Yawezekana huu ukawa ndio mwisho wa nguvu na ushawishi wa CCM Kanda ya Ziwa. Chama gani mbadala kina mikakati kutumia fursa hii?

wakuu CCM ikiongozwa vizuri ni chama kizuri ikilinganishwa na vyama vingine. alipokuwa anaipeleka Magufuli CCM ilikuwa ni kama kikundi cha mafia na sio chama ha siasa. Mimi nimerudi CCM baada ya Magufuli kufa
 
Baada ya kufariki kwa Rais Magufuli sioni ni kwa jinsi gani wakazi wa Kanda hiyo wataendelea kukiunga mkono hiki chama hasa kwa sababu kuu zipatazo tatu kama ifuatavyo.

Mosi: Uungwaji mkono kwa CCM katika Kanda ya Ziwa haukujengwa katika hoja bali ulijengwa katika ushabiki ukanda na ukabila. Ilifika mahali mtu alijisikia fahari kuwa Msukuma ama mtu mwenye asili ya Kanda ya Ziwa. Utakuta zinaalikwa ngoma toka usukumani kwenda kutumbuiza mkoani Dar ili tu kukonga moyo wa Rais. Zaidi ya hayo kisukuma kiligeuka kuwa lugha ya kawaida sana kunako majukwaa ya kisiasa na kiserikali.

Pili: Katika makabila mengi ya kifugaji ambayo ndiyo mengi kwa Tanzania ikiwemo Kanda ya iwa, hayakubaliani sana na jinsia ya kike hasa kunapohusika kuongoza. Wao humchukulia mwanamke kama kiumbe wa dalaja la pili.

Tatu: Miradi mingi iliyoelekezwa huko Kanda ya Ziwa siku za marehemu ina uwezekano mkubwa wa kutelekezwa au kutekelezwa kwa kiwango kidogo sana, hii nayo itaongeza chuki kwa watu wa Kanda ya Ziwa kuona ni kana kwamba CCM imesaliti maono ya shujaa wao.

Endapo uchaguzi ungeitishwa sasa sioni ni jinsi gani CCM ingeepuka kura za hasira toka kanda hii
Ndugu Mtoa Mada Hapo Juu
Kwanza, niseme napenda kujadili siasa. Pili, nisema nilikuwa si mshabiki wa CCM kabla ya Magufuli, kwa sababu ilikuwa imewasaliti wananchi. Nne, niseme niliikubali agenda ya CHADEMA hasa wakati Dr. Slaa alikuwa mgombea, lakini alipokuja mkuu wa matusi, niliachana na hisia nzuri kwa CHADEMA.

Bila kuwapotezea muda ngoja nijikite kwenye agenda ya upinzani, ambayo naona sasa hivi iko juu ambayo kama ikiendelea hivyo, CCM watajikuta wanapoteza dira pamoja na uwezekano wa kushinda kinyang'anyriro cha kura 2025. Kama inavyoonekana sasa hivi kila kitu mtandaoni ni kumponda marehemu Magufuli na utawala wake. Hii kazi inafanywa na upinzani kimkakati.

Katika huu mkakati inatakiwa iaminishwe kuwa Magufuli ndiyo adui mkuu wa TZ. Utaona sasa hivi hata wale waaminifu wa Magufuli kama vile Ndugai wanajikuta wakimsaliti martehemu bila kujuwa Viongozi wakuu wasipoangalia ni kuacha kuikamilisha miradi mikubwa ya serkali kwa visingizio vya ajabu. Wakati haya yote yanafanyika CCM imenyamaza na mitandao imejaa agenda za kuaminishwa kuwa Magufuli aliua uchumi wa TZ huku kila mtu anajuwa aliupandisha uchumi wetu daraja.

Hayo yote yakiendelea kuna wakati itafika serkali ikakata tamaa na kushindwa kuitekeleza miradi mikubwa ya serkali ambayo ilikuwa ndiyo ahadi ya CCM kwa wananchi. Wakati sisi tumekazana kumdhalalisha Magufuli huku mitandaoni, wananchi hawako na sisi kujuwa ni nini kinachoendelea. Kwa wananchi, mkombozi wao alikuwa mtu mmoja tu. Na mtu huyo ni Magufuli. Haya mengine tunbayojadili humu wala hayamgusi au kumfikia mwananchi wa Mfaranyaki au Majimoto. Barabara zikiharibika bila kutengenezwa wananchi wanajuwa Magufuli angekuwa hai, mambo yasingkekwa hivyo.

