Yesu fake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yesu fake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kaitaba, Oct 16, 2009.

 1. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Taifa moja kubwa linaanda ujio wa Yesu wa bandia, hii inatokana na waumini kusubili kwa muda mrefu kuja kwa yesu na mpaka sasa hajarudi, hivyo basi kuna lijamaa litajitokeza na kutangazwa na vyombo vya habari dunia nzima kuwa ni yesu karudi,

  Tuwe makini......
   
 2. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  hii ni tetesi. weka details ya vvyanzo vyako vya habari. weka wazi nchi. mambo mengine urongo tu. na ww unaweza kuwa unasambaza urongo.
   
 3. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Na hao waumini watakaoamini watakuwa ni wabandia, maana waumini wa kweli wanajua, hakuna ajuaye saa wala siku, na Yesu hatashukua nchi wala mkoa fulani ,atashuka na mawingu na kila jicho litamuona siyo vyombo vya habari vitasema.

  Tuko makini sana sijui wewe?
   
 4. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #4
  Oct 16, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Fuatilia vyombo vya habari hasa vya kidini, kama upo Dar sikiliza Redio wapo, na Prays power Redio kila asubuhi.
   
 5. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0


  Mimi niko makini, ila nahofia wenye imani haba, na wasiojua maandiko, nakupongeza wewe unaelewa maandiko, waelimishe na wengine kama nilivyo fanya mimi.
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Oct 16, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,314
  Likes Received: 22,117
  Trophy Points: 280
  Yesu Mpya Aibuka nchini Urusi, Ana Maelfu ya Wafuasi
  [​IMG]
  Yesu mpya aliyeibuka nchini Urusi, Sergei ToropThursday, September 03, 2009 9:56 AM
  Jamaa wa nchini Urusi amejitangaza kuwa yeye ni Yesu mtoto wa Mungu na amejipatia wafuasi wengi sana nchini humo wanaoamini kuwa yeye kweli ni Yesu. Picha za Yesu huyo mwisho wa habari hii.Akifuga madevu na nywele ndefu, Yesu wa Urusi huzungukwa na wafuasi wake kila anapoenda na amefanikiwa kujikusanyia wafuasi wengi nchini humo na baadhi ya nchi za ulaya.

  Yesu huyo mpya anayeitwa Sergei Torop mwenye umri wa miaka 48, awali alikuwa akifanya kazi kama trafiki polisi kabla ya kuachishwa kazi na baadae kudai kuwa mungu amemtuma kuwaokoa watu.

  Torop amefanikiwa kujikusanyia wafuasi wengi zaidi ya 5,000 wakiwemo wasomi wakubwa nchini Urusi, wasanii na baadhi ya wanasiasa ambao humiminika kwenye kijiji chake cha Petropavlovka kilichopo maili 200 kutoka mji mkuu wa Urusi Moscow kwa nia ya kumuabudu.

  Si ajabu ukipita kwenye kijiji hicho na kukuta watu wamepiga magoti mbele ya picha yake wakisali.

  Baada ya kufanya kazi jeshini kwa kipindi kirefu, Torop alifanya kazi kama trafiki polisi wa nyakati za usiku kwenye mji wa Minusinsk mpaka alipoachishwa kazi.

  Torop alizaliwa upya kama Yesu mwaka 1991 baada ya kuhisi kuwa yeye ni mtoto wa Mungu.

  Torop anasema kwamba ghafla kuna kitu kilimwasha kuwa yeye ni Yesu aliyekuwa akitarajiwa kurudi duniani baada ya miaka 2000 tangia aliposulubiwa msalabani

  Alisema kwamba aligundua kuwa Mungu alimtuma duniani ili awafundishe watu juu ya ubaya wa vita na uharibifu wa mazingira unaofanywa na binadamu.

  Wafuasi wake ambao wamejitolea maisha yao kwaajili yake, hawaruhusiwi kula nyama na amewapiga marufuku kuvuta sigara na kunywa pombe.

  Takribani waumini wake 300 wamejenga nyumba za vibanda kulizunguka kanisa lake ili kupata urahisi wa kumuabudu.

  Maelfu ya watu wengine wameanzisha makazi yao kwenye vijiji vya jirani karibu na kijiji hicho na huvumilia baridi kali la Siberia ili waweze kuwa karibu na masiha wao.

  Katika mlima mmoja uliopo karibu na kijiji hicho, kuna kengele ambayo hupigwa mara tatu kwa siku ili kuwajulisha wafuasi wake wakati wa kuacha kazi na kupiga magoti kusali.

