Yehova witness kutimuliwa kwa kukataza wanafunzi kuimba wimbo wa taifa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yehova witness kutimuliwa kwa kukataza wanafunzi kuimba wimbo wa taifa!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JokaKuu, Jan 12, 2010.

 1. J

  JokaKuu Platinum Member

  #1
  Jan 12, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,781
  Likes Received: 5,022
  Trophy Points: 280
  ..hii sijui imekaaje.

  ..sheria inasemaje kuhusu masuala yenye utata kama haya?.


  Wazungu waliozuia Wimbo wa Taifa kutimuliwa

  Serikali imesema itawafukuza nchini wazungu wa madhehebu ya Mashahidi wa Yehova kwa kujihusisha na vitendo vya kuwashawishi wazazi katika kijiji cha Nkala, Wilaya Mbozi mkoani Mbeya na kuwazuia wanafunzi 300 kuimba wimbo wa taifa shuleni.

  Kauli hiyo ya Serikali ilitolewa jana jijini Dar es Salaam siku chache baada ya kuripotiwa kuwa waumini wa madhehebu ya Mashahidi wa Yehova wamewazuia watoto kuimba Wimbo wa Taifa wakati wakiwa shuleni.

  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza, alisema jana kuwa kitendo cha wanafunzi kukataa kuimba Wimbo wa Taifa ni sawa na uhaini.

  Alisema Serikali itawafukuza nchini wazungu hao ikipata ushahidi kuwa ndiyo wanaoshawishi wazazi kuwazuia watoto wao kuimba wimbo huo.

  Alisema amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na viongozi wengine, kwenda kijijini hapo kufanya uchunguzi kubaini sababu za wazazi kuwakataza watoto wao kuimba wimbo huo. "Kila nchi ina Wimbo wake wa Taifa na hicho ndicho kitambulisho cha utaifa hivyo kitendo cha kuzuia wanafunzi kuimba maana yake watoto hao wanakana utaifa wao," alisema Mahiza.

  Kwa mujibu wa mmoja wa waumini wa madhehebu hayo kijijini hapo, imani ya dini yao haiwaruhusu kuimba Wimbo wa Taifa wala kuisujudia Bendera kwa kuwa huyo si Mungu wao na kwamba wanaye Bwana mmoja tu ambaye ni Kristo.

  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Nkala, Syliverster Mpemba, alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kuongeza kuwa tangu 2007 watoto hao walipogoma kuimba Wimbo wa Taifa na kufukuzwa shule hawajaandikishwa wanafunzi kwa ajili ya kuanza darasa la kwanza.

  Alisema tangu mwaka 2007 idadi ya wanafunzi katika kijiji hicho imekuwa ikishuka kwa wastani wa watoto 90 ambao wazazi wao wanatoka madhehebu ya Mashahidi wa Yehova.
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,186
  Trophy Points: 280
  Hivi Tanzania tuna separation of church and state?

  What's next, mtataka tuombe kwa jina la Kikwete?

  Kama mtu dini yake haiamini kuimba wimbo wa taifa mwacheni.

  This is a clear issue of draconian religious persecution.

   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kiranga,
  Hapana. Hakuna cha Draconian hapa. Hata Biblia inasema mpe Kaisari kilicho chake. Kama hawa wazungu wanataka watu wasiimbe wimbo wa taifa waanzie kwao. Sio kuwadanganya watoto wetu. Hawa mawitness nakumbuka miaka ya 60 walifukuzwa Tanzania na Malawi kwa uhalifu huo huo.
   
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,186
  Trophy Points: 280
  Biblia hiyo hiyo, tena kwenye amri kumi, imesema

  Wimbo wa taifa ni kulisujudia taifa.

  Marekani Jehovah Witnesses wameshinda hii case, kwa hiyo hii pointi yako ya waanzie kwao ni moot.

  Tukiwakatalia hapa ni kuonyesha nchi yetu ilivyo totalitarian tu na isivyo na freedom of worship.

  What's next? Tutataka kuwakusanya watu wote saa fulani waimbe wimbo wa taifa? This is sheer Maoism.
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  na tukiwakubalia tunaanza kukaribisha uasi kwa misingi ya dini. Anarchy will rule. Hapana, hakuna sheria ya kuwakusanya kwa nguvu watu wote waimbe wimbo wa taifa, lakini pale inapohitajika au inapobidi sitaki kusikia kuwa Jehova Witness hataki. Hata mimi ni Mkristo. Yesu alifumbua yote. Alituasa tuwe watiifu kwa Kaisari na huku tukiwa wafuasi wake.
   
 6. October

  October JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Wimbo wa taifa si Kusujudia taifa,
  Ungeweka Quotation ya Mstari wa Biblia uliotumia ningeweza kuchangia zaidi.

  Kweli siungi mkono swala la kukataa kuimba wimbo wa taifa, lakini vilevile kuwafukuza viongozi wa dini kwa vile tu wamekataa kuimba wimbo wa taifa ni uonevu.

  Yule Shehe Mjamaika mwenyewe ambae anajulikana kwa kuchochea mauaji hakufukuzwa Tanzania sembuse hawa watu ambao hawamdhuru binadamu?

  Yapo maovu mengine yanayostahili kufukuzwa lakini sio hili la hawa watu.
   
 7. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #7
  Jan 12, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,186
  Trophy Points: 280
  Tatizo ukristo unaji contradict, huku kwenye amri kumi unaambiwa usimsujudie yeyote zaidi ya mungu, huku Yesu anasema mpe Kaizari ya Kaizari.

