Yaya Toure amshutumu Pep Guadiola kuwa anawabagua wachezaji kutoka Afrika

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,399
AAyeehr.img

Yaya Toure

Kuna baadhi ya watu wakizungumza kitu basi lazima dunia isimame na iwasikilize hata kama wanazungumza maneno machache sana. Mmoja wa watu wa aina hiyo ni Yaya Toure ambae ni mchezajj nyota wa zamani wa kiungo anaeweza kuitwa "Maestro".

Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Manchester City ya Uingereza na timu ya taifa ya Ivory Coast Yaya Toure, amemshutumu vikali meneja wa timu ya Manchester City kuwa ni mmbaguzi kwa wachezaji kutoka Afrika.

Akizungumza na jarida ya France Football baada ya kuondoka rasmi kwenye timu hiyo ya Uingereza ambayo imekuwa bingwa tena kwa msimu wa 17/18, Yaya Toure ametoa shutuma hizo kwa Guadiola kwamba amekuwa mbaguzi katika timu za Barcelona na Manchester City dhidi ya waafrika na ameapa kuvunja imani hiyo ya Guadiola.

Mchezaji huyo wa kiungo wa kimataifa ambae amekaa Machester City kwa miaka nane alijiunga na timu hiyo kutoka Barcelona ya Hispania mwaka 2010 ambapo timu hiyo ilikuwa chini ya Guadiola na kwamba ni uamuzi wa Guadiola ndiyo uloruhusu yaya Toure kusajiliwa na Machester City.

Toure mwenye umri wa miaka 35 na ambae pia kwa sasa ni mchezaji wa zamani wa Ivory Coast amesema Guadiola alipokuja Machester City aliamua kwa makusudi kutomchezesha kabisa katika kampeni zote za ligi kuu na hata ile ya kombe la FA la Uingereza kwa sababu tu ya wivu dhidi yake.

Toure amedai katika mahojiano na jarida hilo la France Footbal kwamba si yeye tu kama mchezaji kutoka Afrika ambae anamfikiria hivyo Pep Guadiola bali wachezaji wengi tu kutoka barani humo wana mawazo hayo hasa kwenye ligi la Uhispania ya La Liga.

433ff.jpg


Toure anasema anataka kuvunja imani hiyo ya Guadiola na anahisi ni wivu na kutaka kumdidimiza mtu mwingine kwa makusudo ya kumvunja moyo.

Anasema kwamba, “kuna wakati huwa tulikuwa tukitizamana kwa namna ya ajabu kana kwamba tuna ugomvi na nilipomkazia macho alikuwa anaonyesha woga na wasiwasi“

Toure anaamini kwamba alitakiwa acheze msimu wote wa 17/18 bila shida lakini badala yake anasugua kiti cha wachezaji wa akiba na huku Guadiola akimsifia kwa vyombo vya habari kuwa ni mchezaji mwenye mchango mkubwa kwa timu yake huku akiwa hachezeshi.

Toure alinza mechi moja tu dhidi ya Brighton na hata kwenye fainali ya kombe la FA dhidi ya Arsenal aliachwa nje licha ya kucheza fainali nne mfululizo kabla ya Guadiola kuja City.

Yaya Toure anasema Guadiola amemnyang’anya nafasi ya kuwaaga wapenzi na mashabiki wa Machester City na alikuwa anapenda aje aagwe kama Andre Iniesta kule Barcelona au Gialuigi Buffoon pale Juventus ambao wameagwa kwa heshima zote.

Anasema “hiyo ni roho mbaya sana na ukatili, unadhani hali hiyo ingeruhusiwa kutokea kwa Iniesta pale Barcelona?”

Toure anasema kwamba ipo siku anasubiri kuona Pep Guadiola akipanga timu yake yenye wchezaji watano wa kutoka Afrika na waso raia wa nchi za Ulaya kama yeye na ikifika siku hiyo atatoa zawadi ya keki.

Akielezea tabia halisi ya Guadiola ni kwamba anapenda kutawala bila kujibiwa na kuna wachezaji ambao wanakuwa radhi kulamba mikono yao kuonyesha kumnyenyekea.

Anasema yeye hayuko tayari kwa aina hi ya uhusiano ingawa namheshimu Guadiola kama meneja wake.

Pep Guadiola ana mtindo wake wa uchezaji ambapo humtumia mchezaji mmoja tu wa kiuongo na mara nyingi katika timu alizopanga alikuwa akimtumia sana MBrazil Fernandihno kama kiuongo mkabaji wake.

NB: Mahojiano ya Yaya Toure yapo kwenye jarida ya France Football.

France Football , toute l'actualité du football
 
Huyu jamaa ni mbaguzi haswaaa sitosahau alivyomtosa Samuel Eto wa Cameroon wakati alivyokuwa kwenye kiwango bora cha juu wakichukua vikombe vitatu mwaka msimu wa mwaka 2008-2009 pamoja na Champions League na akifunga goli la kwanza kwenye fainali dhidi ya Manchester United na akiwa ni mfungaji bora wa Barca.

Mwaka uliofutia akamlazimisha aende Inter Milan ya Jose Mourhino ili amchukue Zlatan Ibrahimovic, Mungu ni mwema wakakutana nusu fainali na Barcelona mwaka uliofuatia , yaliyobaki ni historia, Barca ikabanjuliwa na Inter milan na ikaenda kuchukua ndoo tatu pamoja na Champions League! na Eto yule yule aliyemwona si lolote.
 
Etoo alilazimishwa kwenda inter pesa juu na zlatan ili tu atoke barcelona na etoo alikuwa kwenye kiwango bora kabisa
Kuna interview moja ya etoo iko YouTube alimponda Pep vibaya sana.

Anasema mwanzoni pep akumsalimia wala kumsemesha walipokuwa vyumbani walipotoka nje kwa waandishi wa habari akataka kumsalimia kwa kumkumbatia etoo akamkatalia akasepa zake.
 
Kuna interview moja ya etoo iko YouTube alimponda Pep vibaya sana.

Anasema mwanzoni pep akumsalimia wala kumsemesha walipokuwa vyumbani walipotoka kwa waandishi wa habari akataka kumsalimia kwa kumkumbatia etoo akamkatalia akasepa zake.
Huyu jamaa ukatalunya umemkaa vibaya nafikir hata wakina ramos atakuwa hawapend
 
Jamaa dume zima lina mambo ya ajabu kabisa. sijui anajihisi kama anakiwango kama cha iniesta au modric nahisi.

Kuna kipindi alinuna kisa timu haijamfanyia birthday !!!!!!!!!

Lakini si alicheza na Iniesta pale Nou Camp?
 
Jamaa dume zima lina mambo ya ajabu kabisa. sijui anajihisi kama anakiwango kama cha iniesta au modric nahisi.

Kuna kipindi alinuna kisa timu haijamfanyia birthday !!!!!!!!!

Kubali au ukatae, Yaya Toure ndiye alikuwa mchezaji influential sana Manchester City wakati wa Roberto Mancini na Emmanuel Pellegrino.

Au umesahau hiyo?
 
Back
Top Bottom