Yawezekana Rais amevunja sheria ya Mchakato wa Katiba kwa kuwaapisha kina Baregu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yawezekana Rais amevunja sheria ya Mchakato wa Katiba kwa kuwaapisha kina Baregu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 14, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 14, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Ninaamini kwa kuwaapisha baadhi ya watu kuwa� wajumbe wa Kamati ya rais ya Maoni kuhusu Katiba Mpya Rais Kikwete amevunja sheria ambayo yeye mwenyewe aliisaini. Sheria ya kusimamia mchakato huu inasema wazi kuhusu wajumbe wa Tume kuwa pamoja na mambo mengine kuwa:

  [SIZE=-1]tuangalie:

  Akimuapisha Mbunge

  [/SIZE] tume-mbunge.jpg
  [SIZE=-1]
  Hapa anamwapisha Mwakilishi (baraza la wawakilishi)

  [/SIZE] tume-mwakilishi.jpg
  [SIZE=-1]
  Hapa akimwapisha Prof. Mwesiga Baregu - Mjumbe wa Kamati Kuu ya CDM na Mkuu wa kampeni yake 2010

  [/SIZE] tume--baregu.jpg
  [SIZE=-1]
  Hapa chini anamwaipsha Dr. Sengodo Mvungi ambaye ni Mjumbe wa kamati kuu ya NCCR Mageuzi[/SIZE]

  tume-mvungi.jpg

  [SIZE=-1]My Take:

  a. Yawezekana labda natumia kipengele siyo sahihi kwa hiyo kama nakosea niko tayari kusahihishwa. Kama ni makosa basi hoja za hapa chini zipuuzwe.
  b. Kama sheria inakataza kabisa na waziwazi kuwa wabunge na wawakilishi au viongozi wa kisiasa wasiwe wajumbe wa Tume na hakuna exception ni kwanini tuwaone wajumbe hawa kuwa ni halali?
  c. Kama kweli watu hawa walipaswa kuwemo ndani ya tume hii kwanini sheria isingebadilishwa kwanza? au sasa wameshaingia ndio sheria itabadilishwa kuhalalisha?
  d. Je, kama rais ameshindwa kuzingatia sheria aliyoipigia debe yeye mwenyewe watu wengine wakivunja sheria inakuwaje? Je,yawezekana Bungeni likaulizwa swali kupata maelezo juu ya uhalali wa wajumbe hawa?
  e. Sheria inaposema asiwe kiongozi wa chama cha siasa "of any category" siyo kwamba it is too vast kiasi kwamba hata mwanachama wa kawaida tu anaweza kuhesabiwa kuwa ni kiongozi wa "category" fulani? yaani hata mshauri tu wa chama anaweza kuqualify kuwa ni kiongozi?


  HANSARDI YA BUNGE FEB 8, 2012
  [/SIZE]
   
 2. M

  Mnyama Hatari JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ebana eeeh....hii kali. Sasa tusubiri spin.
   
 3. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,765
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  kutakuwa na maon binafs kuwakilishwa kutokana na shinikizo la vyama kwa vile ndo mwakilishi wao.
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Apr 14, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji,

  Utetezi # 1:

  ..inawezekana Raisi haijui sheria kwasababu hakuisoma.

  ..lakini Raisi ana nia nzuri tu ktk uteuzi huo.

  Utetezi # 2:

  ..Raisi ni mchumi kitaaluma, siyo mwanasheria.

  ..washauri wake wamemuangusha.
   
 5. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,261
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye RED mimi mwenyewe hoi........kwahiyo angekuwa siyo mchumi basi nchi hii ingekuwa imefirisika kama Ugiriki!! maana nchi inaongozwa na mchumi na uchumi uko hoi vipi ingeongozwa na fundi mchundo.
   
 6. U

  Uswe JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  hiyo 6.5 ilikua mjadala mkubwa sana lakini ilibadilishwa kuruhusu kila mtu wakiwemo wabunge na wanasiasa
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Apr 14, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  I had that feeling kwa sababu wazo hili linanitisha; nilikuwa natafuta mabadiliko ya sheria hii yalikuwaje.. lakini bado wabunge wote bado niwajumbe wa Baraza hilo la Katiba?
   
 8. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Haukuwa na sababu ya kunukuu uzi mzima, mnatutesa tunaotumia simu jamani.
  Ukijibu tu kwa kupost kawaida kila mtu anaelewa kuwa hili ni jibu la kwenye bandiko halisi.
   
 9. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,142
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji, tunashukuru kwa observation yako. tusubiri tuone kama kuna majibu ya ujinga huo.kama majibu hayatopatikana, basi tuanze kuhitimisha si rahisi kupata katiba mpya
   
 10. m

  mjanja1 Member

  #10
  Apr 14, 2012
  Joined: May 11, 2010
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [FONT=&amp]Nimejitahidi kufanya utafiti na kupitia sheria ya mapitio ya katiba (mabadiliko) 2011 “the Constitutional Review (Amendment) Act, 2011”, sheria ya mapitio ya katiba, 2011 “ the Constitutional Review Act, 2011”, katiba ya sasa na Hansard za bunge kuhusu suala hili. [/FONT] [FONT=&amp]NIKILI pia kuwa SIKUFANIKIWA KUIONA sheria ya mapitio ya katiba (mabadiliko) 2011 “ the Constitutional Review (Amendment) Act, 2011” kama ilivyopitishwa na bunge kwani haipo katika website ya bunge HADI LEO leo hii tr. 6.4.2011 hivyo nimerely katika kumbukumbu za Hansard KUHUSIANA NA SUALA HILI.[/FONT]

  [FONT=&amp]KWA HISTORIA TU.[/FONT]
  [FONT=&amp]sheria ya mapitio ya katiba, 2011 “ the Constitutional Review Act, 2011”, (HAPO AWALI KABLA YA MABADILIKO )ilikuwa na vifungu vifuatavyo kuhusu uteuzi wa wajumbe wa kamati ya katiba:-[/FONT]
  [FONT=&amp]SEHEMU YA TATU[/FONT]
  [FONT=&amp]6.-(1) Rais, baada ya kushauriana na kukubaliana na Rais wa[/FONT]
  [FONT=&amp]Zanzibar atateua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajul11bewa[/FONT] [FONT=&amp]Tume.[/FONT]
  [FONT=&amp](2) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo cha (3),[/FONT]
  [FONT=&amp]muundo wa Tume utazingatia msingi wa kuwepo kwa uwakiUshi ulio[/FONT]
  [FONT=&amp]sawa kwa kila upande wa Jamhuri ya Muungano.[/FONT]
  [FONT=&amp](3) Katika kufanya uteuzi wa wajumbe wa Tume, Rais[/FONT]
  [FONT=&amp]atazingatia masuala yafuatayo:[/FONT] [FONT=&amp](a) uzoefu katika kufanya mapitio ya katiba na sifa za[/FONT]
  [FONT=&amp]kitaaluma za wajumbe kwenye mambo ya katiba, sheria,[/FONT] [FONT=&amp]utawala, uchumi, fedha na sayansi ya jamii;[/FONT]
  [FONT=&amp](b) jiografia na mtawanyiko wa watu katika JamtlUri ya[/FONT] [FONT=&amp]Muungano wa Tanzania;[/FONT]
  [FONT=&amp](c) umri, jinsia na uwakilishi wa makundi mbalimbali ya[/FONT] [FONT=&amp]kijamii; na[/FONT]
  [FONT=&amp](4) Bila ya kuathiri ibara ndogo ya (3), mtu hatoweza[/FONT] [FONT=&amp]kuteuliwa kama mjumbe wa Tume mpaka mtu huyo awe na uaminifu[/FONT]
  [FONT=&amp]wa hali ya juu ya tabia isiyo.tiliwa shaka na jamii.[/FONT]

  [FONT=&amp](5) Bila ya kujali kifungu kidogo cha (3), mtu hatakuwa na[/FONT]
  [FONT=&amp]sifa za kuteuliwa kuwa mjumbe wa Tume endapo mtu huyo:-[/FONT]