  Hapa hamna anarchy, kwa sababu hamna evil intention, watu wanataka peacefully ku sit out sujuda hizi za serikali, dini yao inawakatataza.Mnaweza kuwalazimisha, lakini mtakuwa kama Nebuchadnezzar aliyewapitisha Daniel Meshack na Abednego kwenye tanuri la moto (supposedly).

  Ukishaanza kuwalazimisha watu kuisujudia serikali unaanza religious persecution.

  Serikali kama inafanya mambo yake murua mbona hao Witnesses hata asilimia moja hawafiki? Wawaache hao na wengine wote wasiotaka kuimba huo wimbo wachill kivyao, ama sivyo Tanzania ikubali kwamba ni nchi totalitarian inayoshurutisha watu kutenda visivyo kwa mujibu wa dini zao.

  Haya mambo yashaongelewa US tangu enzi za kabla ya Vita Vikuu vya kwanza

  http://en.wikipedia.org/wiki/Persecution_of_Jehovah's_Witnesses_in_the_United_States

  http://en.wikipedia.org/wiki/United_States_Supreme_Court_cases_involving_Jehovah%27s_Witnesses
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,186
  Trophy Points: 280
  Kusujudia maana yake nini?
   
 9. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #9
  Jan 12, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,186
  Trophy Points: 280
  Kwanza wimbo wa taifa wenyewe uko discriminatory.

  Unaanza kwa kusema "Mungu ibariki Tanzania"

  Sasa na sisi tusioamini mungu si tutaona huu wimbo ni kichaa kitupu, tukisema hatutaki kuimba on this ground utatulazimisha?
   
 10. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #10
  Jan 12, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  "Mungu ibariki Tanzania, wabariki viongozi wake, hekima, umoja na amani....."

  Mungu wa kwenye wimbo wa Taifa ni mungu gani, wawakristo, waislam au wapagani.?

  Serikali ya Tanzania siyo ya kidini, huyu mungu kwenye wimbo wa Taifa ni mungu yupi, au Tanzania kama Taifa lina mungu wake?
   
 11. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #11
  Jan 12, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kiranga,
  Ukristo hauko contradictory. Ukisikia aliyoyasema Yesu katika Agano Jipya ni kwamba alikuja kuimarisha yale ambayo Musa aliyaweka. Kwa mtaji huu, falsafa ya Yesu ina mshiko zaidi. I would not call it contradictory but rather evolutional.
   
 12. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #12
  Jan 12, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,186
  Trophy Points: 280
  Kama alikuja kuimarisha ya agano la kale mbona agano la kale linasema clearly kwamba mungu ana wivu, na msimsujudu mwingine, na Yesu anasema Kaisari akitaka kusujudiwa poa tu?

  Kuna contradictions kibao kati ya old and new testaments, don't even go there.

  Tena contradiction nyingine humo humo old testament

  Hebu ona hapa

  http://skeptically.org/newtestament/id19.html
   
 13. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #13
  Jan 12, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwani tumeshafikia hatuwa ya kila mtu afanye kwa mujibu wa dini yake inavyomtaka? Au kwa dini hii tu?
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Jan 12, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Good question!
   
 15. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #15
  Jan 12, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,186
  Trophy Points: 280
  Si tunajidai hatuna religious persecution?

  As long as hakuna evil intention, kila mtu afanye kwa mujibu wa dini yake.

  Anayeabudu mti poa, anayekataa kuimba wimbo poa.

  Kwani wasipoimba atakufa mtu?

  Ukoloni tu!
   
 16. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #16
  Jan 12, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Mbona unautumia vibaya uhuru wa kutowa mawazo? Naona unachofanya hapa ni kujionyesha kuwa una mabwana zako unaowaweka mbele zaidi ya Taifa.
   
 17. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #17
  Jan 12, 2010
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mbona mnawaonea hao jehovah...? Tanga wanafunzi wa kiislam hukatazwa kuimba wimbo wa taifa hata kutoa mchango wa mwenge kisa eti wimbo wa taifa ni wakikristo na mwenge eti dhumuni lake ni kueneza ukristo....hao ni wanafunzi wa advance sio primary....najua baadhi yao watakkuwepo humu...tunawasubiri mjibu hizi tuhuma....
   
 18. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #18
  Jan 12, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,186
  Trophy Points: 280
  Tuheshimiane,

  Patakuwa hapakaliki hapa, ohooo.Mwanaume kuambiwa ana bwana tusi.

  Taifa? Taifa liko wapi? Hao illuminati wanaowachezeeni katika mchezo wa redio mjione mna kitu kinaitwa taifa ndio washawateka akili?

  Siku hizi hamna taifa, na hii si Tanzania tu, mpaka Marekani, mambo ni mwendo wa ma Corporatocracy tu, ma Halliburton yashachukua kila kitu, wewe unabaki na concept za Westphalia za 1600 huko!
   
 19. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #19
  Jan 12, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mbona hawatafukuzwa kwa kukataa kuimba wimbo wa Taifa? Pengine hujaisoma hii habari bora ungesoma tena na baadae unaweza kuja tena na kajitabia chako cha udini tupo tayari kukusikiliza.
   
 20. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #20
  Jan 12, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Samahani sana lakini naomba nijuulishwe. KUSUJUDI ni kitendo gani?
  Ama katika dini yangu ya kiislamu kusujudi ni kupiga magoti na kuerka kipaji cha uso aridhini, jee wenzetu katika dini yenu kusujudi ni huko au la?
   
Loading...