Yeriko Nyerere na Evarist Chahali wote ni ma-'opportunists', Hakuna wa kumnyoshea mwenzake kidole

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Imeripotiwa katika mtandao wa jamiiforums kuwa kijana wa Kitanzania aishie Scotland, EVARIST CHAHALI kuwa amemtakia kila la heri aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana baada ya kumaliza muda wake wa kutumikia nafasi hiyo ya Katibu Mkuu.
Mbali na kumtakia kila la heri Kinana, Chahali pia amebainisha kile alichodai kuwa ni Kinana kumdhulumu kiasi cha Shilingi za Kitanzania milioni 12.5 , kiasi anachodai aliahidiwa kupewa ili kumpigia Kampeni mgombea urais wa CCM katika uchaguzi mkuu wa 2015.

Inawezekana madai ya Chahali ni ya kweli lakini ukweli zaidi unaoonekana ni kwamba Chahali anatafuta uhalali tu wa kuendelea kuichafua Serikali ya awamu ya tano ambayo kimsingi imejipambanua kupambana na ubadhilifu wa mali ya Umma Uzembe, ufisadi na Rushwa.

Baada ya Porojo za Chahali, Kijana mwingine mshika mapembe ndani ya chama kimoja cha siasa, YERIKO NYERERE ameibuka na kimshambulia CHAHALI na kusema kuwa pesa anazodai kudhulumiwa na kinana zilikuwa apewe ili kumchafua aliyekuwa mgonbea wa CHADEMA, EDWARD LOWASSA.

Screenshot_20180602-202714.png

YERIKO anatoa tuhuma hizo dhidi ya CHAHALI na kutaka kuuonesha Umma wa Tanzania kuwa LOWASSA ni msafi na kwamba tuhuma dhidi yake mwaka 2015 zilikuwa za kumchaafua.tu. YERIKO anatoa tuhuma hizo dhidi ya CHAHLI huku alisahau kuwa mwaka. 2015 huo huo aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa Jamiiforums kuwa LOWASSA ni muuaji na hafai hata kuwa mwenyekiti wa nyumba kumi kwa kile alichodai kuwa alianzisha wodi ya vilema wa BODABODA katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa vile ndiye aaliwanunulia vijana hao pikipi.

Kilio hiki bwana Lowassa utakilipia kabla ya 2015

Hitimisho: CHAHALI NA YERIKO wote wanasumbuliwa na njaa tofauti ni njaa zao kuuma nyakati tofauti na pengine kuwa na watu tofauti tofauti wa kutibu njaa zao.
Inawezekana mwaka 2015, Chahali alitegemea kutibu njaa zake kupitia CCM bahati mbaya mambo yakaenda ndivyo sivyo na kwa mantiki hiyo Chahali hana sababu nyingine ya kuichukia Serikali ya awamu ya tano, Serikali ambayo kamwe haiwezi kumruhusu anuse hata harufu ya kuganga njaa kipumbavu hivyo.

Mwaka 2015 Yeriko alikuwa anasumbuliwa na njaa ambayo sasa imetibiwa na LOWASSA baada ya kuhamia CHADEMA.

Nimalizie tu kwa kuwaomba Watanzania kutumia kauli za CHAHALI na YERIKO kupata somo kwamba siyo kila mtu anayejifanya kupiga kelele za kuishambulia Serikali huwa ni kelele zenye sababu za msingi bali wengine wanakuwa wamenyimwa fursa za kuganga njaa zao.

Nawatakia maandalizi mema ya kuanza kulijenga taifa kesho jumatatu baada ya mapumziko ya mwisho wa wiki.
 
