YAWEZA KUWA KOSA KWA KUKUTWA NA MBEGU YA BANGI?

Lipijema

JF-Expert Member
Mar 8, 2015
809
1,193
Nawasalimu, binafsi sijawahi kutumia hiyo kitu tangu nizaliwe na wala sina matarajio ya kutumia hiyo kitu. Hizo mbegu huwa ninasafirisha kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa ajili ya matumizi ya kuchanganya na sumu ya kuulia panya, kwa sababu nilielekezwa ya kwamba panya huwa wanakula sana hizo mbegu na hivyo huwa ni vyepesi kuwamaliza na ni kweli nimeona mafanikio mazuri sana, sasa kwa bahati mbaya ikitokea nimekamatwa na hizi mbegu aidha kwenye usafiri au nyumbani kwangu yaweza kuwa so!?
 
Watakukamataje kwani unaziweka machoni au.
Nchi hii hakuna kosa ukielewana na wakubwa wa eneo ulilopo iwe polisi,DC n.k.
 
Back
Top Bottom