Hapo ndiyo unakuja upinzani. Wakati mmetupa Magufuli kwa kurubuniwa na upinzani, ILANI KUU ya upinzani katika uchaguzi 2025 itakuwa TUCHAGUENI UPINZANI TUENDELEZE MIRADI YA MAGUFULI. Hii ilani inaweza kuisambaratisha CCM kwa sababu wamekuwa wajinga kukubali kuendeshwa na upinzani kwa heap politics zinazoendani na kumkebehi Magufuli. Tayari watu kama Ndugai, ambao hawaoni mbali wameanza kucheza ngoma ya na upinzani. Ninyi ingieni mkenge, 2025 mtaona jinsi upinzani utakavyomtumia Magufuli kuparta kura. Haya ya mitandaoni ni kuwageuza waganga njaa wa CCM kuanza kutafuta pa kusimama. Ili kufanikiwa wanaonyesha kuwa mama SSH anaachana na sera za Magu, na wao kama vichaa wanaanza kubweteka eti Magu alidanganywa. Sasa kama alidanganywa na wewe ni spika wa bunge mwenye uwezo wa kuonana na raisi mbona hukumtonya?
CCM mkkingia mkenge kwa hili, mjue upinzani utatumia umaarufu wa Magufuli huko vijijni kupata kura. Wananchi wakiwauliza kwa nini mliwaacha barabarani hamtakuwa na la kujibu. Mnakumbuka ilikuwa kidogo tu, Dr. Slaa achukue nchi, na hii ni baada ya uwozo wa awamu ya nne. nani hajui magumu yaliyokuwepo. Nani alikuwa hajui nchi ilikuwa na raisi wa heshima na siyo executive. Nani hajui jinsi wauza madawa walivyokuwa wanatamba! Nani hajui kuwa tatizo la kutatuliwa kwa nusu saa likuwa linachukuwa miaka. Kwamfano ukiomba passport na uko tayari kutumia pesa unaipata ndani ya masaa. Lakini kama huna pesa inaweza kuchukuwa miezi. CCM agalieni mnachezewa kisaikolojia, mkiingia tu hamtatoka.
 
Yaani mpaka karne hii ya 21 bado tunaongelea habari ya ukanda!! Kumbe magufuli alichaguliwa kwa sababu anatokea kanda ya ziwa! Na siyo kwa sababu alikidhi vigezo sahihi!
Welldone umemjibu vizuri mno mtoa hoja ambaye amejipatia u stupidity!
 
wakuu CCM ikiongozwa vizuri ni chama kizuri ikilinganishwa na vyama vingine. alipokuwa anaipeleka Magufuli CCM ilikuwa ni kama kikundi cha mafia na sio chama ha siasa. Mimi nimerudi CCM baada ya Magufuli kufa
Wewe siyo mwana CCM. Wewe ni mwana CHADEMA.
 
Baada ya kufariki kwa Rais Magufuli sioni ni kwa jinsi gani wakazi wa Kanda hiyo wataendelea kukiunga mkono hiki chama hasa kwa sababu kuu zipatazo tatu kama ifuatavyo.

Mosi: Uungwaji mkono kwa CCM katika Kanda ya Ziwa haukujengwa katika hoja bali ulijengwa katika ushabiki ukanda na ukabila. Ilifika mahali mtu alijisikia fahari kuwa Msukuma ama mtu mwenye asili ya Kanda ya Ziwa. Utakuta zinaalikwa ngoma toka usukumani kwenda kutumbuiza mkoani Dar ili tu kukonga moyo wa Rais. Zaidi ya hayo kisukuma kiligeuka kuwa lugha ya kawaida sana kunako majukwaa ya kisiasa na kiserikali.

Pili: Katika makabila mengi ya kifugaji ambayo ndiyo mengi kwa Tanzania ikiwemo Kanda ya iwa, hayakubaliani sana na jinsia ya kike hasa kunapohusika kuongoza. Wao humchukulia mwanamke kama kiumbe wa dalaja la pili.

Tatu: Miradi mingi iliyoelekezwa huko Kanda ya Ziwa siku za marehemu ina uwezekano mkubwa wa kutelekezwa au kutekelezwa kwa kiwango kidogo sana, hii nayo itaongeza chuki kwa watu wa Kanda ya Ziwa kuona ni kana kwamba CCM imesaliti maono ya shujaa wao.

Endapo uchaguzi ungeitishwa sasa sioni ni jinsi gani CCM ingeepuka kura za hasira toka kanda hii
Ni mapema mnoo kusema lolote kwa sasa, ila unaweza kuwa na ukweli kwa hilo.
 
Back
Top Bottom