Yes they can, zambia wameweza sisi zamu yetu lini? Mpira ni kazi ilipayo sana.

Kitomai

JF-Expert Member
May 21, 2009
1,060
281
Zambia wamefanya jambo ambalo limewashitusha wengi. Wengi walisema kama siyo Ivory Coast basi itakuwa Ghana. Mambo yamekuwa kinyume kabisa. Leo ule usemi usemao umdhaniaye ndiye siye umetimizwa. Vijana wa Chipolopolo wameitumia vizuri miili yao ya akili. Walikuwa wakicheza huku wakifikiri, siyo kufikiri tu, bali kufikiri vizuri. Waliruhusu fikra zenye kuwapa ushindi kuingia katika mifumo yao mikuu ya kufikiri. Hawakuruhusu mazingira na wachezaji maarufu wenye majina makubwa huko ulaya kuwapangia wafikirie kitu gani.
Wao walichokuwa wanakijua kichwani mwao ni kimoja tu. Wamejipanga watapata ushindi. Muda wote walikuwa wakifikiria ushindi. Hawakufikiria kushindwa kwa sababu kushindwa kwao ni jambo lisilowahusu, kama hulihitaji jambo walitafutia nini?
Tunajifunza nini, nini siri ya mafanikio yao. Tujifunze kutoka kwao tusiende kujifunza kwa walioshindwa.
TFF nendeni huko Zambia mkajifunze siri ya mafanikio ya kuweza kwao. Waziri wa michezo hupo? Na wewe nenda huko ukajifunze kwa hawa jirani zetu. Mpira ni ajira tosha tena inalipa kweli kweli, angalia mishahara ya wachezaji wa kulipwa. Ebu tazama jinsi mishahara ilivyo minono inayatokana na kazi ya football.

Ranking 2011/Hii ni ripoti ya 2011.

1. Lionel Messi (ARG / Barcelona): € 31 million (€ 10 million in salary, bonuses of € 1 million, € 20 million advert contract)
2. Cristiano Ronaldo (POR / Real Madrid): € 27.5 million (€ 13 million in salary, bonuses of € 0.5m, € 14 million advert contract)
3. Wayne Rooney (ENG / Manchester Utd): € 20.7 million (€ 13.2 million in salary, bonuses of € 0.5m, € 7m advert contract)
4. Kaka (BRA / Real Madrid): € 19.3 million (10 million € salary, 300 000 € bonuses, € 9 million advert contract)
5. David Beckham (ENG / Los Angeles Galaxy): € 19 million (€ 4.1 million in salary, 400 000 € bonuses, € 14.5 million advert contracts)
6. Ronaldinho (BRA / Flamengo): € 18.3 million (€ 7.5 million in salary, bonuses of € 3.3m, € 7.5m advert contract)
7. Carlos Tevez (ARG / Manchester City): € 15.4 million (€ 10 million in salary, bonuses of € 3 million, € 2.4 million advert contract)
8. Frank Lampard (ENG / Chelsea): 14.2 M € (8.2 Me salary, € 1 million bonus, € 5 million in advert contracts)
9. Fernando Torres (ESP / Chelsea): € 14 million (€ 8 million in salary, 800 000 € bonuses, € 5.2m advert contract)
10. Yaya Toure (CIV / Manchester City): € 13.8 million (11.1 million € salary, 500 000 € bonuses, € 2.2m advert contract)
11. Thierry Henry (FRA / New York Red Bulls): 13.6 M € (4.1 Me salary, € 3.5 million bonus, € 6 million advert contract)
12. Bastian Schweinsteiger (GER / Bayern Munich): € 13.2 million (€ 8 million in salary, bonuses of € 1.2m, € 4 million advert contract)
13. Samuel Eto'o (CAM / Inter Milan): € 13 million (€ 9 million in salary, bonuses of € 2 million, € 2 million advert contract)
14. Philipp Lahm (GER / Bayern Munich): € 12.9 million (€ 10 million in salary, bonuses of € 1.1m, € 1.8m advert contract)
15. Didier Drogba (CIV / Inter Milan): € 12.8 million (€ 7.5 million in salary, 800 000 € bonuses, € 4.5m advert contract)
16. Zlatan Ibrahimovic (SWE / AC Milan): € 12.5 million (€ 9 million in salary, bonuses of € 1 million, € 2.5 million advert contract)
17. Franck Ribéry (FRA / Bayern Munich): € 11.9 million (10 million € salary, 800 000 € bonuses, € 1.1m advert contract)
18. Steven Gerrard (ENG / Liverpool): € 11.7 million (€ 7.2 million in salary, 500 000 € bonuses, € 4 million advert contract)
19. Carles Puyol (ESP / FC Barcelona): € 11.4 million (€ 8.5 million in salary, bonuses of € 1.4m, € 1.5m advert contract)
20. Gianluigi Buffon (ITA / Juventus): € 11.3 million (€ 6 million in salary, 100 000 € bonuses, € 5.2m advert contract)