  Yesu huyo wa Urusi hutumia muda mwingi akichora picha kwenye nyumba yake anayoishi na mkewe na watoto wake sita ambapo mmoja wa watoto hao ni wa mmoja wa wafuasi wake na alijitolea kumlea.

  Wakosoaji nchini humo wamekuwa wakimtuhumu kutumia imani kuwahadaa wafuasi wake kwa sababu zake binafsi.

  Katika miaka ya hivi karibuni Yesu huyo amekuwa akisafiri kwenda katika baadhi ya nchi za ulaya kama vile Ufaransa, Italia na Uholanzi kwaajili ya kuwabatiza wafuasi wake wapya katika nchi hizo.

  Yesu huyo amekuwa akidai kuwa kanisa lake haliingizi pesa yoyote na safari zake hizo katika nchi za ulaya hudhaminiwa na watu wanaomualika. GONGA HAPA KWA PICHA ZA YESU WA URUSI
  source nifahamishe.com
   
 7. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #7
  Oct 16, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Literal intepretation? Kama (1) dunia siyo flat, na (2) umbali kutoka ardhini mpaka mawinguni ni 1 - 3 km; inawezekanaje kila jicho/mtu amuone?
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  Oct 16, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  siku za mwisho ndo hizi inatupasa tusome nyakati
   
 9. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #9
  Oct 16, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wale wote waliotaka ushahidi, huyu jamaa kautoa tayari, kuna mwenye swali?
   
 10. N

  Nzinyangwa Member

  #10
  Oct 16, 2009
  Joined: Aug 27, 2008
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama mtu anadanganywa na Kakobe, Mwingira, Mzee wa upako na kuna wengine wanajiita 'Mitume na manabii' kuwa wanaponya UKIMWI na kama mtu alidanganyika kuwa ile picha tunayoiona ni ya Yesu na sinema inayoonyeshwa kwa promosheni kila wakati wa Pasaka ni halisi na kama mtu huyo amedanganyika kuwa "Yesu ni Mungu" kwanini mtu huyo iwe vigumu kudanganyika kuwa yule jamaa ni Yesu?
   
 11. E

  EMMANUEL SHOMBE Member

  #11
  Oct 16, 2009
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dunia nimekwisha mpaka leo kuna yesu feki?
   
 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  Oct 16, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Dunia haipo flat na bado kuna 'dini' moja al maaruf sana inayojinadi kuwa kitabu chake kimejaa sayansi mpaka Bing Bang theory lakini bado wanaabudu kuelekea uelekeo fulani kana kwamba dunia ni flat!
   
 13. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #13
  Oct 16, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Cant say more! covered. lets wait for the exams.
   
 14. K

  Kilian Senior Member

  #14
  Oct 17, 2009
  Joined: Apr 26, 2009
  Messages: 147
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mimi mwenzangu ulipoanza kuchangia katika sentensi za mwanzo, ukijaribu kuhoji jinsi watu wanavyodanganyika, kuwaamini kina kakobe na hao wanaojiita manabii na mitume, nilidhani labda unajua unachokiongea. Lakini unapomlizia mjadala wako kwa kuhoji umungu wa Kristo..."Yesu ni Mungu", unanitia mashaka. Nimengudua hata wewe hujui unachoongea. Sikushangai, inawewzekana wewe sio Mkristu, na kama ni mkristu, basi biblia husomi, na ikiwa unasoma basi huielewi. Biblia inaweka wazi umungu wa kristo katika sehemu mbalimbali kwenye agano Jipya. Enjili ya Yohana inaanza kwa falisafa safi na kali ambayo inaliweka hilo wazi kabisa. Sitashangaa kwamba pia hukuielewa kwakua imetumika lugha ya ndani sana na lugha ya picha....hapo mwanzo alikuweko neno....naye neno alikuwa mungu.... Naomba usome tena vizuri. reje tena maeneo mbalimbali yesu anaposema yeye na babani mmoja na aliyemwona yeye amemwana baba.Ndugu yangu unahitaji imani kuelewa mabo haya na hekima kuyapambanua nakuyapokea. biblia inasemavyema inaposema... "nakushukuru baba, bwana wa mbingu na nchi kwakuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga". Mwombe mungu akufunulie hayo, usitumie hekima ya kibinadamu, hutayaelewe yatakuchangaya tu.
   
 15. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Wamisionari nuksi kweli, yaani wamefanikiwa kuwaaminisha watu wa ulimwengu hata jinsi mwonekano wa Mwokozi ulivyo!!
   
 16. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #16
  Apr 21, 2015
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,546
  Likes Received: 1,599
  Trophy Points: 280
  angekuja na afrika kuchukua wafuasi, maana waumini kama wamechoka kumsubiri masihi...
   
Loading...