Yericko Nyerere ajibiwa, Mama Mghwira atampisha Prof. Lipumba kama Dr. Slaa alivyompisha Lowassa

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Kwenye akaunti yake ya tweeter, Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, aliandika maneno yenye kuwakebedhi aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi(CUF), Prof. Ibrahim Harouna Lipumba na Mwenyekiti wa Chama cha ACT-WAZALENDO, Mama Anna Mngwira yaliyosomeka "HONGERA PROF. LIPUMBA KWA KUJIUNGA NA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO, pole mama yangu @annamugwira utalazimika kujiuzulu umpishe kitini prof. Lipumba".

2016-09-06 07.40.53.png

Katika kuchangia andiko la Yeriko Nyerere naye akakutana na maneno haya "ATAMPISHA KAMA DR. SLAA ALIVYOMPISHA LOWASSA HAPO CHADEMA"

2016-09-06 07.40.16.png

Naye kiongozi mkuu wa ACT-WAZALENDO akapigilia msumari kw kuandika:
"HATUNA MAJADALA KUHUSU WANACHAMA WAPYA. MKUMBUKE HAO WANAOENEZA TUNA WANACHAMA WAPYA NDIYO HAO HAO WALISEMA HIVYO HIVYO 2015, IKAWAJE?"
Zitto anamaanisha kuwa mwaka 2015 ni CHADEMA hao hao waliosema LOWASSA anahamia ACT-WAZALENDO, Lakini mwisho wa siku akahamia kwo.

2016-09-06 07.38.54.png

Mytake: Maneno ya Prof. Kitila mkumbo yanabaki kuwa hai. "wanasiasa wanapaswa kuwa na akiba ya maneno"
 
Attachments

  • 2016-09-06 07.40.53.png
    2016-09-06 07.40.53.png
    9.4 KB · Views: 74
Hivi Uvccm hamna uwezo wa kuanzisha mada za maana za kujenga nchi badala ya kuokoteleza vijihabari vya kuunga Unga.
 
Tatizo ukitofautiana na Chadema, utastahili adhabu ya mfano wa kifo. Ila ukitoka sehemu nyingine na kujiunga nao wewe ni ni shujaa. Watakukumbatia kwa nguvu zote hata kama umejipaka mavi mwili mzima. Hili dude Chadema silielewi

ni janga la kitaifa
 
Kwenye akaunti yake ya tweeter, Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, aliandika maneno yenye kuwakebedhi aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi(CUF), Prof. Ibrahim Harouna Lipumba na Mwenyekiti wa Chama cha ACT-WAZALENDO, Mama Anna Mngwira yaliyosomeka "HONGERA PROF. LIPUMBA KWA KUJIUNGA NA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO, pole mama yangu @annamugwira utalazimika kujiuzulu umpishe kitini prof. Lipumba".

View attachment 394508
Katika kuchangia andiko la Yeriko Nyerere naye akakutana na maneno haya "ATAMPISHA KAMA DR. SLAA ALIVYOMPISHA LOWASSA HAPO CHADEMA"

View attachment 394504
Naye kiongozi mkuu wa ACT-WAZALENDO akapigilia msumari kw kuandika:
"HATUNA MAJADALA KUHUSU WANACHAMA WAPYA. MKUMBUKE HAO WANAOENEZA TUNA WANACHAMA WAPYA NDIYO HAO HAO WALISEMA HIVYO HIVYO 2015, IKAWAJE?"
Zitto anamaanisha kuwa mwaka 2015 ni CHADEMA hao hao waliosema LOWASSA anahamia ACT-WAZALENDO, Lakini mwisho wa siku akahamia kwo.

View attachment 394505
Mytake: Maneno ya Prof. Kitila mkumbo yanabaki kuwa hai. "wanasiasa wanapaswa kuwa na akiba ya maneno"

Logic yako ni nini ?
 
Akienda hapo haishangazi kwasababu ACT ni CCM B iliyomtumia Lipumba kuisaliti CUF kama Yuda Iskariote alivyotumiwa kumsaliti Yesu.

Na mkimzingua hapo ataenda kuwa mwenyekiti wa BAKWATA insh'allah
 
Yeriko Nyerere na Ben Saanane ndiyo kazi yao ilibaki mitandaoni, MBOWE na LOWASSA hawezi kukubali hawa vijana wakashika nyadifha kubwa zitakazowafanya wawe busy kiasi cha kutoonekana mitandaoni maana wao kazi yao ni kuwapotosha wasoma mitandao kwa maandiko ya hovyo hovyo kama haya.
 
Chadema ni chama cha ajabu sana. wana Udikteta wa mawazo. ni chama cha kuogopwa sana. kila kitu kwao ni sawa tu ila kwa wengine ni dhambi kubwa sana.
 
Akienda hapo haishangazi kwasababu ACT ni CCM B iliyomtumia Lipumba kuisaliti CUF kama Yuda Iskariote alivyotumiwa kumsaliti Yesu.

Na mkimzingua hapo ataenda kuwa mwenyekiti wa BAKWATA insh'allah
Hoja hamnazo tena siku hizi, CCMB ni ACT? Siyo CUF tena? Naamini hata Lowassa akiamua kuhamia CUF mtarudia kula matapishi kuwa CUF ni CCMB.
 
Back
Top Bottom