Yehova witness kutimuliwa kwa kukataza wanafunzi kuimba wimbo wa taifa!

Kiranga,
Hapana. Hakuna cha Draconian hapa. Hata Biblia inasema mpe Kaisari kilicho chake. Kama hawa wazungu wanataka watu wasiimbe wimbo wa taifa waanzie kwao. Sio kuwadanganya watoto wetu. Hawa mawitness nakumbuka miaka ya 60 walifukuzwa Tanzania na Malawi kwa uhalifu huo huo.
Wanataka kuua uzalendo africa
 
Kwanza wimbo wa taifa wenyewe uko discriminatory.

Unaanza kwa kusema "Mungu ibariki Tanzania"

Sasa na sisi tusioamini mungu si tutaona huu wimbo ni kichaa kitupu, tukisema hatutaki kuimba on this ground utatulazimisha?
Nyerere alisema hatumchagui mtu asiyeamini Mungu. Marekani dollar imeandikwa in God we trust. Kwa hiyo wimbo wa taifa unamtambua Mungu muumba mbingu na nchi. Hao miungu wengine ni shughuli yako mwenyewe
 
Hapana.

Nyerere hakusema hatumchagui mtu asiyeamini mungu.

Alisema kwamba katiba yetu haikatazi mtu asiye na dini kuwa rais. Aliinyesha kutokuwa na kipingamizi cha msingi cha kutaka mtu asipate urais jwa sababu ya imani za dini. Unachosema wewe ni tofauti na alichisema Nyerere.

Na zaidi ya hapo, Katibu wake Nyerere wa siku nyingi, marehemu mama Joan Wickens (mzungu), alikuwa atheist, hakuamini mungu. Na Nyerere alijua hilo. Lakini halikumsumbua. Mimi najua habari hizi personally kwa sababu mama yangu alifanya kazi karibu sana na Mama Joan Wickens miaka hiyo Ikulu.

Wanaomjua Nyerere wenyewe wanajua hilo.

Waliomsikia kwenye redio ndio wanapotosha habari na kusema kwamba Nyerere alisema hatumchagui mtu asiyeamini mungu.
 
Hapana.

Nyerwre hakusema hatumchagui mtu asiyeamini mungu.

Alisema kwamba katiba yetu haikatazi mtu asiye na dini kuwa rais.

Na zaidi ya hapo, Katibu wake Nyerere wa siku nyingi, marehemu mama Joan Wickens (mzungu), alikuwa atheist, hakuamini mungu. Na Nyerere alijua hilo. Lakini halikumsumbua. Mimi najua habari hizi personally kwa sababu mama yangu alifanya kazi karibu sana na Mama Joan Wickens miaka hiyo Ikulu.

Wanaomjua Nyerere wenyewe wanajua hilo.

Waliomsikia kwenye redio ndio wanapotosha habari na kusema kwamba Nyerere alisema hatumchagui mtu asiyeamini mungu.
Alisema kama amuamini mungu tutatafuta namna ya kumwapisha, ambayo itamfunga kwa mungu tena
 
Hapana, namna ya kumuapisha si lazima imfunge kwa mungu.

Mtu anaweza kuapa kwa sheria/ katiba tu.
 
Sheria yoyote itakayolala kuiridhisha serikali kwa wema, inaridhiwa na mungu. Bora asiape kwa chochote
 
Wakimtaja mtume, sorry.

Point yangu ni kwamba, Muislamu anaposema "La ila aillaha Muhammad Rasul Allah" anakuwa kashajiweka kwamba mungu anayemuamini yeye ni yule ambaye Muhammad ni mtume wake, sasa akija mtu mwingine anayesema mungu wake tofauti na huyo mungu ambaye kamfanya Muhammad kuwa mtume wake, halafu wote wawili wake oamoja na kuimba "Mungu Ibariki Tanzania" mungu huyu ni yupo?

Aliyemfanya Muhammad juwa mtume wake au tofauti?
Kiranga nafikiri hukunielewa.

Mimi nilikuwa narekebisha hapo uliposema Mungu kuna baadhi ya Waislam wanamwita S.A.W kitu ambacho si kweli, na nikakuambia S.A.W ni kwa ajili ya Mtume Muhammad (S.A.W).

Kwa kukuweka sawa kwakuwa hukuelewa S.A.W inastahiki iwekwe wapi, ndio nikakufahamisha, lengo langu si kumjadili Mtume Muhammad (S.A.W).

Lengo langu lilikuwa kurekebisha pale uliposema kuna baadhi ya Waislam wanamwita Mwenyezi Mungu S.A.W.

Kitu ambacho si kweli.

Sisi Waislam Mwenyezi Mungu tunamwita Allah (A.W).

A.W ni A-zza Wajjala, ambayo maana yake tunamtukuza Allah ambae ni Mshindi mwenye uwezo/kuweza na si S.A.W kama ulivyosema wewe
 
Kiranga nafikiri hukunielewa.

Mimi nilikuwa narekebisha hapo uliposema Mungu kuna baadhi ya Waislam wanamwita S.A.W kitu ambacho si kweli, na nikakuambia S.A.W ni kwa ajili ya Mtume Muhammad (S.A.W).

Kwa kukuweka sawa kwakuwa hukuelewa S.A.W inastahiki iwekwe wapi, ndio nikakufahamisha, lengo langu si kumjadili Mtume Muhammad (S.A.W).

Lengo langu lilikuwa kurekebisha pale uliposema kuna baadhi ya Waislam wanamwita Mwenyezi Mungu S.A.W.

Kitu ambacho si kweli sisi Waislam Mwenyezi Mungu tunamwita Allah (A.W).

A.W ni A-zza Wajjala, na si S.A.W kama ulivyosema wewe

Nikipoandika S.A.W nilitaka kuandika "La illah illa allah Muhammad Rasul Allah".