  [FONT=&amp](a) NI MBUNGE, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi la[/FONT]
  [FONT=&amp]Zanzibar, diwani au kiongozi wa chama cha katika ngazi .[/FONT]
  [FONT=&amp]zote;[/FONT] [FONT=&amp](b) ni mtumishi katika vyombo vya usalama;[/FONT] [FONT=&amp](c) ni mtu aliyewahi kuhukumiwa kwa kutenda kosa, au ni[/FONT] [FONT=&amp]mtuhumiwa katika shauri lililopo mahakamani linalohusu[/FONT]
  [FONT=&amp]shitaka la kukosa uaminifu au maadili; au[/FONT] [FONT=&amp](d) si raia wa Tanzania.[/FONT] [FONT=&amp]Wadau wakalalamika sana akiwemo na LISSU akapiga kelele sana sana, wakabadili hicho kifungu[/FONT] [FONT=&amp] Bungeni Lissu akasema:-[/FONT] [FONT=&amp]MUSWADA NA JEDWALI LA MAREKEBISHO LA SERIKALI[/FONT] [FONT=&amp]Mheshimiwa Spika,[/FONT] [FONT=&amp]Sasa naomba, kwa ruhusa yako, niwasilishe uchambuzi wa Muswada wenyewe pamoja na Jedwali la Marekebisho lililowasilishwa na Serikali, nikianzia na mapendekezo ya marekebisho ya vifungu mbali mbali vinavyohusiana na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.[/FONT] [FONT=&amp]TUME YA MABADILIKO YA KATIBA[/FONT] [FONT=&amp]Mheshimiwa Spika,[/FONT] [FONT=&amp]Ibara ya 2 ya Muswada inapendekeza kufanya marekebisho katika kifungu cha 6(5)(a) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kwa kufuta maneno “au kiongozi wa chama cha siasa wa ngazi yoyote.” Jedwali la Marekebisho la Serikali lililowasilishwa sambamba na Muswada linapendekeza marekebisho sio tu ya ya kifungu cha 6(5)(a), bali pia kinapendekeza kuongezwa masharti ya ziada katika kifungu cha 6 cha Sheria. Kwanza, inapendekezwa kwamba maneno “, diwani au kiongozi wa chama cha siasa katika ngazi zote” yafutwe na badala yake yabaki maneno “Mbunge na Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.”[/FONT]

  [FONT=&amp]Mheshimiwa Spika,[/FONT] [FONT=&amp]Ili kuelewa maana ya marekebisho yanayopendekezwa, ni muhimu kurejea katika kifungu cha 6(5) kinachopendekezwa kurekebishwa na Muswada huu. Kifungu hiki kinaweka masharti ya kuteuliwa kuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kuwaondolea sifa za kuteuliwa Wabunge, Wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, madiwani na viongozi wa vyama vya siasa wa ngazi zote. Kwa mapendekezo ya Muswada huu na Jedwali la Marekebisho la Serikali, watu pekee ambao sasa hawatakuwa na sifa za kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume ni Wabunge na Wawakilishi wa Zanzibar. Kwa maneno mengine, madiwani na viongozi wa vyama vya siasa wa ngazi zote watakuwa na sifa za kuteuliwa ili mradi tu wanazo sifa za kitaaluma na nyinginezo zilizotajwa katika kifungu cha 6(3) cha Sheria.[/FONT]

  [FONT=&amp]Mheshimiwa Spika,[/FONT] [FONT=&amp]Katika maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wakati wa mjadala wa kupitishwa kwa Sheria hii tarehe 15 Novemba mwaka jana, tuliliambia Bunge lako tukufu kwamba, kwa kukataza viongozi wa vyama vya siasa kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume, kifungu cha 6(5)(a) “… k(i)naondoa kwenye mchakato wa Katiba Mpya kundi kubwa la watu wenye utaalamu na uzoefu katika masuala mbali mbali ya kisiasa, kikatiba, kisheria, kiuchumi, kiutawala, kifedha na kisayansi jamii. Vile vile, viongozi wa vyama vya siasa wanawakilisha makundi makubwa ya kijamii yenye mtawanyiko wa watu na wa kijiografia katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na wanawakilisha watu wa umri na jinsia zote kama inavyopendekezwa katika Muswada Mpya.”

  Pendekezo letu kwamba Wabunge na Wawakilishi wa Zanzibar nao wawe na sifa za kuteuliwa wajumbe wa Tume halipo katika mapendekezo ya Muswada huu na Jedwali la Marekebisho la Serikali. Hata hivyo – katika kuendeleza moyo wa maridhiano na give and take – Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaridhika na kuunga mkono mapendekezo ya marekebisho ya kifungu cha 6(5)(a) ili kuwapa madiwani na viongozi wa vyama vya siasa sifa za kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume.[/FONT]
  [FONT=&amp](Wabunge wa CCM wakapiga makofi na kushangilia sana)[/FONT]

  [FONT=&amp]MABADILIKO HAYO YAKAPITISHWA YOTE.[/FONT] [FONT=&amp]

  Leo hii:-[/FONT]
  [FONT=&amp]
  TUME YA MABADILIKO YA KATIBA[/FONT]
  [FONT=&amp]
  (Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura 83,[/FONT]
  [FONT=&amp]Toleo la 2012, Vifungu 5, 6 na 7)[/FONT] [FONT=&amp]______________________________[/FONT] [FONT=&amp]
  13. Mhe. Al-Shaymaa J. KWEGYIR (Mb)[/FONT]


  [TABLE="class: cms_table_MsoNormalTable"]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"] [FONT=&amp]GENERAL[/FONT][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [FONT=&amp]Salutation[/FONT][/TD]
  [TD] [FONT=&amp]Honourable[/FONT][/TD]
  [TD="width: 42%"]
  [FONT=&amp]Member picture[/FONT][FONT=&amp]
  [​IMG][/FONT]​
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [FONT=&amp]First Name: [/FONT][/TD]
  [TD] [FONT=&amp]Al-Shaymaa[/FONT][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [FONT=&amp]Middle Name[/FONT][FONT=&amp]: [/FONT][/TD]
  [TD] [FONT=&amp]John[/FONT][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [FONT=&amp]Last Name:[/FONT][/TD]
  [TD] [FONT=&amp]Kwegyir[/FONT][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 20%"] [FONT=&amp]Member Type:[/FONT][/TD]
  [TD="width: 38%"] [FONT=&amp]Special Seat[/FONT][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [FONT=&amp]Constituent:[/FONT][/TD]
  [TD] [FONT=&amp]No Constituency[/FONT][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [FONT=&amp]Political Party:[/FONT][/TD]
  [TD] [FONT=&amp]CCM[/FONT][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [FONT=&amp]Office Location:[/FONT][/TD]
  [TD] [FONT=&amp]Box 61530, Dar Es Salaam[/FONT][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [FONT=&amp]Office Phone: [/FONT][/TD]
  [TD] [FONT=&amp]+255 773 238804/+255 713 238804[/FONT][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [FONT=&amp]Ext.: [/FONT][/TD]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [FONT=&amp]Office Fax: [/FONT][/TD]
  [TD] [FONT=&amp]-[/FONT][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [FONT=&amp]Office E-mail: [/FONT][/TD]
  [TD] [FONT=&amp]akwegyir@parliament.go.tz[/FONT][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [FONT=&amp]Member Status: [/FONT][/TD]
  [TD] [FONT=&amp]Current Member[/FONT]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [FONT=&amp]Start date:[/FONT][/TD]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [FONT=&amp]End date:[/FONT][/TD]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [FONT=&amp]Date of Birth [/FONT][/TD]
  [TD] [FONT=&amp]8 April 1960 [/FONT][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  [TABLE="class: cms_table_MsoNormalTable"]
  [TR]
