Yawezekana Rais amevunja sheria ya Mchakato wa Katiba kwa kuwaapisha kina Baregu?

Muswada wa mabadiliko ya sheria inayohusu uanzishwaji wa katiba uliondoa zuio la wanasiasa kuteuliwa na rais. Thread hii haina maana tena kwani muanzishaji amekiri kuwa alinukuu vifungu kabla ya mabadiliko. THREAD CLOSED
 
Mjanja1, nashukuru kwa kupitia hansard hivyo; inaonekana basi kama mabadiliko yamekuwa kama yalivyo kina Baregu wanaweza kuwa sahihi kuingia kwenye tume lakini mbunge na mwakilishi hawakutakiwa kuingia siyo?

hapana MM, hata wabunge kuwepo ni sahihi, nakumbuka ole sendeka alipigania sana hii issue pale iliporudi bungeni kwa mara ya pili, nasikitika tu kwamba sijapata bado kumbukumbu kutoka records za bunge, ila bado ninapekua
 
MM, aise asante kwa kuanzisha mjadala huu, umeonyesha umakini wako. Sasa haya ya cv ya uongo tena? Mh! Najizuiya kuamini ni kosa kubwa namna hi la kikatiba kwa mku wa nchi kulifanya. Raisi kwenye hotuba nilimsikia akisema kwa kuwa hajasikia minong'ono alihesabu kuwa wajumbe wa tume wanakubalika, hi pekee haitoshi kutoa ruhusa ya kufanya makosa kwa kisingizio cha kutokuwepo kwa maneno mtaani kuhusu mjumbe wa tume. Binafsi nachelda kuamini kosa hili limefanyika. Wenye aces na amended constitution review act watuwekee hapa tuone namna ya kurekebisha jambo hili. Pamoja na critics zote, tushiriki kujenga na kurekebisha makosa senstive kama haya.
 
Sisi Wavivu wa kufuatilia mambo kwa undani and yet tunaamini sisi ndio wenye akili. In short sheria ilishabadilishwa na hiyo hoja ilitoka kwa CDM. Kasome amendment za sheria hiyo kwenye tovuti ya bunge... Ni jambo la kawaida kuacha original act. Na kuweka schedule ya amendments....

hiki ndio nachosema, ilipita amendments kuruhusu wanasiasa, siwezi kuisahau ile siku, niliganda kwenye tv karibu siku nzima, kwa hili jamani JK hajavunja sheria, ngoja twendelee kupekua record za bunge, tutamwaga taarifa hapa
 
Hapa ndipo ninapopata walakini na wawakilishi wetu kule Bungeni.Wegine ni member humu ndani JF lakini hawaji au haweweki document ya ukweli ilituweze kujadili vizuri.Lakini wakiguzwa wao kama wao wakofasta kujibu mashambulizi.P/se Myika,Zito etc you must be reading this thread come with the Amendment doc and save Us time.
 
hiki ndio nachosema, ilipita amendments kuruhusu wanasiasa, siwezi kuisahau ile siku, niliganda kwenye tv karibu siku nzima, kwa hili jamani JK hajavunja sheria, ngoja twendelee kupekua record za bunge, tutamwaga taarifa hapa

Mkuu unaposema ilipita amendment kuhusu "wanasiasa" unamaanisha pia wabunge?
 
Hiki kipengele cha kuwaengua wanasiasa katika tume ya katiba kiliondolewa katika marekebisho yaliyofanywa na bunge mwezi wa February mwaka huu.
 
mtunga sheria ndio..........................., nimesoma maoni yenu, ila je nini kifanyike maana naona tayari watu wameshaapishwa na kisheria wanatakiwa kuanza kazi mara 1.
 
Amendments zilizoletwa bungeni mwezi February 2012, ni hizi hapa. Kama marekebisho yalipitshwa kama yalivyoletwa bungeni, basi inaelekea wabunge hawawezi kuteuliwa kwenye tume. Kimsingi hata bila hii sheria sio busara tume anyway. That is common a sense. Kuna wabunge hapa watatuambia unless kama walikuwa wamelala. Waziri wa sheria aliwasilishwa bungeni mswada huu wa marekebisho.

Kwa Kiswahili

Muswada kwa Ajili ya kufanya marekebisho katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011.

1. Sheria hii itaitwa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 na itasomwa ikiwa ni sehemu ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka, 2011.

2. Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 inafanyiwa marekebisho kama ifuatavyo:
(a) katika kifungu 6(5), kwa kufuta katika aya ya (a) -
(i) "mkato";
(ii) maneno "au kiongozi wa chama cha siasa katika ngazi zote";


(b) katika kifungu cha 18, kuongeza masharti yafuatayo mara baada ya kifungu kidogo cha (5):

"(6) Kwa madhumuni ya kifungu hiki, Tume inaweza kuruhusu asasi, taasisi au makundi ya watu kuandaa mikutano kwa ajili ya kutoa fursa kwa wanachama wake kutoa maoni yao juu ya Rasimu ya Katiba na kisha kuwasilisha maoni hayo kwenye Tume."

MADHUMUNI NA SABABU


Muswada huu unapendekeza kufanya marekebisho katika vifungu vya 6 na 18 vya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 kwa sababu mbili. Kwanza kuondoa kizuizi cha kutoteuliwa kuwa Wajumbe wa Tume baadhi ya watu ambao si Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar au Madiwani.

Pili, kuruhusu asasi, taasisi au makundi ya watu kuandaa mikutano kwa ajili ya kutoa fursa kwa wanachama wake kutoa maoni yao juu ya Rasimu ya Katiba na kisha kuwasilisha maoni hayo kwenye Tume

In English

An Act to amend the Constitutional Review Act, 2011.

1. This Act may be cited as the Constitutional Review (Amendment) Act, 2011 and shall be read as one with the Constitutional Review Act, 2011.

2. The Constitutional Review Act, 2011 is amended as follows:
(a) in section 6(5), by deleting in paragraph (a)-
(i) a "comma" and substituting for it the word "and"; and
(ii) the phrase "or a leader of a political party of any category";


(b) in section 18, by adding the following provision immediately after subsection (5):
"(6) For the purpose of this section, the Commission may allow organisations, associations or groups of persons to convene meetings in order to afford opportunity to its members to air their views on the Draft Constitution and forward such views to the Commission.

This Bill propose amendments to sections 6 and 18 of the Constitutional Review Act, 2011 for two purposes: first, debarring from appointment as Commissioners members of the public who are not Members of Parliament, Members of House of Representatives of Zanzibar or Councilors. Secondly, it is sought to allow organizations, associations and groups of persons to collect views of their members on the Draft Constitution and forward such views to the Commission.

Alipowasilisha hayo marekebisho waziri wa sheria alisema

Mheshimiwa Spika, Muswada huu unapendekeza kufanya marekebisho katika vifungu vya 6, 12, 13, 17, 18 na 21 vya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011. Lengo la mapendekezo haya katika vifungu hivyo ni kuondoa sharti la Viongozi wa Vyama vya Siasa, kwa ngazi yoyote kutoteuliwa kuwa Wajumbe wa Tume; kumruhusu Rais kualika Vyama vya Siasa vyenye usajili wa kudumu; Mashirika ya Dini, Taasisi, Asasi na makundi mengine ya watu wenye malengo yanayofanana kutayarisha Orodha ya Majina ya Wajumbe ili Rais achague miongoni mwao Wajumbe wa Tume; na kuainisha utaratibu wa kumwondoa Kamishna wa Tume na kuruhusu Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa, Wakurugenzi wa Manispaa na Makatibu wa Mabaraza ya Miji au Wilaya, kupokea taarifa za programu zitakazoendeshwa katika maeneo yao, badala ya Wakuu wa Wilaya. Aidha, marekebisho hayo yanalenga pia kuruhusu Jumuiya, Asasi, Taasisi au makundi ya watu yenye malengo yanayofanana kuandaa mikutano kwa ajili ya kutoa fursa kwa ajili ya kukusanya maoni juu ya Rasimu ya Katiba na kisha kuwasilisha maoni hayo kwenye Tume.

Mheshimiwa Spika, katika Jedwali la Marekebisho, tunapendekeza kuwa Ibara ya pili ya Muswada ifanyiwe marekebisho kwa kuiandika upya. Lengo la mapendekezo hayo ni kuondoa kizuizi kwa Madiwani kuwa Wajumbe wa Tume. Kwa kuwa Madiwani hawataingia katika hatua ya Bunge Maalum la Katiba, tunapendekeza kuwa wasizuiwe kuwa Wajumbe wa Tume iwapo itaonekana kuwa wapo wenye sifa za kuteuliwa kuwa Wajumbe wa Tume. Jedwali la Marekebisho linapendekeza kuongeza masharti katika Ibara hiyo ya pili ya Muswada kwa kuongeza masharti mapya katika kifungu cha sita cha Sheria ya Marekebisho ya Katiba. Masharti yanayopendekezwa yanalenga kumwezesha Mheshimiwa Rais kuvialika Vyama vya Siasa, Mashirika ya Kidini, Asasi za Kiraia, Jumuiya, Taasisi na makundi mengine yenye malengo yanayofanana, kumpatia orodha ya majina, ambayo miongoni mwao Rais atateua Wajumbe wa Tume.
 
