Yesu feki aliyezua gumzo Afrika kusini na Kenya afariki dunia

cheusimangala_

Senior Member
Dec 1, 2018
117
250
Picha na video zinazomuonyesha mwanamume aliyevaa nguo kama Yesu kristo zimesambazwa pakubwa katika mitandao ya kijamii Afrika.

Lakini jamaa huyu ni nani na anafanya nini?

Ujumbe mmoja katika twitter, uliosambazwa zaidi ya mara 8,000 miongoni mwa wengine na mwanasiasa wa upinzain Afrika kusini Julius Malema, unasema "mchungaji kutoka Afrika kusini amemualika Yesu Kristu kutoka mbinguni kuhubiri kanisani mwake"

Lakini kwa uhalisi picha hizo zimetoka katika hafla iliyofanyika wiki iliyopita katika mji wa Kiserian kiasi ya kilomita 25 kusini magharibi mwa mji mkuu Nairobi nchini Kenya

Mwanamume huyo ni mhubiri kutoka Marekani na muigizaji anayeitwa Michael Job, aliyekuwa anahudhuria misa ya madhehebu mbalimbali ya kikristo ambako alialikwa kuzungumza.

Anaishi Orlando, Florida, ambako amekuwa akiigiza kuwa Yesu katika bustani maalum The Holy Land Experience theme park, inayojitambulisha kama "jumba halisi la biblia la ukumbusho".

Katika video aliyoipakia katika ukurasa wake wa Facebook mwishoni mwa juma, maduka ya kuuza bidhaa za ukulima na samani yanaonekana kwa nyuma - ambayo ndio yanayoonekana pia katika picha zilizosambazwa na kudaiwa kuwa zimepigwa Afrika kusini.

Watu wamekuwa wakifanya mzaha katika mtandao wa Twitter kuhusu picha hizo na namna wachungaji barani Afrika wanapenda kudai kufanya miujiza.

Mojawapo ya ujumbe uliosambazwa katika mablogu unatuhumu kuwa "mchungaji wa Kenya anadai amempata Yesu kristu akitembea mitaani Kenya".

Picha ilioambatana na ujumbe huo kwenye twitter ni ya Bwana Job aliyekuwa anahutubu wiki iliyopita katika kanisa la Pentecostal Evangelistic Fellowship of Africa (Pefa) lililopo mjini Kitengela nje kidogo ya mji mkuu Nairobi.

Katika video za mahubiri aliyokuwa anayotoa Kenya, mchungaji huyo wa Marekani anaahidi miujiza na uponyaji - mambo ambayo ameshtumiwa kwayo katika mitandao ya kijamii.

Hii sio ziara yake ya kwanza barani Afrika, mapema mwaka huu alikuwa nchini Togo, licha ya kwamba picha alizoweka kutoka huko hakuonekana akiwa amevaa mavazi ya kuiga - bali alikuwa amevaa suti.

fn.png


=======

Jamaa huyu anayejiita yesu feki amefariki leo

Yesu feki aliyetembelea Kenya afariki Dunia

Michael Job raia wa Marekani ambaye ni mhubiri na muigizaji anayeidaiwa kuwa Yesu Feki, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu hospitalini.

Hospitali ya Heyn imethibitisha kifo hicho na wamesema alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa mapafu na amefariki wakati akipatiwa matibabu hospitalini hapo.

Yesu feki alikaribishwa na Wachungaji wawili kutembelea nchini Kenya wiki iliyopita na alikuwa mgeni katika siku ya tamasha la dini ya wakristo nchini humo na kudanganya watu kuwa yeye ni Yesu amerudi kama alivyoahidi.

Wiki iliyopita Serikali ya nchini Kenya ilimuondoa Michael Job na kuwakamata wachungaji hao wawili kwa kosa la kumualika Yesu huyo wa uongo.

Picha na Video zilimuonyesha Michael Job akiwa amevalia mavazi kama ya Yesu wa ukweli zilienea kwa wingi katika mitandao ya kijamii hasa barani Africa.

Chanzo: (EATV)
 

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Sep 16, 2009
9,306
2,000
Michael Job raia wa Marekani ambaye ni Mhubiri na Muigizaji anayeidaiwa kuwa Yesu feki, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu hospitalini, Yesu feki alikaribishwa na Wachungaji wawili kutembelea nchini Kenya wiki iliyopita. #MillardAyoUPDATES https://t.co/D7q8ZkF7VY
 

mshilakule

JF-Expert Member
Jul 13, 2015
271
250
Huenda wanataka baada ya siku tatu wamtangaze huyo feki wao kama amefufuka maana dunia ya sasa uongo umepindukia
 

carter

JF-Expert Member
Jan 23, 2009
3,097
2,000
Amekufa lini huyu? Chanzo kutoka hospital aliyofikiwa na umauti, au ndio tujiandae na sinema mpya? Anaweza fufukia bongo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom