Yawezekana kuwa na ushirika na Mungu pasipo kuwa na dini?

IsangulaKG

JF-Expert Member
Oct 14, 2010
706
386
Kama kawaida niwapo safarini napata fursa ya kujisemeza (talking to myself) kama njia ya kuzianika fikra zangu.Natambua pia kwamba zipo topics ambazo zimejengewa kingo kifikra kwamba hazipaswi "kuguswa" na kwamba yule anayezigusa hata kama anajisemeza mwenyewe basi atakuwa "anatumiwa" na upande usiokubaliana na topics hizo.Mfano hivi karibuni umezuka ukingo wa fikra kwamba yeyote anayehoji ama kujitafakarisha kuhusu mambo ya "utawala" basi anatumiwa na "upinzani" hata kama hana chama na wengine wameenda mbali kupakaza kutumiwa huko kwa mataifa ya magharibi.Vivyo hivyo, katika dini zimejengwa kuta za kifikra kwamba yeyote anayehoji au kujitakafakarisha kwa mambo kadhaa basi anatumiwa na shetani ama kama wainjilisti wanavyosema ni "wakili wa shetani" . Kuta za aina hii kifikra zimefanya wengi wetu kupokea badhi ya mambo ya kidini kama yaliyo hata kama mioyo yetu inagugumia kwa kukosa majibu.

Kabla sijaendelea kujisemeza najikumbisha kwamba natambua thamani ya ushirika wangu wa moja kwa moja na Mungu ambao umekuwepo, upo na utaendelea kuwepo hata kama dini, madhehebu na makanisa hayatakuwepo. Hii ni kwa sababu yapo matukio kadhaa ambayo sina jinsi ya kuyaelezea zaidi ya kuamini uwepo wa 'supernatural power' ambayo ni mshirika katika safari yangu ya maisha. Mifano ni mingi sana lakini kwa uchache mfano Gari iliyo mbele yangu wakati wa safari inapata ajali na abiria wengi kupoteza uhai na siyo niliyomo. Ama kuugua ugonjwa unaoua wengine wengi lakini mimi nikapona. Hapa hoja ni ushirika wangu wa moja kwa moja na Mungu na siyo dini.Ushirika ambao ungeweza kuwepo hata kama dini zisingekuwepo.

Nikirejea kwenye kujisemesha, kwangu mimi dini ni 'intermediary' ama kitu/nyezo inayosimama kati ya mwanadamu mwenye ushirika na Mungu na Mungu wake. Kwa maneno mengine, dini ni kama bakuli linalobeba chakula kinacholeta shibe ya imani kwa Mungu. Kwa muktadha huu, bado mtu anaweza kuwa na ushirika wa moja kwa moja na Mungu wake pasipo kuwa na dini kama vile ambavyo mtu anavyoweza kupata shibe paso kutumia bakuli kujipatia Chakula. Yapo makosa makubwa sana kuamini kuwa ni lazima mtu awe na dini (ukristo ama uislamu) ili kuwa na ushirika na Mungu.

Neno 'Kristo' laonekana kuwa na mzizi wa 'uamini katika ukristo' ama Yesu Kristo.Kama hii ni sahihi, tungeweza kusema ukristo umekuwepo baada ya Yesu Kristo.Lakini ukweli ni kwamba Biblia inaonyesha wanadamu walikuwa na ushirika na mawasiliano ya moja kwa moja na Mungu hata kabla hatujajua uwepo wa Kristo.Fikiria Adamu pale bustani ya Edeni, Abraham na Musa wote hawa waliweza kuwa na ushirika na kuwasiliana na Mungu moja kwa moja pasipo kuhitaji dini. In fact, Agano la Kale la Biblia sehemu kubwa haioneshi dini kama nyenzo pekee ya kuwa na ushirika na Mungu. Tena, habari za masinagogi na mahekalu (nyumba za ibada) kama kiashiria cha uwepo wa dini zimeshamiri baada ya ujio wa Yesu na tunaona kuwa yalikuwa yanatumika kwa mambo yasiyokuwa ya kiMungi hata wakati wa Yesu Kristo.Naamini sasa naweza kukiri moyoni kuwa nikiamua naweza kuwa na ushirika na Mungu hata pasipo kuwa na dini.