Leo hii msomi gani au mwanasiasa gani hapa bongo anaweza kupata karibu karibu na hao!
Michezo ni kazi. Michezo ni ajira. Watoto wajengwe tokea chini. Michezi inalipa. Wapi UMISHUNTA, UMISETA!
Tunataka wasomi wa football, wasomi wa riadha, wasomi wa masumbwi, wasomi wa muziki, n.k

Kwa ushindi huo lazima mawakala wa huko ulaya na kwingine kote duniani wataanza kuitazama Zambia kwa Mwanga tofauti na wengi watapata ajira yenye mshahara mnono.
 

Attachments

  • zambian.jpg
    zambian.jpg
    45.4 KB · Views: 57
Yani unawaambia viongozi wa TFF na Waziri waende wakajifunze badala ya team? Uko serious au wewe ni waziri au kiongozi wa TFF unapima upepo wa per-diem humu?
 
Sio lazima wa tz nao wao na vipaji vya mpira wa miguu. Kama tumeshindwa miaka yote,tujaribu hata mashindano ya kuvuta kamba, kufukuza kuku,tukiyafanya kisiriaz kabisa yanaweza kutuweka kwenye ramani michezo. Aliyeanzisha mpira wa miguu unadhani alianzajeanzaje?
 
Yaaaaaani Tanzania? Yani yani yani yani yaaani hii Tanzania? Kweli? Tanzania hii hiiii aisee, uko serious kabisaaaa....
 
wachezaji wetu waache kudanganya umri wao, ligi yetu imejaa vibabu hivyo inakuwa vigumu kupata wachezaji vijana ambao wanaweza kuhimili ushindani, mfono muulize kaseje au sajigwa umri wao halisi watakuambia kuwa bado hawajafikisha miaka thelathini
 
wazambia hao walikufa first eleven karibu yote, jamaa wakaanza moja na wamerudi kwenye mafanikio. Sisi wametupita tena, wacha tuendelee na ndumu zetu na tff waendelee kusinzia kama wassira.
 
Ina maana hujui hii vitu vyote vinavyohitaji jitihada ili tufanikiwe. Watanzania tukiongozwa na viongozi uchwara. Huwa tunaambiwa hutuna BAHATI. Badala ya kufanya jitihada tusonge mbele, wanabaki kutusisitizia. Hatuna bahati ya kufanya vizuri katika michezo ya kimataifa.
 
wazambia hao walikufa first eleven karibu yote, jamaa wakaanza moja na wamerudi kwenye mafanikio. Sisi wametupita tena, wacha tuendelee na ndumu zetu na tff waendelee kusinzia kama wassira.

Wazambia wanaweza kila kitu. Hata kwenye siasa za mageuzi na demokrasia. Sasa hivi wana Rais mpya King cobra Satah. Ana less than 3 months toka aingie madarakani lakini ameshaifanyia nchi yake mambo makubwa. Anachukua Ubimgwa wa Afrika mapema hii mwee! Jamani sisi na miaka yetu 50 eti tumethubutu tumeweza halafu eti tunasonga mbele! ****!
 
Tutaweza pindi ccm watakapotoka madarakani!zambia wameshinda baada ya Satta kuingia madarakani!
 
