Yawezekana Rais amevunja sheria ya Mchakato wa Katiba kwa kuwaapisha kina Baregu?

Mkuu MM,
Kama umebahatika kupata hiyo Amendment utubandikie, plse!

mtasababisha tatizo kubwa sana kwa Bunge; vyote vilivyosemwa Bungeni vipo kwenye hansardi humo. Mjanja1 na EMT wameweka mijadala yote; mtu akitaka kusoma aingie kwenye hansard za Feb 8, 2012 ajisomee mwenyewe mtaona ni ni Bunge lilikubaliana (soma majibu ya Waziri wa Bunge, Sera). Sasa ikiandikwa sheria nje ya yale yaliamuriwa na Bunge ni tatizo kubwa zaidi kwani tumeshalina tena mwaka jana ambapo serikali ilidaiwa kuingiza maneno kwenye sheria ambayo wabunge walikuwa hawajakubaliana.
 
ndio lakini wabunge na wawakilishi wanakatazwa!

Hapana MM, wabunge na wawakilishi ruksa! labda twende taratibu, 6.5 yote ni hii hapa

6(5) Notwithstanding subsection (3), a person shall not qualify for appointment as a member of the Commission if that person is:
(a) a Member of Parliament, a Member of the House of Representatives of Zanzibar, a Councilor or a leader of a political party of any category;
(b) a member of security organs;
Composition of the Commission
Terms of Reference
(c) a person who has been convicted of, or is the subject of proceedings in the court of law for an offence involving dishonesty or moral turpitude; or
(d) a non-citizen of Tanzania.

Sasa mabadiliko ni haya na kimsingi mabadiliko haya yalifuta kabisa (yali-delete) 6(5)(a) ambayo ilikua inawapiga marufuku au inawaondoa wabunge na wawakilishi kutoka zanzibar kuteuliwa kuwa miongoni mwa wajumbe wa tume

MHE. CHRISTOPHER O. OLE-SENDEKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi. Nimeleta mabadiliko juu ya jedwali la mabadiliko kama inavyosomeka kwenye karatasi ambayo Wabunge wanayo pale kwenye section (6). Nimeomba tufute sehemu ile ya (a) katika subsection (5) na kwa maana hiyo tunapaswa sasa kupandisha (b) iwe (a) na (c) iwe (b).

Mheshimiwa Zitto aliunga mkono hivi,
MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi ya Upinzani Bungeni haina pingamizi
na mapendekezo ambayo Mheshimiwa Ole-Sendeka ameyaleta. (Makofi)

Mwenyekiti siku hiyo aliuliza;

MWENYEKITI: Unaunga mkono? Kambi ya Upinzani au ni Zitto mwenyewe? Hakuna Kambi
ya Upinzani.

Tundu Lisu naye akasema,

MHE. TUNDU LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, msimamo wetu kama Kambi Rasmi ya Upinzani siku zote imekuwa kwamba Wabunge, Wawakilishi, wanasiasa, wasomi, provided wana uwezo na kuwa na zile qualification za kitaaluma zinazotakiwa, wana haki ya kuteuliwa kuwa Wajumbe wa Tume. Huu ndiyo ulikuwa msimamo wetu tangu mwanzo, na ndiyo ulikuwa msimamo wetu leo asubuhi na msimamo wetu sasa hivi. Kwa hiyo, pendekezo la Mheshimiwa Ole-Sendeka, tunaliunga mkono mia kwa mia

AG nae akafunguka;
MWENASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, inaonekana kuna consensus kwamba Wabunge na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wasizuiwe. Kwa hiyo, sisi tutaiondoa kama ndiyo consensus.

Mambo yakaisha hivi
MWENYEKITI: Mheshimiwa Ole-Sendeka unahitaji kusema chochote? Maana ni kama umekubaliwa.
Tukufu.