Kama watu wa mwanzo waliweza kuwa na ushirika na Mungu bila dini, kwa nini dunia imeaminishwa kuwa tunahitaji dini kuwa na ushirika na Mungu?

Tukiangalia historia, warumi (Imperium Rōmānum) walikuwa kati ya watu wa mwanzo kabisa kutumia dini kama nyenzo ya kutawala fikra za watu wao. Enzi za Caesar (Kaisali) na akina Augustus kwa mfano, kulizuka mavuguvugu ya vitu kama "wapagani" ama "wapinga dini" katika dola ya kirumi ya kale na waliuawa hasa kwa Upanga ama kuchomwa moto ama kutundikwa msalabani. Hali hii ya kuwauwa watu wasioendana na misingi ya Kirumi ndiyo baadae imekuja kuzua madehebu tofauti kama Lutheran, SDA na mengine mengi ya kikristo.

Wakoloni walipotaka kuitawala Africa, walikumbana na vikwazo vya mapambano ya kivita toka kwa wenyeji mfano mfalme Menelik II wa ethiopia aliyewashinda waitaliano ama Samory Touré wa Mandinka Africa Magharibi dhidi ya wafaransa. Mojawapo ya Nyenzo muhimu iliyofanikisha kuingia kwa wakoloni kirahisi ilikuwa ni Dini. Wamisionari walijazwa Afrika ili kuwapooza mioyo na kuhubiri upendo na amani wakati huo huo wazungu wakiendelea kuwatumikisha waafrika na hata kuwauza kama watumwa. Inawezekana wapo walioubiri neno kwa kuamini kuwa wanatimiza wajibu wa kweli wa kimungu na pengine wapo waliojua kuwa wanatumika kama nyenzo ya kiuchumi kwa mabepari. Ndiyo maana baada ya manepari kufanikisha malengo yao ya kunyonya Afrika na baada ya kelele nyingi dhidi ya vitu kama utumwa, wachumaji wakaondoka watuachia dini na madhehebu.

Kumekuwa na tafiti nyingi sana na machapisho mengi ya jinsi ambavyo dini inachangia kulifukarisha bara la Africa-kama ilivyotumika enzi za kikoloni kama nyenzo ya kuwanyonya waafrika rasilimali zao- sasa inatumiwa na waafrika wenyewe kuwanyonya na kkuwafukarisha wenzao. Wanaofuata dini hawana makosa zaidi ya kuanguka katika mtego wa wahubiri wakoloni. Si nadra kuona wahubiri wengi (ukitoa wachache)wakijilimbikizia mali (kama wakoloni) kwa kutumia sadaka na zaka za wanyonge.Pengine ndiyo maana Kagame ameamua kufuta zaidi ya makanisa 600 kwa kuliona hili. Dini pia yaweza kutumiwa kujenga fikra za uwoga dhidi ya dola tawala kwa kiasi fulani (si nadra kuona viongozi wa dini wachache wakiwataka wafuasi wao waziheshimu mamlaka). Kwa ufupi, dini kwa kiasi kikubwa kwa sasa inatumika kutimiza malengo yaleyale yaliyoifanya iletwe na wakoloni. Bahati mbaya kwa sasa inatumiwa na wakoloni weusi kuwanyonya weusi wenzao.

Ni kwa sababu hii nafikia hitimisho kuwa kumbe naweza kuwa na ushirika wa moja kwa na Mungu wangu bila kuwa na dini nikiamua.Kwa sababu hata kama dini zitapotea, ushirika wangu na Mungu hauwezi kuteteleka.

Nimefika safari yangu.