Nimetaka radhi kwa kuchanganya hilo na kuelezea jinsi gani Muislamu asivyotakiwa kukubali mungu ambaye sio mungu aliyemtuma Muhammad.

Kiuhalisia, muislamu hata kuimba "Mungu ibariki" bika kuelewa mungu gani anayetakiwa kubariki ni shirki, kwa sababu Muislamu hawezi kuimba wimbo huu na Wakristo, Wabuda, Wazoroasti hqlafu wote wakawa wanamuomba Allah. Na muislamu kushiriki sala inayomuomba mungu asiyejulikana ni shirki.

Hii ni habari ya msingi kabisa.

Ambayo hujaijibu.
 
Sheria yoyote itakayolala kuiridhisha serikali kwa wema, inaridhiwa na mungu. Bora asiape kwa chochote
Hapana.

Mungu hayupo. Ni hadithi tu.

Kama yupo, thibitisha kwamba yupo.

Unaweza kunipa uthibitisho usiopingika kwamba mungu yupo?
 
Nikipoandika S.A.W nilitaka kuandika "La illah illa allah Muhammad Rasul Allah".

Nimetaka radhi kwa kuchanganya hilo na kuelezea jinsi gani Muislamu asivyotakiwa kukubali mungu ambaye sio mungu aliyemtuma Muhammad.

Kiuhalisia, muislamu hata kuimba "Mungu ibariki" bika kuelewa mungu gani anayetakiwa kubariki ni shirki, kwa sababu Muislamu hawezi kuimba wimbo huu na Wakristo, Wabuda, Wazoroasti hqlafu wote wakawa wanamuomba Allah. Na muislamu kushiriki sala inayomuomba mungu asiyejulikana ni shirki.

Hii ni habari ya msingi kabisa.

Ambayo hujaijibu.
Kama umekubali ulikosea, sawa.

Tufanye yamekwisha.

Mimi na wewe najua hatutoweza kufikia muafaka.

Sababu nakufahamu silaha yako kuu ni moja tu (ambayo haina nguvu).

Utaniambia nithibitishe uwepo wa Mungu, kitu ambacho tulishawahi jadili mimi na wewe kitambo.

Najua hapa tutaishia kubishana na hatutoafikiana
 
Sheria yoyote itakayolala kuiridhisha serikali kwa wema, inaridhiwa na mungu. Bora asiape kwa chochote
Wewe usibishane na huyo Kiranga.

Jamaa ni mbishi na ukimbana anabadilisha maneno.

Mfano hai fuatilia tokea nilipoanza nae jana.

Jinsi anavyotetea hoja yake na kusema alitaka kusema Laa Ilaaha Illa llah Muhammadan Rasuulullah na si S.A.W.

Kitu ambacho haviingiliani hata kidogo.

Ni katika kutetea ubishi wake.

Yaani mchezo alioufanya hapo hata mtoto wa chekechea anaustukia mchezo huo, labda mtoto mwenyewe awe zoba
 
Kama umekubali ulikosea, sawa.

Tufanye yamekwisha.

Mimi na wewe najua hatutoweza kufikia muafaka.

Sababu nakufahamu silaha yako kuu ni moja tu (ambayo haina nguvu).

Utaniambia nithibitishe uwepo wa Mungu, kitu ambacho tulishawahi jadili mimi na wewe kitambo.

Najua hapa tutaishia kubishana na hatutoafikiana
Kama huwezi kuthibitisha uwepo wa mungu, ni kazima ukubaki kwamba unaamini kitu ambacho ni hadithi isiyoweza kuthibitishika.
 
Kiranga ndugu yangu.

Mimi hapa nakwepa ubishani na wewe.

Kwasababu wewe huamini kabisa uwepo wa Mungu na Mimi naamini uwepo wake.

Kwa kuepusha tofauti zetu za kiimani, bora mimi na wewe tusijadili kabisa suala hili.

Amini unavyoamini, na mimi naamini ninavyoamini, nakuhakikishia na kukuahidi ya kuwa mimi na wewe tutaenda sawa vizuri sana, bila mtafaruk wowote
 
Tatizo wewe unaweka msisitizo kwenye habari ya kuepuka mtafaruku.

Wakati mimi naweka msisitizo kwenye kupata ukweli.

Unanikumbusha mjadala mmoja Unguja. Sheikh akasema "Muislamu haogopi challenge".

Inaonekana unaogopa challenge na unaiangusha imani yako.
 
Mimi siogopi.

Ninachofanya hapa naepusha mabishano, kiasi kwamba nikiendelea, kwa Imani yangu itakuwa kama nakufuru.

Ndicho ninachokiepuka hapa.

Ingekuwa mada nyingine tofauti na Imani, tungepelekana.

Ila kwa hii hapana, itakuwa si kueleweshana bali tutakuwa kama tupo kwenye kilabu cha pombe mbovu, tumeshalewa kisha tunapigishana kelele
 
Ndiyo kuogopa kwenyewe huko.

Imani yako ni dhaifu kiasi kwamba haiwezi kuhimili mjadala.
 
Kutokana na maelezo ha mtoa post... hii ishu ilitokea 2010 na sasa ni 2016, sasa ningetegemea kuona ripoti ya uchunguzi na maamuzi ya mahakama juu ya hili suala.

Ndipo kila mtu ajitathimini juu ya mchango aliotoa juu ya hii issue.
Mashahidi wa Jehovah walishinda hii kesi.
 
safukuzwe tu hawana maana, wanasoma bibilia ipi hao? maandiko yanasema ya kaisari mpe kaisari na ya Mungu mpeni Mungu pia inasema heshimuni mamlaka iliyowekwa,
 
Back
Top Bottom