Yesu feki aliyezua gumzo Afrika kusini na Kenya afariki dunia

Someni story nzima jamaa mwenyewe kasema hajadai mahali popote kuwa yeye ni Yesu. Tatizo waafrika kukurupuka tu!!! Jamaa alikuwa anaigiza maisha ya Yesu. Jinsi alivyofanana na ile picha ya maisha ya Yesu wakadhani ni yeye. Ukweki ni kuwa yeye ndiye aliyeigiza ile filamu ya maisha ya Yesu. Hebu tujiulize swali "Hivi Yesu anafanan na huyo mu kweli?" Hakuna aliyemwona Yesu akajua alivyo zaidi ya watu kudhani yuko kama yule muigizaji!!!! Soma hii story https://www.foxnews.com/faith-value...sus-imposter-after-visit-to-africa-goes-viral
Mbona tunaipigia picha yake magoti!!!
 
Asas Dairies Ad

NBC Ad

MenuMagazeti AyoTV Top Breaking Mastaa Michezo Mkito Kurasa -Bio -Contact -Matangazo
Millardayo.com



TOP STORIES
Yesu feki aliye-trend Kenya afariki dunia




By
Pascal Mwakyoma TZA
on
August 6, 2019





http://millardayo.com/jsusdhy/#respond
Screen-Shot-2019-08-06-at-3.48.44-AM-660x400.png

Michael Job raia wa Marekani ambaye ni Mhubiri na Muigizaji anayeidaiwa kuwa Yesu feki, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu hospitalini.
Hospitali ya Heyn imethibitisha kifo hicho na wamesema alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa mapafu na amefariki wakati akipatiwa matibabu hospitalini hapo.
Yesu feki alikaribishwa na Wachungaji wawili kutembelea nchini Kenya wiki iliyopita na alikuwa mgeni katika siku ya tamasha la dini ya wakristo nchini humo na kudanganya watu kuwa yeye ni Yesu amerudi kama alivyoahidi.
Wiki iliyopita Serikali ya nchini Kenya ilimuondoa Michael Job na kuwakamata wachungaji hao wawili kwa kosa la kumualika Yesu huyo wa uongo.
 
Hapa kwetu kwa wanaojua sura ya Mwamwindi wamlete anayefanana naye pale Iringa na kusema karudi kukomesha tabia ya dharau ya wakuu wa mikoa.
Kesho yake hukuti mtu ofisi za hawa wakubwa, maana muziki wa Mwamwindi haukuwa wa mchezo!
 
Picha na video zinazomuonyesha mwanamume aliyevaa nguo kama Yesu kristo zimesambazwa pakubwa katika mitandao ya kijamii Afrika.

Lakini jamaa huyu ni nani na anafanya nini?

Ujumbe mmoja katika twitter, uliosambazwa zaidi ya mara 8,000 miongoni mwa wengine na mwanasiasa wa upinzain Afrika kusini Julius Malema, unasema "mchungaji kutoka Afrika kusini amemualika Yesu Kristu kutoka mbinguni kuhubiri kanisani mwake"

Lakini kwa uhalisi picha hizo zimetoka katika hafla iliyofanyika wiki iliyopita katika mji wa Kiserian kiasi ya kilomita 25 kusini magharibi mwa mji mkuu Nairobi nchini Kenya

Mwanamume huyo ni mhubiri kutoka Marekani na muigizaji anayeitwa Michael Job, aliyekuwa anahudhuria misa ya madhehebu mbalimbali ya kikristo ambako alialikwa kuzungumza.

Anaishi Orlando, Florida, ambako amekuwa akiigiza kuwa Yesu katika bustani maalum The Holy Land Experience theme park, inayojitambulisha kama "jumba halisi la biblia la ukumbusho".

Katika video aliyoipakia katika ukurasa wake wa Facebook mwishoni mwa juma, maduka ya kuuza bidhaa za ukulima na samani yanaonekana kwa nyuma - ambayo ndio yanayoonekana pia katika picha zilizosambazwa na kudaiwa kuwa zimepigwa Afrika kusini.

Watu wamekuwa wakifanya mzaha katika mtandao wa Twitter kuhusu picha hizo na namna wachungaji barani Afrika wanapenda kudai kufanya miujiza.

Mojawapo ya ujumbe uliosambazwa katika mablogu unatuhumu kuwa "mchungaji wa Kenya anadai amempata Yesu kristu akitembea mitaani Kenya".

Picha ilioambatana na ujumbe huo kwenye twitter ni ya Bwana Job aliyekuwa anahutubu wiki iliyopita katika kanisa la Pentecostal Evangelistic Fellowship of Africa (Pefa) lililopo mjini Kitengela nje kidogo ya mji mkuu Nairobi.

Katika video za mahubiri aliyokuwa anayotoa Kenya, mchungaji huyo wa Marekani anaahidi miujiza na uponyaji - mambo ambayo ameshtumiwa kwayo katika mitandao ya kijamii.

Hii sio ziara yake ya kwanza barani Afrika, mapema mwaka huu alikuwa nchini Togo, licha ya kwamba picha alizoweka kutoka huko hakuonekana akiwa amevaa mavazi ya kuiga - bali alikuwa amevaa suti.

View attachment 1173531

=======

Jamaa huyu anayejiita yesu feki amefariki leo

Yesu feki aliyetembelea Kenya afariki Dunia

Michael Job raia wa Marekani ambaye ni mhubiri na muigizaji anayeidaiwa kuwa Yesu Feki, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu hospitalini.

Hospitali ya Heyn imethibitisha kifo hicho na wamesema alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa mapafu na amefariki wakati akipatiwa matibabu hospitalini hapo.

Yesu feki alikaribishwa na Wachungaji wawili kutembelea nchini Kenya wiki iliyopita na alikuwa mgeni katika siku ya tamasha la dini ya wakristo nchini humo na kudanganya watu kuwa yeye ni Yesu amerudi kama alivyoahidi.

Wiki iliyopita Serikali ya nchini Kenya ilimuondoa Michael Job na kuwakamata wachungaji hao wawili kwa kosa la kumualika Yesu huyo wa uongo.

Picha na Video zilimuonyesha Michael Job akiwa amevalia mavazi kama ya Yesu wa ukweli zilienea kwa wingi katika mitandao ya kijamii hasa barani Africa.

Chanzo: (EATV)
MUNGU hadhihakiwa,wale fake pastors wajifunze kupitia jambo hili
 
HUYO MTU HAJAFA.SOMA BBC SWAHILI.YUPO HAI NA ALHAMISI ANA MKUTANO HUKO NAKURU KENYA.HABARI YA KIFO CHAKE NI FAKE NEWS.
 
Mambo ya Mungu ayataki mzaa sasa ameenda kukutana nae af amwambie upuuzi aliokua anafanya wa kudanganya watu dunian
 
Nadhani a aweza sasa kukutana na Yesu halisi na kuulizwa swali moja la msingi ambalo ni.
....unakumbuka matendo yako?
 
Back
Top Bottom