kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 8,990
- 17,879
Yemen yaionya Israel isijaribu kuivamia, yajibu vitisho vya Tel Aviv
Wizara ya Mambo ya Nje ya Serikali ya Uokovu ya Yemen imetahadharisha kuwa, vita vikubwa vitaibuka katika eneo la Asia Magharibi iwapo utawala wa Kizayuni wa Israel utathubutu kuivamia Yemen.
Taarifa iliyotolewa jana Jumapili na wizara hiyo imesema kuwa, badala ya kuzitishia nchi nyingine katika eneo, Israel inapaswa kujishughulisha zaidi na suala la kuyadhibiti maeneo iliyoyaghusubu.
Taarifa hiyo ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Serikali ya Uokovu ya Yemen ni jibu kwa matamshi ya vitisho yaliyotolewa juzi Jumamosi na jeshi la utawala haramu wa Israel.
Katika mahojiano na shirika moja la habari siku ya Jumamosi, msemaji wa jeshi la utawala wa Kizayuni alisema kuwa, utawala huo unazihesabu Yemen na Iraq kama nchi hatari zaidi katika eneo, na kwamba Tel Aviv inaitazama Yemen kwa jicho la karibu.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Yemen imeeleza bayana kuwa, "iwapo Israel itachukua hatua yoyote dhidi ya Yemen, basi maslahi yote ya Wazayuni na waitifaki wao katika Bahari Nyekundu yatakuwa shabaha halali (ya Yemen)."
Makombora mapya ya vikosi vya Yemen
Wizara ya Mambo ya Nje ya Serikali ya Sanaa imesisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni utakuwa wa kwanza kupata hasara kubwa iwapo vita kamili vitaripuka katika eneo.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, utawala huo khabithi unatafuta visingizio mbalimbali kuhalalisha hatua zake za uhasama dhidi ya mataifa mengine hususan uvamizi wake dhidi ya Palestina, na pia kuficha kushindwa kwake kuzishawishi nchi mbalimbali kuanzisha uhusiano nao wa kawaida.