Yesu feki aliyezua gumzo Afrika kusini na Kenya afariki dunia

Picha na video zinazomuonyesha mwanamume aliyevaa nguo kama Yesu kristo zimesambazwa pakubwa katika mitandao ya kijamii Afrika.

Lakini jamaa huyu ni nani na anafanya nini?

Ujumbe mmoja katika twitter, uliosambazwa zaidi ya mara 8,000 miongoni mwa wengine na mwanasiasa wa upinzain Afrika kusini Julius Malema, unasema "mchungaji kutoka Afrika kusini amemualika Yesu Kristu kutoka mbinguni kuhubiri kanisani mwake"

Lakini kwa uhalisi picha hizo zimetoka katika hafla iliyofanyika wiki iliyopita katika mji wa Kiserian kiasi ya kilomita 25 kusini magharibi mwa mji mkuu Nairobi nchini Kenya

Mwanamume huyo ni mhubiri kutoka Marekani na muigizaji anayeitwa Michael Job, aliyekuwa anahudhuria misa ya madhehebu mbalimbali ya kikristo ambako alialikwa kuzungumza.

Anaishi Orlando, Florida, ambako amekuwa akiigiza kuwa Yesu katika bustani maalum The Holy Land Experience theme park, inayojitambulisha kama "jumba halisi la biblia la ukumbusho".

Katika video aliyoipakia katika ukurasa wake wa Facebook mwishoni mwa juma, maduka ya kuuza bidhaa za ukulima na samani yanaonekana kwa nyuma - ambayo ndio yanayoonekana pia katika picha zilizosambazwa na kudaiwa kuwa zimepigwa Afrika kusini.

Watu wamekuwa wakifanya mzaha katika mtandao wa Twitter kuhusu picha hizo na namna wachungaji barani Afrika wanapenda kudai kufanya miujiza.

Mojawapo ya ujumbe uliosambazwa katika mablogu unatuhumu kuwa "mchungaji wa Kenya anadai amempata Yesu kristu akitembea mitaani Kenya".

Picha ilioambatana na ujumbe huo kwenye twitter ni ya Bwana Job aliyekuwa anahutubu wiki iliyopita katika kanisa la Pentecostal Evangelistic Fellowship of Africa (Pefa) lililopo mjini Kitengela nje kidogo ya mji mkuu Nairobi.

Katika video za mahubiri aliyokuwa anayotoa Kenya, mchungaji huyo wa Marekani anaahidi miujiza na uponyaji - mambo ambayo ameshtumiwa kwayo katika mitandao ya kijamii.

Hii sio ziara yake ya kwanza barani Afrika, mapema mwaka huu alikuwa nchini Togo, licha ya kwamba picha alizoweka kutoka huko hakuonekana akiwa amevaa mavazi ya kuiga - bali alikuwa amevaa suti.

View attachment 1173531

=======

Jamaa huyu anayejiita yesu feki amefariki leo

Yesu feki aliyetembelea Kenya afariki Dunia

Michael Job raia wa Marekani ambaye ni mhubiri na muigizaji anayeidaiwa kuwa Yesu Feki, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu hospitalini.

Hospitali ya Heyn imethibitisha kifo hicho na wamesema alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa mapafu na amefariki wakati akipatiwa matibabu hospitalini hapo.

Yesu feki alikaribishwa na Wachungaji wawili kutembelea nchini Kenya wiki iliyopita na alikuwa mgeni katika siku ya tamasha la dini ya wakristo nchini humo na kudanganya watu kuwa yeye ni Yesu amerudi kama alivyoahidi.

Wiki iliyopita Serikali ya nchini Kenya ilimuondoa Michael Job na kuwakamata wachungaji hao wawili kwa kosa la kumualika Yesu huyo wa uongo.

Picha na Video zilimuonyesha Michael Job akiwa amevalia mavazi kama ya Yesu wa ukweli zilienea kwa wingi katika mitandao ya kijamii hasa barani Africa.

Chanzo: (EATV)
mkuu Vipi studio mbona hakuna rekodi mpya ?
 
Amesahau farao alikiri nini alivokiona cha mtemakuni bahari ya shamu (GOD IS GOD) watu wengi sana walio mdhihaki MUNGU wsliishia kufa vifo vya aibu kubwa na fedheha. Fanya utani wote lakini sio dhihaka kwa aliekupa pumzi. Cc pumzihaiuzwi.
 