du nimefuatilia maoni ya wanaJF na nikikumbuka mchakato wa nani awe kwenye tume hiyo napata wasiwasi wa washauri wa raisi kutokuwa makini. Ki kawaida Raisi anawajibu kwa mambo mengi ndo maana anakuwa na wadau wa kumshauri mambo husika na kuyapitia kwa hapa wamemdanganya. Hili ndo tatizo kubwa kwa nchi yetu kutokuwa makini katika yale tuliyoamua!
 
du nimefuatilia maoni ya wanaJF na nikikumbuka mchakato wa nani awe kwenye tume hiyo napata wasiwasi wa washauri wa raisi kutokuwa makini. Ki kawaida Raisi anawajibu kwa mambo mengi ndo maana anakuwa na wadau wa kumshauri mambo husika na kuyapitia kwa hapa wamemdanganya. Hili ndo tatizo kubwa kwa nchi yetu kutokuwa makini katika yale tuliyoamua!
 
yes, including wabunge chief.

Mkuu unajua Waziri wa sheria alivyowasilisha the amendments bungeni alipendekeza, pamoja na mambo marekebisho mengine, kufanya marekebisho katika kifungu cha 6 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 kwa kuondoa kizuizi cha kutoteuliwa kuwa Wajumbe wa Tume baadhi ya watu ambao si Wabunge au Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.

Je amendment hii ilipitishwa na wabunge kama ilivyowasilishwa na waziri au wabunge waliifanyia marekebisho na kuondoa kizuizi cha kutoteuliwa kuwa Wajumbe wa Tume baadhi ya watu ambao ni Wabunge na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar?
 
WaTanzania wa2 wa ajabu sana wanasoma na wanafikiria kwa hisia; hakuna jambo lililoongelewa kwa muda mrefu kama hili ni jambo la kusikitisha kwamba haikueleweka kwamba sheria imebadilika... VERY SAD. In fact kusema hivyo ni matusi kwa vyama vilivyopeleka hayo majina kama kweli wanasiasa walikuwa hawastahili. Then ni matusi pia kwa hao wasomi kukubali ki2 ambacho kingekuwa against sheria. Tuache uganga wa kienyeji; kudhani everyday president atakosea... Pls utilize your endowed geni


kaka soma kwa makini pst yangu elewa na pia fanya utafiti. Soma hansard soma sheria arafu ndo uje na hicho unachokisema. Pia waweza leta sheria ambayo wewe unahis ni sahihi. Visit bunges website.

unasemaje kuhusu hili la cv ya kwg?

pole na ukada unaokufumba macho. Jst liberal my friend.

Huyo hata umwambie nini, mradi tu amponde Kikwete, kwake hata jema la Kikwete ni ovu.

Ni mtu mmoja fitna wa hali ya juu, anaweza kuubadili ukweli na akaufanya uongo na uongo akaufanya ukweli. That is how dangerous he/she is.
 
EMT, hawa wenzetu kina Kasheshe wanabisha tu kwa sababu hawafikirii hata kidogo kuwa Rais anaweza kuvunja sheria! Wanaamini serikali "ikisema" na hawashuku "serikali ikifanya". Kwa kadiri ninavyofahamu hadi hivi na ushahidi wote uliopo ni kuwa sheria inakataza wabunge na wawakilishi kuwa wajumbe wa Tume! Hakuna mtu hata mmoja aliyeonesha kuwa wabunge na wawakilishi wanaruhusiwa. Wanachoogopa ni huo uwezekano kuwa ni kweli Rais anaweza kuwa amevunja sheria aliyoisaini mwenyewe!!!
 
mtunga sheria ndio..........................., nimesoma maoni yenu, ila je nini kifanyike maana naona tayari watu wameshaapishwa na kisheria wanatakiwa kuanza kazi mara 1.

well kama wameteuliwa watu wasiotakiwa kuwemo huwezi kusema "wameapishwa". Kwa mfano Rais hawezi kumteua mtu asiye na sifa ya kuwa Jaji wa Mahakama Kuu halafu mkasema "si ameshamteua"? Well, wanatakiwa kujiuzulu mara moja!
 
Back
Top Bottom