Gembe
JF-Expert Member
- Sep 25, 2007
- 2,483
- 164
Ndugu wajumbe,
Kwa takribani wiki mbili nimekuwa nikipitia viatbu vya sheria kuona uhallai wa kubadilishwa kwa kesi ya braza ditto kutoka kuua mpaka kuua bila kukusudia,Je ni sheria gani ilitumika?kwa utafiti wangu kwanza nilianza na katiba ya nchi..Ibara ya 45 ambayo inazungumzia uwezo wa kutoa msamaha.

45
.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika ibara hii, Rais anaweza
kutenda lolote kati ya mambo yafuatayo:-
(a) kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na hatia mbele ya mahakama kwa kosa
lolote, na aweza kutoa msamaha huo ama bila ya masharti au kwa masharti, kwa mujibu
wa sheria;
(b) kumwachilia kabisa au kwa muda maalum mtu yeyote aliyehukumuwa kuadhibiwa
kwa ajili ya kosa lolote ili mtu huyo asitimize kabisa adhabu hiyo au asitimize adhabu
hiyo wakati wa muda huo maalum;
(c) kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote iwe adhabu
tahafifu;
(d) kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa ajili ya
kosa lolote au kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu ya kutoza, au kuhozi (au
kuchukua) kitu cha mtu mwenye hatia ambacho vinginevyo kingechukuliwa na Serikali
ya Jamhuri ya Muungano.
ukiangalia kipengele hicho hapo,unaona kabisa Mheshimiwa Rais anapewa mamlaka ya kubadilisha kosa lolote.
nimetoa Hoja,naomba tuijadili hoja hii na nafikiri hii ni moja ya mapungufu ya katiba yetu,na nafikiri ndio maana ni vigumu hata mafisadi wa EPa kutajwa kwa majina na kushtakiwa,na hivi karibuni broza D atapewa madaraka ya kwuakilisha nchi.