IsangulaKG







Facebook:
 
Msingi wa hoja yako ina makosa mengi sana. Kwanza unachanganya habari za Rumi na Kanisa Katoliki. Unasema Rumi kutesa waamini (ukimaanisha Katoliki) ndio iliyoleta madhehebu (kosa jingine). Unakijua kitabu cha ufunuo? Unajua habari zake zilihusu dola ipi? Dola hiyo ilikuwa na uhusiano gani na Kanisa? Unajua hayo madhehebu uliyotaja yameanza majuzi tu miaka ya 1500s? Hapo Rumi itokee wapi? Alafu labda turudi kwenye swala la msingi je dini ni nini? Hata Yesu alifata misingi yote ya dini ya kiyahudi wakati akitimiliza agano jipya. Mitume waliishi kishirika baada ya Yesu kuondoka. Unawezaje kumjua Mungu bila kuwa na sehemu utayofundishwa/ hubiriwa? Sasa hapo unapoenda kumjua Mungu na kuabudu ni nini? Si dini? Labda uelewi maana ya dini. Siku hizi kuna wahubiri wanaotumia msemo wa sihubiri habari za dini bali Yesu Kristo ....ni sawa lakini ina mantiki kwa sehemu na haindoi ukweli wa Yesu kusimika dini ya Kikristo na kuteua kiongozi wake wa kwanza ambaye ni Petro. Kitendo cha Petro kuteuliwa kuwa askofu wa kwanza kwa Kanisa ni kielelezo tosha kuwa Yesu alisimika visible church yenye utawala. Utaona hata mitume walipiga kura kuchagua mtu wa kuchukua nafasi ya Yuda aliyejinyonga ....hii pia ni dhahiri ni utawala na msingi wa Ukristo. Hii dhana ya mahusiano binafsi na Mungu haina maana kuvunja mahusiano na Kanisa( dini kama mnavyoita siku hizi). Bila hiyo dini/ Kanisa ungekuwa hujabatizwa na kumjua Kristo.
 
Ukisoma kitabu cha mwanzo utaona Mungu alimuumba Adamu na kumuweka duniani akatawale. kusudio la Mungu kwa mwanadamu ni kuitawala dunia. Adamu alivyopoteza mamlaka hayo ya kutawala kwa shetani ndipo alipopoteza hata ile direct fellowship na Mungu. Adamu hakuwa anaomba/ sali sababu alikuwa na mahusiano ya moja kwa moja na Mungu. Mfumo wetu wa mahusiano na Mungu ulibadilika kuanzia hapo na Adamu kufukuzwa Edeni. Ndipo mwanadamu ikatubidi tuanze ushirika mpya na Mungu ili tupate msaada wake. Mungu alianza kuweka taratibu/ sheria ili kumtii/ kupata ushirika nae. Uwepo wa sheria hizo kuanzia kwa Adamu hadi nyakati za akina Musa na kupewa amri kumi ilifanya kuwepo na utaratibu wa kumuabudu Mungu kwa jamii za wayahudi. uwepo wa ushirika wa watu wanaomuamini Mungu mmoja tayari ni dini. Kwanini dini ionekane haifai sasa wakati bila dini huo Ukristo tusingeujua? Imagine wamissionari walioleta dini wasingefika huku unafikiri ungekuwa na hiyo jeuri ya kutaka ushirika wa Mungu nje ya dini? Tumepata nuru kupitia dini na huwezi kujifungia chumbani kwako na kujifanya una ushirika na Mungu huku ushirikiani na wenzako katika kumwabudu na kumtumikia. Mkishaungana watu kadhaa mnaomwamini Mungu kwa lengo la kumwabudu tayari ndio dini yenyewe. Usifikiri kile ki ministry kule uswahilini kwavile kimeanza miaka 20 iliyopita si dini! Kama ingeanza miaka 1500 iliyopita ingesambaa dunia nzima na leo mngeiweka ni sehemu ya dini.
 
Back
Top Bottom