  [TD="colspan: 5"] [FONT=&amp]EDUCATIONS[/FONT][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 35%"] [FONT=&amp]School Name/Location [/FONT][/TD]
  [TD="width: 27%"] [FONT=&amp]Course/Degree/Award [/FONT][/TD]
  [TD="width: 15%"]
  [FONT=&amp]Start Date[/FONT]
  [/TD]
  [TD="width: 13%"]
  [FONT=&amp]End Date[/FONT]
  [/TD]
  [TD="width: 10%"]
  [FONT=&amp]Level[/FONT]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [FONT=&amp]Agha Khan Primary School[/FONT][/TD]
  [TD]
  [FONT=&amp]Primary Education[/FONT]​
  [/TD]
  [TD]
  [FONT=&amp]1968[/FONT]​
  [/TD]
  [TD]
  [FONT=&amp]1971[/FONT]​
  [/TD]
  [TD]
  [FONT=&amp]PRIMARY[/FONT]​
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [FONT=&amp]Forodhani Primary School[/FONT][/TD]
  [TD]
  [FONT=&amp]Primary Education[/FONT]​
  [/TD]
  [TD]
  [FONT=&amp]1972[/FONT]​
  [/TD]
  [TD]
  [FONT=&amp]1974[/FONT]​
  [/TD]
  [TD]
  [FONT=&amp]PRIMARY[/FONT]​
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [FONT=&amp]Forest Hill Secondary School[/FONT][/TD]
  [TD]
  [FONT=&amp]O-Level Education[/FONT]​
  [/TD]
  [TD]
  [FONT=&amp]1975[/FONT]​
  [/TD]
  [TD]
  [FONT=&amp]1975[/FONT]​
  [/TD]
  [TD]
  [FONT=&amp]SECONDARY[/FONT]​
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [FONT=&amp]Forodhani Secondary School[/FONT][/TD]
  [TD]
  [FONT=&amp]O-Level Education[/FONT]​
  [/TD]
  [TD]
  [FONT=&amp]1976[/FONT]​
  [/TD]
  [TD]
  [FONT=&amp]1978[/FONT]​
  [/TD]
  [TD]
  [FONT=&amp]SECONDARY[/FONT]​
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [FONT=&amp]College of Diplomacy[/FONT][/TD]
  [TD]
  [FONT=&amp]Diploma (Law)[/FONT]​
  [/TD]
  [TD]
  [FONT=&amp]2006[/FONT]​
  [/TD]
  [TD]
  [FONT=&amp]-[/FONT]​
  [/TD]
  [TD]
  [FONT=&amp]DIPLOMA[/FONT]​
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [FONT=&amp]University of Dar es Salaam[/FONT][/TD]
  [TD]
  [FONT=&amp]LLB[/FONT]​
  [/TD]
  [TD]
  [FONT=&amp]2008[/FONT]​
  [/TD]
  [TD][/TD]
  [TD]
  [FONT=&amp]GRADUATE[/FONT]​
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  [TABLE="class: cms_table_MsoNormalTable"]
  [TR]
  [TD] [FONT=&amp]CERTIFICATIONS [/FONT][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  [FONT=&amp] Je hii ni sawa kweli?, hasa ukizingatia RAISI [/FONT][FONT=&amp]katika kiapo chake cha uraisi anasema:- …. “ataitunza na kuilinda katiba ya nchi”. Na Katiba inaelekeza kuwa nchi ya Tanzania itaendeshwa kwa kuzingatia matakwa ya katiba, sheria na taratibu zilizopo.[/FONT]

  [FONT=&amp]Sina ubaya wala kinyongo na Mh. Aliteuliwa namweshimu sana kama mtu makini na hodari kwa kupigania haki na maslhai ya watu wanyonje kwenye jamii lakini kuwepo kwake hapa kwa mtazamo wangu ni kinyume na sheria ambayo serikali iliilazimisha iwe hivyo kwa nguvu sana licha ya kupingwa na wadau mbalimbali.[/FONT]

  [FONT=&amp]IKIWA [/FONT][FONT=&amp]hili limefanyika kinyume cha sheria, je wasaidizi wa raisi katika masuala ya sheria wanafanya nini? Au aliwakaidi? [/FONT] [FONT=&amp]Je kwa kutokuzingatia matakwa ya sheria ya mabadiliko ya katiba kama ilivyobadilishwa,2012 KATIBA iliyopo imelindwa na kutetewa, na pia ujumbe gani unapelekwa kwa wananchi wa kawaida kuhusu utawala wa sheria?. [/FONT] [FONT=&amp]Na nini kifanyike sasa kama kunatatizo?[/FONT] [FONT=&amp]Tulitazame na kuliangalia hili kwa upana ili tudumishe demokrasia na utii wa sheria katika nchi hii.[/FONT] Sikonge likes this.

