Yellow Buses - SUMATRA hamlioni hili

Mkaa Mweupe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
654
183
Wanajamvi Habarini za muda,

Kama sikosei, miaka kama miwili iliyopita SUMATRA walisisitiza kuwa magari ya kubeba wanfunzi ni lazima yawe na rangi ya Njano (Yellow Bus) ikiwa ni mojawapo ya vigezo kupewa leseni ya uchukuzi.

Ni jambo jema kwani inasaidia kujua kuwa waliomo ndani ya gari husika ni wanafunzi na hivyo sisi madereva wengine kuchukua tahadhari tusije poteza Taifa la kesho. Pia ni standard ya duniani kote.

Jambo la kushangaza ni kwamba kuna watu hawatekelezi hilo lakini nao SUMATRA wamelifungia macho. Kuna baadhi ya Taasisi zenye kutoa huduma hii magari yao yote hawajatia japo mstari wa njano lakini SUMATRA kimya.

Bila kupepesa macho mfano wa wazi ni hii taasisi ya St Mary Schools, sijui kwa kuwa mmiliki ni kada wa CCM au vipi, sijasikia wala kuona magari yao yakibanwa. Au ndo kusema kuwa kuna walio juu ya sheria?

Nawasilisha.
 
Pia hata hayo yaliyopakwa rangi ya Njano, upakiaji (idadi) ya watoto huwa haizingatiwi. wakipita mbele ya traffic utadhani anaona msukule unapita.
 
Na yako sub-standard kabisa.......madirisha ya wakubwa huku vitoto vinachungulia nje kama kuku wanaoenda mnadani

BASI+1.jpg
 
Safari_ni_Safari, hapo nyuma huo msemo sijauelewa. Je, hao watoto humo ndani wataelewa."DON'T ASK DON'T TELL"
 
Magari ya ST mary's yanatisha,ni mabovu kupindukia, hayana rangi ya njano!mch lwakatare anaongoza kwa kuvunja sheria
 
Magari ya ST mary's yanatisha,ni mabovu kupindukia, hayana rangi ya njano!mch lwakatare anaongoza kwa kuvunja sheria
.

Na isitoshe lile pingamizi aliloweka kwa kujenga eneo tengefu inabidi liondolewe Kama aliingia choo cha kike ni kwa ujinga wake... Hamna kumuonea mtu huruma za kijinga.
 
Back
Top Bottom