MHE. CHRISTOPHER O. OLE – SENDEKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nalishukuru Bunge lako

MWENYEKITI: Nadhani wote wamekubaliana. Ngoja niwahoji. (Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Ibara iliyotajwa hapo juu ilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima pamoja na Marekebisho yake)

Source: Hansard ya Tarehe 8 feb 2012, MM kaweka link hapo juu, mie nilichofanya ni kusoma tu na kumwaga hapa vile vipengele vinatuhusu kwa faida ya mjadala huu na kwa wale wanatumia simu na wasingeweza kufungua hilo li-PDF:)
 
Uswe umeshamaliza mjadala,kikwete na wasaidizi wake wako makini.Maswala ya kujadil kwenye stický hii sasa ni
1.Faìda na hasara za mbunge mwakilìshi kuwa kwenye hiyo tume
2.Cv ya shaima kwegyr
 

Hapana MM, wabunge na wawakilishi ruksa! labda twende taratibu, 6.5 yote ni hii hapa



Sasa mabadiliko ni haya, kimsingi mabadiliko haya halifuta 6(5)(a) ambayo ilikua inawapiga inawaondoa wabunge na wawakilishi kutoka zanzibar kuwa miongoni mwa wajumbe wa tume



Mheshimiwa Zitto aliunga mkono hivi,


Mwenyekiti siku hiyo aliuliza;



Tundu Lisu naye akasema,



AG nae akafunguka;


Mambo yakaisha hivi


Source: Hansard ya Tarehe 8 feb 2012, MM kaweka link hapo juu, mie nilichofanya ni kusoma tu na kumwaga hapa vile vipengele vinatuhusu kwa faida ya mjadala huu na kwa wale wanatumia simu na wasingeweza kufungua hilo li-PDF :)
Yaelekea kulikuwa na mjadala wa mabadiliko kwenye hicho kipengele cha 6 (5) kuruhusu ushiriki wa viongozi wa kisiasa na wabunge/ wawakilishi kwenye tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya. Lakini swali langu ni je hicho kipengele kilichonakiliwa kimetoka kwenye Bill au Act? Kwa kuwa Act ni sheria kamili basi rais atakuwa amevunja sheria kama mabadiliko hayo hayakuingia kwenye muswada wa sheria!
Jambo jingine linalovutia ni mpangilio wa maneno kwenye sentensi wakati wa drafting hasa kwenye sehemu inayosema "...a political leader of a political party of any category"
Hapa kuna shida! Haya maneno "of any category" yana-modify "political party" sio "political leader"! Matokeo yake ni absurdity! Maana iliyokusudiwa imepotea. Sentensi ingesomeka kama "...a political leader of any category of a political party". Naomba kuwasilisha.
 
Huyo hata umwambie nini, mradi tu amponde Kikwete, kwake hata jema la Kikwete ni ovu.

Ni mtu mmoja fitna wa hali ya juu, anaweza kuubadili ukweli na akaufanya uongo na uongo akaufanya ukweli. That is how dangerous he/she is.

nchi inaendeshwa kwa sheria sio mapenzi ya mtu. Kama bunge halikuruhusu wabunge wala wawakilishi kuwa wanatume hapo chuki inatoka wapi jamani? Arafu hapa hatujasema juu ya kikwete tunasungmzia taasisi ya uraisi.

ya cv ya kwig je? Nayo ni chuki?
 
Nadhani hakuna shaka sana kuhusu kilichojadiliwa na kukubaliwa na msingi wa makubaliano hayo. Kama ni kweli wabunge na wawakilishi wanaruhusiwa kuingia kwenye Tume (kama tulivyoona) na watu hao hao wanakuwepo kwenye Baraza la Kutunga Katiba (kwa mfano nina uhakika wanasiasa na watu wengine wengi wataingia kwenye baraza hilo under "political parties representatives) ni kwa kiasi gani mchakato mzima utakuwa umesimamiwa na "wanasiasa"?

Binafsi sijapenda kabisa kuwa wabunge na wawakilishi kuwa wajumbe wa baraza la kutunga Katiba na watu wengine ambao tayari misimamo yao kuhusu katiba inajulikana kuwemo ndani ya Tume ya Katiba. If you look at carefully there is some kind of redundancy!
 
hadi sasa JK amefata sheria, ila namuunga mkono MM kwamba swali sasa ni 'Je, kwa kiasi gani mchakato mzima unasimamiwa na wanasiasa? au kama alivyosema segwanga, zipi ni faìda na hasara za mbunge mwakilìshi kuwa kwenye hiyo tume?

