kwa kimombo wanasema entraprenyuashipu!

Lakini mnasahau kuwa Vigogo na wakubwa wao ni ruksa kuuza ardhi lakini wananchi wengine mnakemewa?

Hivi leo hii jamaa wa kule Kisarawe wakiuza ardhi kuzlish Jatropha si mpaka FFU wataletwa kuwaswaga, lakini Mkuuwa Wilaya akishirikiana na Kamishna wa ardhi kwanza watawanyang'anya wanyonge ardhi kisha kuiuza kwa Mwekezaji kwa bei ya meno ya dhahabu!
 
Moelex wenye tatizo ni kina Yona.. ili kukamilisha dili walitakiwa waende ardhi kutransfer certificate of occupancy.. lakini wao wakataka fedha zaidi. Matokeo yake ndiyo haya sasa.

Mkuu, sio hivyo ninavyoelewa mimi. Since 2006, walitakiwa kulipwa hela zao yaani kuconsumate hiyo sale agreement, ndio transfer ya title deed ingetoa kama formality tu.

You don't believe kwamba walilipwa then wakahold title, sababu kesi ingekuwa mahakamani siku nyingi sana.

Issue ni kuwa baada ya deal kutokwenda popote kwa miaka 3, wakina Yona wamepata shughuli nyingine na ardhi yao, kwa hiyo wanataka kumove on, ndio huyo balozi tapeli analeta za kuleta, kelele magazetini why?? Also sio fair 2010 kutaka kulipa hela za 2006, hell no.

Lakini mimi sababu mwenyewe sihusiki nadhani waende mahakamani tu.

Kilichoniudhi ni hiyo gear kana kwamba mradi una interest na wananchi maskini. Sehemu za kujenga nyumba za bei nafuu ziko nyingi mno Tanzania, waende wizarani watapewa maeneo mengi tu washindwe wenyewe.
 
Ni lini watu watakuwa na kukinai katika msamiati wao?

1. Fursa zinazojitokeza..wa kwanza kujua ni viongozi wetu... ina maana hutumia nafasi zao kwa manufaa yao tu?.... huu nao sio matumizi mabaya ya madaraka?
2. Ina maana viongozi ndio wateule wa kula keki ya taifa wao peke yao tu?
Kila fursa... utaona ni kiongozi, akichomekea huko watu wake( ndugu hasa)

Tufike mahali tuwe na moyo wa kutosheka.... viongozi wana mishahara mikubwa, marupurupu, pension za uhakika.... na bado wanadaka kila kinachoingia... waone haya na wamuogope Mungu!
Na ndio maana wanatuona wote hatuna akili. Kila siku wanasafiri kwenda nje wakitudanganya kwenda kututafutia wawekezaji. Basically wanaowatafuta ni business partners, sio wawekezaji. Hawana uchungu na nchi hii hata kidogo. Ni wao na watoto wao tu, na hili la Yona ni kivuli tu cha nini kinaendelea nyuma ya pazia.Kuna mambo mazito na ya aibu aibu tu kila siku iendayo Tanzania.
 
Back
Top Bottom