Awamu hii ya tano chini ya Mwenyekiti asiyependa kukosolewa imeonyesha kushindwa kwenye mambo mengi sana kutokana na kukurupuka na kutegemea ushauri kutoka kwa watu wasio na weledi kama Makonda kuongoza nchi
 
ebu lala tu ww maana usingizi haujakuisha
1.5 T zipo wap?
ben yuko wap?
walioingia mkataba wa madini na uvivu ni kina nani?
alafu unakuja sema hii awamu inapambana na rushwa na ubadilifu wa fedha za wananchi.

miaka 20 ijayo kutaundwa kamati ya bunge kuchunguza haya
uwanja wa Chato
reli ya umeme
ununuzi wa ndege
alafu wabunge hawa hawa waliotaka kuwatoa ata macho wapinzani bungeni ndio hao hao watashangaa kitakachokuwa ndani ya report
 
Pesa ni kila kitu, Yeriko alishawekwa Kapuni na Lowassa, Taratibu Chahali naye yuko njiani
 
ebu lala tu ww maana usingizi haujakuisha
1.5 T zipo wap?
ben yuko wap?
walioingia mkataba wa madini na uvivu ni kina nani?
alafu unakuja sema hii awamu inapambana na rushwa na ubadilifu wa fedha za wananchi.

miaka 20 ijayo kutaundwa kamati ya bunge kuchunguza haya
uwanja wa Chato
reli ya umeme
ununuzi wa ndege
alafu wabunge hawa hawa waliotaka kuwatoa ata macho wapinzani bungeni ndio hao hao watashangaa kitakachokuwa ndani ya report
Awamu hii mtatapatapa sana
 
Awamu hii ya tano chini ya Mwenyekiti asiyependa kukosolewa imeonyesha kushindwa kwenye mambo mengi sana kutokana na kukurupuka na kutegemea ushauri kutoka kwa watu wasio na weledi kama Makonda kuongoza nchi
wewe utakuwa Yeriko au Chahali, maana ulivyokurupushwa siyo kawaida
 
Tattizo la mtu mwenye njaa ndilo hilo, hanaga kitua cha kuzuia madhaifu yake yasionekane. Wanachokifanya Chahali na Yeriko ni kujidhalilisha tu, yaani mtu anataja waziwazi kuwa alinyimwa pesa za rushwa? Hovyo kabisa
 
Imeripotiwa katika mtandao wa jamiiforums kuwa kijana wa Kitanzania aishie Scotland, EVARIST CHAHALI kuwa amemtakia kila la heri aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana baada ya kumaliza muda wake wa kutumikia nafasi hiyo ya Katibu Mkuu.
Mbali na kumtakia kila la heri Kinana, Chahali pia amebainisha kile alichodai kuwa ni Kinana kumdhulumu kiasi cha Shilingi za Kitanzania milioni 12.5 , kiasi anachodai aliahidiwa kupewa ili kumpigia Kampeni mgombea urais wa CCM katika uchaguzi mkuu wa 2015.

Inawezekana madai ya Chahali ni ya kweli lakini ukweli zaidi unaoonekana ni kwamba Chahali anatafuta uhalali tu wa kuendelea kuichafua Serikali ya awamu ya tano ambayo kimsingi imejipambanua kupambana na ubadhilifu wa mali ya Umma Uzembe, ufisadi na Rushwa.

Baada ya Porojo za Chahali, Kijana mwingine mshika mapembe ndani ya chama kimoja cha siasa, YERIKO NYERERE ameibuka na kimshambulia CHAHALI na kusema kuwa pesa anazodai kudhulumiwa na kinana zilikuwa apewe ili kumchafua aliyekuwa mgonbea wa CHADEMA, EDWARD LOWASSA.

View attachment 793511

YERIKO anatoa tuhuma hizo dhidi ya CHAHALI na kutaka kuuonesha Umma wa Tanzania kuwa LOWASSA ni msafi na kwamba tuhuma dhidi yake mwaka 2015 zilikuwa za kumchaafua.tu. YERIKO anatoa tuhuma hizo dhidi ya CHAHLI huku alisahau kuwa mwaka. 2015 huo huo aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa Jamiiforums kuwa LOWASSA ni muuaji na hafai hata kuwa mwenyekiti wa nyumba kumi kwa kile alichodai kuwa alianzisha wodi ya vilema wa BODABODA katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa vile ndiye aaliwanunulia vijana hao pikipi.

Kilio hiki bwana Lowassa utakilipia kabla ya 2015

Hitimisho: CHAHALI NA YERIKO wote wanasumbuliwa na njaa tofauti ni njaa zao kuuma nyakati tofauti na pengine kuwa na watu tofauti tofauti wa kutibu njaa zao.
Inawezekana mwaka 2015, Chahali alitegemea kutibu njaa zake kupitia CCM bahati mbaya mambo yakaenda ndivyo sivyo na kwa mantiki hiyo Chahali hana sababu nyingine ya kuichukia Serikali ya awamu ya tano, Serikali ambayo kamwe haiwezi kumruhusu anuse hata harufu ya kuganga njaa kipumbavu hivyo.