Mnaikumbuka hii falsafa, hili tuendelee katika kila kitu tunahitaji: 1.Watu. 2.Siasa safi. 3.Ardhi na 4. Uongozi bora.
Tunayo ardhi bora iliyosheheni rutuba, madini, mafuta na gesi ya asili. Hapo katika siasa safi, uongozi bora na watu kwa mtazamo wangu naona ndiyo kuna matatizo. Athari zinaonekana katika sekta zote kuazia elimu, afya, Makaazi, matharani Dar es Salaam, unaambiwa aslimia 30% ya wakaazi wa Dar es Salaam wanakaa katika maeneo yasiyopimwa ili hali kuna wizara inayoshughulika na ardhi na makaazi, kuna idara za mipango miji kataka ngazi zote kuanzia ngazi ya kata, kuna chuo kikuu kishiriki cha ardhi kila mwaka kinatoa wasomi.
Naona kuna tatizo la kutokutaka kuwajibika pale tunaposhindwa jambo. Badala ya kuwajibika tunautupia lawama upande fulani kana kwamba upande huo ndiyo chimbuko la kushindwa kwetu.
Hili ni tatizo kubwa karibu katika kila kona ya maisha ya wabongo wengi. wenyenchi wanaitupia lawama serikali na serikali nayo inawatupia inawarudishia hizo lawama. Kimtazomo wangu serikali haiwezi kutatua matatizo ya wananchi kwa kuwa serikali kama serikali yenyewe ni tatizo, nasema serikali yeyote ile hata ya America ni tatizo. Serikali kama haionyeshi uwezo wa kushughulia matatizo ya wananchi na hao wananchi walioiweka hiyo serikali wanabakia kulialia tu badala ya kuiweka pembeni ili baadaye waiweke nyingine na hiyo nyingine ikionyesha udhaifu inawekwa pembeni bandika bandua hapo ndipo serikali itakaposhika adabu. [FONT=trebuchet ms, arial, helvetica]ze of Japan (145,000 sq. miles)[/FONT]364,900 sq mi
Nasema tena watu waendelezwe kielimu. Mfano Japani ina ukubwa wa mita za mraba miles 145,000 za ardhi na katika hizo ni asilimia 16% ya ardhi ndiyo yenye rutubu. Na kwa takwimu za nyuma kidogo ina wakaazi 150mil. Njoo Tz, ina ukubwa wa mita za mraba miles 364,900 na katika hizo asilimia 90 ni ardhi yenye rutuba. Huko Japan wana tatizo la winta na majanga ya kibinadamu ndiyo kwao. Hali ya uchumi na huduma za jamii zipo katika hali nzuri sana kuliko sisi. Tatizo ni nini hasa mpaka sisi tukabakia mkiani? Elimu duni bila shaka! Wananchi wengi hawana elimu ya kutosha kupambana na mazingira. suluhu tuwekeze katika elimu, elimu ya kumuendeleza mtu, siyo bora elimu bali elimu bora.
 
Tutaweza pindi ccm watakapotoka madarakani!zambia wameshinda baada ya Satta kuingia madarakani!
hili wazo lako lina uzito maana sasa Wazambia inaelekea they have decided to change the way how they used to think. Na wameanza na 'kiini' cha matatizo!

hapa wasiwasi wa kufanikiwa unaongezeka maana namsikia Mzee Ndolanga baana ya 'kuchapwa bakora' pale msikiti wa Kichangani, Magomeni anainyemelea TFDA sasa! Na kwa jinsi sisi 'Mitanzania' tulivyo sio ajabu kukuta huyu bwana anachomozea kwenye TFF!

Na mleta thread anasema TFF waende Zambia kujifunza, hiyo delegation itakayoenda huko wewe mwenyewe utasema!

Lakini kuna kitu kinawaunganisha zaidi Wazambia na hicho naona ndio kinazisaidia hata timu nyingine, sio vizuri kukileta hapa maana inaweza kuwa 'uchochezi'

 
Wenzetu wapo serious. Si unaona yule mchezaji aliyetaka kuleta za kuleta wakamrudisha nyumbani.Nidhamu ni muhimu sana. Na jambo lingine ni wachezaji kujiona Miungu watu. Wachezaji wetu wengi wakishajua tu kupiga chenga moja mbili na kupata hela ya bia moja mbili , basi wameridhika. Niamewangalia sana wachezaji wa zambia kwa vimo vyao ni sawa tu na hawa wakibongo. Si warefu. Sasa kutokana na tatizo la kutokuwa na wachezaji wenye vimo virefu, inatakiwa mpira wetu uwe wa kutandaza chini, wanasema < kimo cha kuku>. Wachezaji wa zambia waliwasumbua sana Ivory coast walipokuwa wanacheza mpira wa chini. Wale waivoria ni warefu na mpira ukiwa wa juu, walikuwa wanaumudu. Kwa hiyo tunaweza hata sisi kama tutabadilisha aina ya uchezaji kulingana na maumbile ya wachezaji wetu. Naona huku jamii forum kuna watu wanafaa kuwa washauri na si vibaya tukamshauri kocha.
 
Njaa ya pesa na kuingiza siasa kwenye michezo ndio matokeo wa kutofanikiwa hata cku moja kila kukicha ni afadhali na jana,taifa stars ya polsen ni afadhali na ya maximo,hapo hakuna cha kujifunza wala nn kwan wote waliopo kwenye hizo mamlaka wako after money basiii!
 
Back
Top Bottom