  [​IMG] Edit Post [​IMG] Reply [​IMG] Reply With Quote [​IMG]

   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kuwa Mjumbe wa Kamati kuu pekee kwenye chama hakumaanishi wewe ni kiongozi wa kisiasa.

  Ni kama vile kuwa mjumbe wa kamati ya kero za rushwa hakumaanishi kuwa wewe ni kiongozi wa mtoa au mpokea rushwa.

  Fikiri.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Apr 14, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Mjanja1, nashukuru kwa kupitia hansard hivyo; inaonekana basi kama mabadiliko yamekuwa kama yalivyo kina Baregu wanaweza kuwa sahihi kuingia kwenye tume lakini mbunge na mwakilishi hawakutakiwa kuingia siyo?
   
 13. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,482
  Likes Received: 5,557
  Trophy Points: 280
  Kwa nilivyoelewa bandiko la Mjanja1 wabunge na wawakilishi hawakutakiwa kuwemo ingawa kuruhusiwa viongozi wa siasa kushiriki inaweza kuwa mwanya uliotumika kupitisha hao wabunge na wawakilishi maana hakuna tafsiri ya hao wanasiasa wawe na sifa gani! naomba kusahihishwa mambo ya sheria haya.
   
 14. J

  Jadi JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 1,402
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  huyu Rais hakuisoma hiyo sheria, nchi hii ndio ilivyo,ni rahisi sana kuweka maandishi na ni ndoto kuyafuata,wenyewe mmeona
   
 15. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #15
  Apr 14, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,667
  Likes Received: 17,711
  Trophy Points: 280
  Kwa uelewa wangu na jinsi nilivyoisoma presentation ya Lisu ni wabunge na wawakilishi pekee ndiyo hawaruhusiwi, ila kwaupande wa kina Beregu na Mvungi, JK hajavunja sheria
   
 16. m

  mjanja1 Member

  #16
  Apr 14, 2012
  Joined: May 11, 2010
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  neno shall kisheria linamaanisha mandatory na sio optional. Kwa hivyo hata kama uwe na sifa gani nyingine... Mjumbe wa kamati ya kisiasa . kiongozi wa Walemavu au asas yoyote Provided wewe ni mbunge au mjumbe wa wawakilishi una kuwa disqualified without an option.

  kuna hili la maadili ya wajumbe. Narudia kusema sina personal interest na kwegria mb. But cv aliyoweka bungeni ni ya uongo. She has never been at any udsm ll.b class esp 2008. Kwa kusema uongo kwa umma wa tz ni kuonesha dhairi kuwa maadili yapo chini.

  arafu kama tunachakachua mwanzo kabisa kwa kupindisha kuvunja sheria tulio ipitisha kwa kulazimisha pamoja na kupingwa na umma. Tutegemee nini kwenye katiba mpya. Obvious ni kulazimisha yasiyokuwepo.

  i get a feeling kuna misapplication and embzlement of public funds katika mchakato huu kwani tayari majibu ya nini kiwepo na kisiwepo yanajulikana.speach ya jk jana ni sufficient signal for that.
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Apr 14, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Unajua ukisikiliza hotuba ya Kikwete hakuwauliza hawa wote kama wanataka kuingia kwenye hiyo Kamati wala kuwafanyia vetting ya aina yoyote; yeye katangaza tu na anashukuru hakuna aliyekataa!!
   
 18. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #18
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kwa hapo tunaziangalia sifa zinazomzuia na sio zinazomuingiza katika tume. Kwa hiyo si sahihi kwa mbunge kuwemo kwa kofia ya uanasiasa.
   
 19. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #19
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Washauri wake hufanya humshauri wakijua kuwa ana kinga ya kutoshtakiwa akitoka madarakani
   
 20. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #20
  Apr 14, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  MM, kama tumeridhika kuwa mchakato tayari umekinzana na sheria inayouunda, na anayekiuka sheria hiyo ni mh. rais wa jamuhuri ya muungano wa tz, kwa kutumia sheria zilizopo wenyenchi tunayo nafasi kisheria kuzuia hii kitu?
   
Loading...