tatizo hapa ni kwamba watunga sheria (hawa wa kwetu) huwa makini sana kwa vitu vinavyohusu maslahi yao, yawe ya uchumi au ya kisiasa, kwa wao ni muhimu interest zao kulindwa (na kwa hili hata ninaowapenda sana CDM hawachomoki). na ndio maana, sheria iliyotungwa iko na mwanya mkubwa sana, na tusipoangalia wanasiasa watatuweka pembeni na wao watatuletea katiba ya vyama vyao
 
hiyo 6.5 ilikua mjadala mkubwa sana lakini ilibadilishwa kuruhusu kila mtu wakiwemo wabunge na wanasiasa
Please do not bring in sweeping statements kwenye mambo ambayo ni serious. Ilibadilishwa lini kuwaruhusu wabunge wawe members wa hiyo tume? Tiba
 
WaTanzania wa2 wa ajabu sana wanasoma na wanafikiria kwa hisia; hakuna jambo lililoongelewa kwa muda mrefu kama hili ni jambo la kusikitisha kwamba haikueleweka kwamba sheria imebadilika... VERY SAD. In fact kusema hivyo ni matusi kwa vyama vilivyopeleka hayo majina kama kweli wanasiasa walikuwa hawastahili. Then ni matusi pia kwa hao wasomi kukubali ki2 ambacho kingekuwa against sheria. Tuache uganga wa kienyeji; kudhani everyday president atakosea... Pls utilize your endowed genius if any into productive thing.

Mkuu usishangae sana, JF imegeuka kitchen party, mahali pa udaku na ukiwekwa jamvini tu.....wachangiaji wanakurupuka kama hawana akili nzuri.

It is a shame.........u-great thinkers ni ndoto tu.
 
Please do not bring in sweeping statements kwenye mambo ambayo ni serious. Ilibadilishwa lini kuwaruhusu wabunge wawe members wa hiyo tume? Tiba

Tiba, we ni mvivu sana wa kusoma? hii comment yako ni bandiko nambari 70 katika huu mjadala, hebu rudi nyuma kidogo usome bandiko langu ambalo ni nambari 64, ukishasoma check na badiko la mtoa hoja MM, ambalo ni bandiko nambari 68, ukishasoma urudi ku-comment
 
It is with regret disapointment bado waanzilishi wa thread wanatetea madudu yao


Soma hapa sheria ya mabadiliko ya katiba ... pamoja na bill of amendment

Mungu wabariki wananchi wa Tanzania wapende kujadili hoja na sio watu.

Ambao hamtasoma ndani nawafanyia urahisi zaidi.
(a) in section 6(5), by deleting in paragraph (a)-(i) a "comma" and substituting for it the word "and"; and​
(ii) the phrase "or a leader of a political party of any category";



Mode: Please delete this Thread, maana inatutia aibu. sisi ndio tunaonekana sio makini badala ya hao tunaowatuhumu
 
Kwenye ile thread ya Mwanakijiji ya kupinga Tume iliyoteuliwa na Rais na kutaka kuwe na baraza la katiba, kuna baadi ya watu walikuwa wanaiponda kwa kwa madai kuwa inamponda Rais. Nakajaribu kuwaambia waje na hoja kwa nini maoni ya katiba mpya yatafutwe na tume badala ya baraza la katiba ambacho ni chombo kinachotumika sehemu nyingi duniani kwenye michakato ya katiba mpya. Hawakutaka kujibu, wakaendelea kumshambulia aliyeleta ile mada.

Lakini kulikuwa na kitu ambacho nili-note kwenye uteuzi wa tume. Sikuwelewa ni kwa nini tume ya kutafuta maoni ya katiba mpya iwe na wabunge ndani yake. Kwa vile tayari mbunge ana kazi yake ya ubunge, sikuelewa angejigawaje kuwa mbunge na pia mjumbe wa Tume ya katiba. Hii tume ya katiba si itakuwa inafanya kazi full time? Kama ni hivyo, huyu mbunge atakuwa anajigawaje kwenye kazi za ubunge na zile za tume?

Hata kama ipo sheria inayomruhusu Rais kumteua mbunge kwenye tume, hiyo sheria itakuwa ina walakini kwa sababu mbunge ni mmoja ya watu ambao nafikiri wataipitisha katiba mpya itakapoletwa bungeni. Sasa inakuwaje mbunge anakusanya maoni ya watu halafu anakuja kuyapitisha tena bungeni?

Wakati anaomba marekebisho yafanywe ili kuruhusu wabunge kuwa kwenye tume Mh Ole-Sendeka alisema kuwa "naamini busara ya Rais itaendelea kutumika katika kuteua Wajumbe hawa wa Tume, kwa hiyo, nikasema niombe Wabunge waniunge mkono katika kuiondoa hiyo sehemu ya (a) ya kifungu kidogo cha (5) katika kifungu cha (6) cha Sheria hiyo na katika mabadiliko hayo kama ambavyo nimependekeza."