Mwaka 2015 Yeriko alikuwa anasumbuliwa na njaa ambayo sasa imetibiwa na LOWASSA baada ya kuhamia CHADEMA.

Nimalizie tu kwa kuwaomba Watanzania kutumia kauli za CHAHALI na YERIKO kupata somo kwamba siyo kila mtu anayejifanya kupiga kelele za kuishambulia Serikali huwa ni kelele zenye sababu za msingi bali wengine wanakuwa wamenyimwa fursa za kuganga njaa zao.

Nawatakia maandalizi mema ya kuanza kulijenga taifa kesho jumatatu baada ya mapumziko ya mwisho wa wiki.

Chahali kama kweli ali dhulumiwa kwakazi yoyote iwe ya kampen alete mkataba wa makubaliano hapa JF tupitia kifungu kimoja baada ya kingine ili tuone pakuanzi kuchangi sivinginevyo akishindwa kuleta mkataba atakua ametumwa kumchafu mtu
 
Hawa vijana wawili, Yeriko na Chahali wote wameandika vitabu wanavyoviita vya kijasusi, pesa zilizotumika kuchapisha vitabu hivyo ni pesa chafu , inawezekana kuna sehemu wamegongana , kila mmoja akitaka afaidi fursa
 
Mafisadi yako huko kwenu, ccm yametimuliwa yote.
Change, Ngelejo, Prof. Tiba, Sizonje(kuuza nyumba za serikali), wabunge wa ccm mfano six mapunjo wa mbingo, makatibu wa ccm wa mikoa na kitawi maalum cha wizi na ufisadi cha uvvccm wakiongozwa na Shaka zulu, kinano (pembe za ndovu) nk. Orodha haiwez kuisha leo au kesho
 
Chahali kama kweli ali dhulumiwa kwakazi yoyote iwe ya kampen alete mkataba wa makubaliano hapa JF tupitia kifungu kimoja baada ya kingine ili tuone pakuanzi kuchangi sivinginevyo akishindwa kuleta mkataba atakua ametumwa kumchafu mtu
Huyu kijana nasikia ni mtu wa fursa sana, yeye haoni shida kusema uongo ilimradi tu uongo huo utamuwezesha apate pesa au aonewe huruma.
 
Change, Ngelejo, Prof. Tiba, Sizonje(kuuza nyumba za serikali), wabunge wa ccm mfano six mapunjo wa mbingo, makatibu wa ccm wa mikoa na kitawi maalum cha wizi na ufisadi cha uvvccm wakiongozwa na Shaka zulu, kinano (pembe za ndovu) nk. Orodha haiwez kuisha leo au kesho
Unaongelea ziipendwa? Mbona higusii Mbowe kuishi majengo ya Umma miaka 20 bila kulipa kodi? Na hao uliowataja wako wapi sasa awamu hii ukiondoa Chenge ambaye hata Mbowe alimpa kura ya kuwa Mwenyekiti wa Bunge akijua atapigia kifua asiguswe ufisadi wa NHC? mbona huongelei biashara ya dawa za kulevya ya Mwenyekiti wako? Mbona huongelei hati chafu ya chama chako? Mbona huongelei Chama chako kina zaidi ya miaka 20 kibaishi "Geto" bila ofisi, Ruzuku ambayo ni kodi zetu wanancji inakwenda wapi? Mbona huongelei Wabunge wa viti maalum wa Chama chako kutozwa mil. 1 kila mwezi, zinafanya nini?
 
Chahali amedata anajifanya mjanja kakutana na watoto wa mjn wametumia njaa zake kumfundisha. Povu kwa lote kwa Magu kumbe analipwa mpuuzi yule.
 
Tangu Yericko alete humu jukwaani zile picha za kinamama wa Dar halafu akasema eti ni masista, nimepunguza imani kwenye maandiko yake.

Anadanganya watu ambao hawakuwa na akili bado wakati pale maelezo kukiwekwa picha za matukio ya uhuru.
 
Back
Top Bottom