Yesu angekuwa kama Askofu Gwajima asingewasamehe waliomsaliti na kumtesa

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
13,423
13,935
Askofu Gwajima angeeleweka zaidi kama angewasamehe wote msingizia, kumlaza mahabusu na kumpekuwa kwa dhana kuwa alikuwa anajihusisha na madawa ya kulevya kumbe sio. Heshima yake ingeenea duniani kote kama angewasamehe bure na kuwaombea kwa mungu wake watu hao bila kulazimika kufanya vile alivyofanya dhidi yao. Badala ya kumuachia baba yake wa mbinguni awaadhibu aliamua kuwaadhibu mwenyewe. Yesu alikuwa na nguvu za kuwaadhibu waliomtesa na kumuua lakini aliwasamehe bila kusema saaaana majukwaani.
TUMSIKU BW. Yesu Kristo
 
Kwani umemsikia Gwajima kampiga mtu,au kamchapa mtu kofi,au kamteka mtu?Msema kweli ni mpenzi wa mungu,Gwajima yeye kasema ukweli tu kua Makonda hana vyeti halali,na huo ndio ukweli ni Bashite kweli na hana vyeti kweli,sasa mchungaji kakoea nini hapo?kumbe kusema ukweli mbele za Mungu ni kulipa kisasi?
 
Ila pia gwajima angekuwa yesu ungekuta kashasulubiwa na yesu angekuwa gwajima, ungekuta kabambikiwa kesi na kuwekwa sero na sasa angekuea nageuza almasi kuwa maji
 
Kwani umemsikia Gwajima kampiga mtu,au kamchapa mtu kofi,au kamteka mtu?Msema kweli ni mpenzi wa mungu,Gwajima yeye kasema ukweli tu kua Makonda hana vyeti halali,na huo ndio ukweli ni Bashite kweli na hana vyeti kweli,sasa mchungaji kakoea nini hapo?kumbe kusema ukweli mbele za Mungu ni kulipa kisasi?
Shida kasema ukweli kwakuchelewa. Mh. Makonda alianza kufahamika vizuri kwa watanzania kipindi kile cha kukusanya maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya. Kisha akateuliwa kuwa Mkuu wa wilaya ya kinondoni, hatimaye RC. Askofu alikuwepo muda wote huu lakini alinyamaza na ukweli wake kuhusu Makonda. Amesubiri sekeseke la kutuhumiwa kuhusu madaw ndio aseme ukweli? Huu sio ukweli bali ni kulipiza kisasi, na Yesu hapendi watu walipize visasi kwa waliowakosea ila kwa kuwasemehe tena 7x70 kwa siku
 
Bw. Yesu alikuwa na kazi ya kubeba dhambi ya ulimwengu ambayo iltakiwa ikamilike kwa mauti ya msalaba. Hivyo, hakupaswa hata kujitetea.. Gwajima ni mtumishi wa Yesu kama alivokuwa. Paulo, ambaye alijitetea hata kufikia kumtukana kuhani mkuu Anania baada ya kuamuru Paulo apigwe bila kosa lolote. Gwajima ana haki ya kujitetea anaposingiziwa..
 
Askofu Gwajima angeeleweka zaidi kama angewasamehe wote msingizia, kumlaza mahabusu na kumpekuwa kwa dhana kuwa alikuwa anajihusisha na madawa ya kulevya kumbe sio. Heshima yake ingeenea duniani kote kama angewasamehe bure na kuwaombea kwa mungu wake watu hao bila kulazimika kufanya vile alivyofanya dhidi yao. Badala ya kumuachia baba yake wa mbinguni awaadhibu aliamua kuwaadhibu mwenyewe. Yesu alikuwa na nguvu za kuwaadhibu waliomtesa na kumuua lakini aliwasamehe bila kusema saaaana majukwaani.
TUMSIKU BW. Yesu Kristo
Bashite hajamkosea Gwajima bali kalikosea taifa na Mungu!
 
Back
Top Bottom