Yawezekana CHADEMA wanakosea lakini CCM wanakosea zaidi

Nzelu za bwino

JF-Expert Member
Jan 12, 2020
376
450
Salaam wanajamvi,

Hivi karibuni kumetokea tukio la wabunge wa CHADEMA kujiweka karantini kwa maelezo kuwa wanahofia kuambukizwa Corona. Wametoka bungeni kwa hiari yao wala hawajafukuzwa.

Kwa mujibu wa spika Mh. Job Ndugai alipoulizwa ju kitendo hicho alisema hawajafunja sheria na kanuni yoyote. Pamoja na kutovunja kanuni yoyote wapo watu wanaosema Chadema wamekosea kutohudhuria bunge muhimu na la mwisho hivyo kuwakosesha wananchi uwakilishi bungeni.

Pamoja na hayo, CCM wanakosea zaidi pale wanapowazungumzia CHADEMA muda wote ndani na nje ya Bunge, maana kwa jinsi wanavyoongelewa nikama mna watangaza (promote) zaidi kuliko kuwananga njia nzuri ilikuwa kutowazungumzia kabisa nakujikita kwenye mambo ya msingi bungeni. Kwa hili nikuwakweza sana CHADEMA maana watu wanajiuliza kwa nini wanawalazimisha sana?

Na kwanini inatumika nguvu kubwa kiasi hili? Ushauri Wangu kwa bunge achaneni kabisa na hao Chadema chapeni kazi iliyowapeleka bungeni maana wananchi wanaona ikiwezekana hili bunge la mwisho bila Chadema lingerushwa live.

Nawasilisha.
 
Chadema ni Sacos ya familia

Kuna Chadema sebuleni na Chadema chumbani

Sacos Lengo ni faida, Mbowe ametengeneza faida kubwa kwenye mali ya familia
 
Pamoja na hayo wasiongelewe sana maana wanapewa ujiko bure wabila kulipia.
 
Salaam wanajamvi,

Hivi karibuni kumetokea tukio la wabunge wa CHADEMA kujiweka karantini kwa maelezo kuwa wanahofia kuambukizwa Corona. Wametoka bungeni kwa hiari yao wala hawajafukuzwa.

Kwa mujibu wa spika Mh. Job Ndugai alipoulizwa ju kitendo hicho alisema hawajafunja sheria na kanuni yoyote. Pamoja na kutovunja kanuni yoyote wapo watu wanaosema Chadema wamekosea kutohudhuria bunge muhimu na la mwisho hivyo kuwakosesha wananchi uwakilishi bungeni.

Pamoja na hayo, CCM wanakosea zaidi pale wanapowazungumzia CHADEMA muda wote ndani na nje ya Bunge, maana kwa jinsi wanavyoongelewa nikama mna watangaza (promote) zaidi kuliko kuwananga njia nzuri ilikuwa kutowazungumzia kabisa nakujikita kwenye mambo ya msingi bungeni. Kwa hili nikuwakweza sana CHADEMA maana watu wanajiuliza kwa nini wanawalazimisha sana?

Na kwanini inatumika nguvu kubwa kiasi hili? Ushauri Wangu kwa bunge achaneni kabisa na hao Chadema chapeni kazi iliyowapeleka bungeni maana wananchi wanaona ikiwezekana hili bunge la mwisho bila Chadema lingerushwa live.

Nawasilisha.
Usalama wa wabunge ni muhimu zaidi. Uingereza wanaendesha bunge lao kidigitali sasa kwasababu zilezile za usalama wa wabunge. Hivyo Chadema wamefanya sawa kabisa na ccm wamekosea kabisa.
 
Back
Top Bottom