Mh Ole-Sendeka aliendelea kusema "nilikuwa najaribu kuona kwamba kizuizi hiki ukisema tu kwamba unawaondoa Wabunge Wawakilishi, lakini unasema viongozi wa kisiasa waingie, Wabunge pia ni viongozi wa kisiasa, lakini na Rais atatumia busara kwa sababu nafasi ni 16 Bara, na 16 upande wa Tanzania Zanzibar"

Kwa hiyo, sababu mbili zilizofanya kuruhusu wabunge kuwa kwenye tume ni (a) wabunge nao ni wanasiasa na(b) Rais atatumia busara zake katika kuteua watu watakaounda tume. Kuhusu sababu ya kwanza, ni muhimu kujua pia kuwa wabunge wanatofautiana sana na wanasiasa wengine. Wabunge ni watunga sheria pia. Ni hawa hawa wabunge ambao watakaa chini na kuipitisha katiba mpya. Kigezo hiki tuu kinawazuia wabunge kuwa kwenye tume ya katiba. Pia kusema kuwa wabunge nao ni wanasiasa kwa nini tume yenyewe iwe ya kisiasa in the first place? Hapa sio kama mchakato mzima unachukuliwa mikononi mwa wananchi na kupewa watu wachache ambao ni wanasiasa?

Sababu ya pili kuwa Rais atatumia busara zake, hapa bunge lilikuwa linampa Rais "discretion" ya kuteua wajumbe wa tume. Hapa ndipo linapokuja tatizo lile lile la kumpa Rais madaraka makubwa. Ukiangalia malalamiko mengi yanayotolewa na watu na hasa wapinzani juu wajumbe wa tume yanatokana Rais kupewa madaraka makubwa katika kuteua wajumbe. Lakini stili hawa hawa wapinzani walimpa Rais madaraka hayo makubwa kupitia mlango wa wani. Mpaka Zitto mwenyewe kama alijichanganya:

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi ya Upinzani Bungeni haina pingamizi na mapendekezo ambayo Mheshimiwa Ole-Sendeka ameyaleta. (Makofi)
MWENYEKITI: Unaunga mkono? Kambi ya Upinzani au ni Zitto mwenyewe? Hakuna Kambi ya Upinzani.

Wapo watakauliza whether or not Rais ametumia busara katika kuteua wajumbe wa tume. Tayari kuna ambao wame-raise allegation za mjumbe mmoja. Lakini kwangu bado sijaona sababu ya msingi ya kutafuta maoni kwa kupitia tume in the first place. Ndiyo maana baadhi tumekuwa tukisizitiza kuwa tokea mwanzo mchakato mzima wa katiba mpya ulikuwa haujakaa vizuri. Mbona hata Egypt na Tunisia wanatumia Baraza la Katiba kutengeneza katiba zao mpya? Kwa nini sisi tumeamua kutumia tume? What is so special with commissions?
 
It is with regret disapointment bado waanzilishi wa thread wanatetea madudu yao


Soma hapa sheria ya mabadiliko ya katiba ... pamoja na bill of amendment

Mungu wabariki wananchi wa Tanzania wapende kujadili hoja na sio watu.

Ambao hamtasoma ndani nawafanyia urahisi zaidi.


Mode: Please delete this Thread, maana inatutia aibu. sisi ndio tunaonekana sio makini badala ya hao tunaowatuhumu[/SIZE][/FONT][/SIZE][/FONT]

Mkuu suala la kuwaruhusu wabunge kuteuliwa kwenye tume halipo kwenye hizo documents mbili ulizoweka hapo juu. Those are old documents. Ukisizisoma zinaruhusu wanasiasa lakini bado zina-exluclude wabunge kuwepo kwenye tume. Suala la wabunge kuwepo kwenye tume liko kwenye Hansards za bunge kama Mkuu Uswe alivyoziweka hapo juu kwenye post number 64. Kama ungeweza kutupa the lastest Constitutional Review Act 2001 as amended by the Constitutional Review (Amendment) Act 2001, ingekuwa poa sana.
 
political expediency............ndiyo ugali wetu mchana na usiku.............tunapenda njia za mkato kujibu shida za leo.........
 