Ha ha ha!!! Ndugu yai!!!!
 
Haha huyo yesu feki anaahidi watu miujiza ya kuwaponya alafu yeye anakufa kwa ugonjwa si ufala huo sasa!? 😂
King Mufasa huyo hakujiita Yesu. Tatizo ni ninyi waswahili kukurupuka. Huyo ni muigizaji tu na ni mwinjilisti aliyealikwa na wainjilisiti wenzie kwenye kanisa moja huko Kenya. Walikuwa wanaigiza maisha ya Yesu ndiyo maana alivaa vile. Watu walivyomuona wakaandika waliyoandika. Pia si kweli kwamba kafariki ni fake newss zote!!! Ukweli ni kuwa yule ni tumishi wa Mungu tu.
 
Amesahau farao alikiri nini alivokiona cha mtemakuni bahari ya shamu (GOD IS GOD) watu wengi sana walio mdhihaki MUNGU wsliishia kufa vifo vya aibu kubwa na fedheha. Fanya utani wote lakini sio dhihaka kwa aliekupa pumzi. Cc pumzihaiuzwi.
Someni story nzima jamaa mwenyewe kasema hajadai mahali popote kuwa yeye ni Yesu. Tatizo waafrika kukurupuka tu!!! Jamaa alikuwa anaigiza maisha ya Yesu. Jinsi alivyofanana na ile picha ya maisha ya Yesu wakadhani ni yeye. Ukweki ni kuwa yeye ndiye aliyeigiza ile filamu ya maisha ya Yesu. Hebu tujiulize swali "Hivi Yesu anafanan na huyo mu kweli?" Hakuna aliyemwona Yesu akajua alivyo zaidi ya watu kudhani yuko kama yule muigizaji!!!! Soma hii story https://www.foxnews.com/faith-value...sus-imposter-after-visit-to-africa-goes-viral
 
King Mufasa huyo hakujiita Yesu. Tatizo ni ninyi waswahili kukurupuka. Huyo ni muigizaji tu na ni mwinjilisti aliyealikwa na wainjilisiti wenzie kwenye kanisa moja huko Kenya. Walikuwa wanaigiza maisha ya Yesu ndiyo maana alivaa vile. Watu walivyomuona wakaandika waliyoandika. Pia si kweli kwamba kafariki ni fake newss zote!!! Ukweli ni kuwa yule ni tumishi wa Mungu tu.
Shukrani kwa ufafanuzi wako bwana Nguto
 
Ni kweli kabisa, na binafsi niliisikiliza sermon yake yote akiwa huko Kenya, alimuhubiri Yesu na wakati huohuo kuigiza aliyoyafanya Yesu yaani uponyaji n.k

Someni story nzima jamaa mwenyewe kasema hajadai mahali popote kuwa yeye ni Yesu. Tatizo waafrika kukurupuka tu!!! Jamaa alikuwa anaigiza maisha ya Yesu. Jinsi alivyofanana na ile picha ya maisha ya Yesu wakadhani ni yeye. Ukweki ni kuwa yeye ndiye aliyeigiza ile filamu ya maisha ya Yesu. Hebu tujiulize swali "Hivi Yesu anafanan na huyo mu kweli?" Hakuna aliyemwona Yesu akajua alivyo zaidi ya watu kudhani yuko kama yule muigizaji!!!! Soma hii story https://www.foxnews.com/faith-value...sus-imposter-after-visit-to-africa-goes-viral
 
Dah! Poor him 😔😔😔 ila huenda ni habari ya uongo hii
 
Michael Job ni muhubiri na muigizaji. Katika kuhubiri kwake huwa wanaigiza maisha ya Yesu na yeye uigiza nafasi ya Yesu. Lengo lao huwa ni kufikisha ujumbe.
Akiwa Kenya walimzushia kwamba yeye anajiita Yesu, akakanusha hizo fake news.
This time waswahili wamezusha kwamba kafa. Lakini ni uzushi.

Mpatapo habari, jaribuni fanya research ndogo walau kupitia google ili msiwe mnaamini kila andiko
 
Back
Top Bottom