Mkuu suala la kuwaruhusu wabunge kuteuliwa kwenye tume halipo kwenye hizo documents mbili ulizoweka hapo juu. Those are old documents. Ukisizisoma zinaruhusu wanasiasa lakini bado zina-exluclude wabunge kuwepo kwenye tume. Suala la wabunge kuwepo kwenye tume liko kwenye Hansards za bunge kama Mkuu Uswe alivyoziweka hapo juu kwenye post number 64. Kama ungeweza kutupa the lastest Constitutional Review Act 2001 as amended by the Constitutional Review (Amendment) Act 2001, ingekuwa poa sana.

EMT, unahoja kidogo kuhusu uwakilishi... however, the point is ukisoma kwa makini hiyo ni "bill" ......then malizia mwenyewe....
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Mwanakijiji,

Utetezi # 1:

..inawezekana Raisi haijui sheria kwasababu hakuisoma.

..lakini Raisi ana nia nzuri tu ktk uteuzi huo.

Utetezi # 2:

..Raisi ni mchumi kitaaluma, siyo mwanasheria.

..washauri wake wamemuangusha.

Hii ya kuangushwa angushwa tu kwenye kila kitu, kwani tuna raisi gogo.
 
EMT, unahoja kidogo kuhusu uwakilishi... however, the point is ukisoma kwa makini hiyo ni "bill" ......then malizia mwenyewe....

Mkuu nitakachoeleza hapo chini kinaweza kuwa purely academic for now, lakini may help in future.
Waziri husika alileta bungeni these amendments:

The Constitutional Review Act, 2011 is amended as follows:
(a) in section 6(5), by deleting in paragraph (a)-
(i) a "comma" and substituting for it the word "and"; and
(ii) the phrase "or a leader of a political party of any category";

Sasa ukilangalia hapo, amendment ilikuwa inaruhusu viongozi wanasiasa wa chama chochote cha siasa lakini sio wabunge. Ndio maana pale mwishoni hiyo Bill ilikuwa inasema:

This Bill propose amendments to sections 6 ...... of the Constitutional Review Act, 2011 for two purposes: First, debarring from appointment as Commissioners members of the public who are not Members of Parliament, members of House of Representatives of Zanzibar or Councilors.

Sasa wakati majadiliano bungeni, ndipo Mh Ole Sendeka akaja na hoja kuwa wabunge/wawakilishi nao waruhusiwe kwenye tume kwa sababu nao ni wanasiasa. Kama Hansard zinavyoonyesha, hoja yake ilikubaliwa na kupitishwa na bunge. Kwa hiyo, suala la wabunge kuwepo kwenye tume, kwa mujibu wa Hansards za bunge, halina mjadala.

Lakini mie nilichokuuliza ni kama ungeweza kutupatia the latest Constitutional Review Act 2001 as amended by the Constitutional Review (Amendment) Act 2001, ingekuwa poa sana. Kwa sababu hizi tunayoitumia hapa ni ile ambayo ilikuwa bado kuwa amended.

Halafu kwa upande wako bado una-rely kwenye bill ambayo bado ilikuwa haijawa sheria. Kama ulivyoona kwenye Hansard za bunge, bill inaweza kufanyiwa mabadiliko makubwa makubwa wakati inajadiliwa bungeni. So, what I was asking, was not the bill, but the actual Constitutional Review (Amendment) Act 2001 which was passed by the legislature. The bill is not authoritative, but the actual Act is. Hansards inatusaidia tuu kujua the intention of the legislature in passing that particular law or a section of the the law.
 
MM and JF
Nilikwisha sema ya kwamba Jakaya Mrisho Kikwete is not serious and many of you folks don't even want to commend. Amejaza team ya wasanii and most of them ni waganga njaa. Kuanzia Waziri Mkuu, Maofisa watendaji Ikulu, Mawaziri Katibu Wakuu, Mwanasheria Mkuu and mpaka Majaji ambao hawajawahi kuamua hata kesi ya Kuku? Anavunja sheria Kila siku left and right including hata hiyo katiba anayotaka kuitengeneza.just go and read CAG report over a trillion has been spent by verbal orders from him na Mkulo a state/Govt boy is just laughing. Why the hell do you go on inventing the wheel hata tungedesa ila format kutoka kwa akina Mwai Kibaki it could have done but let us wait and see! Nyie Watanganyika tutumie bongo. Uwiano wa Bara na Zanzibar bado unaumiza kichwani !
 
Back
Top Bottom