Yatokanayo na wizi wa computer za DPP; Mtiririko wa matukio

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,783
Kwanza kuna matukio ya kupongeza... Lakini yapo pia yaliyokosa mashiko na ya mwisho kabisa yaliyoacha maswali mengi kuliko majibu....

Naomba kuongea uhalisia
Kwanza kabisa lazima tukubaliane kuwa kwa nchi ilipokuwa imefikia wakati ule tulihitaji complete overhaul.... Sio siri hiki kilio kilisikika kwa sauti na asilimia ya juu mno... Leo hatutajadili mapungufu yake... Sitajadili pia mahakama ya mafisadi kwakuwa ilikufa kabla ya kuanza kazi kusudiwa.. Tarajiwa....

Lakini bado kukawa na uhitaji wa kuadabisha watu walionekana wapigaji sana... Hawa wakapewa jina la wahujumu uchumi... Na hapa ikatumika sheria ya uhujumu uchumi ili kusiwe na dhamana... Kuna mapungufu kwenye hili lakini leo sio sehemu yake.... Hata sheria yenyewe ya uhujumu uchumi iliyoasisiwa na Marehemu Sokoine PM by then ilikuwa na mapungufu mengi ndio maana watuhumiwa wengi waliishia kuachiliwa huru baada ya muda... Mshana senior Rip loving Dad alikuwa mhanga

Turejee kwetu sasa.. Kama ni overhaul ilifanyika kweli kweli... Japo makengeza na makunyanzi yapo lakini kuna uthubutu umeonekana. Sasa kukamata lilikuwa jambo la kwanza, kushtaki lilikuwa jambo la pili... Ugumu ukaja kwenye kuthibitisha mahakamani na kutia hatiani kulingana na ithibati na ushahidi usioacha shaka... Mambo yalikwamia kwenye ngwe hii... Na hili ni kwasababu ya aina ya mashtaka... UHUJUMU UCHUMI....

Baada ya kupiga hesabu uchaguzi unakaribia na watuhumiwa bado wako mahabusu huku kukiwa hakuna ushahidi yakinifu.. Ndio ukabuniwa mkakati wa kuomba msamaha kwa masharti ya kurudisha KIASI cha pesa kwenye ofisi ya DPP kisha msamaha huo usajiliwe mahakamani
Huko kulikuwa na upinzani wa kisheria lakini mambo yakasukumwa hivyo hivyo na hatimaye washtakiwa kupitia wanasheria wao wakaanza kurudisha KIASI cha pesa walizokubaliana... Hapa napo ikatokea fursa ya kupiga... KIASI kilichotolewa na watuhumiwa si KIASI kilichowakilishwa kunako husika......

Ni katikati ya hicho kizungumkuti ndio wananchi wakatangaziwa kuwa watuhumiwa walioandika barua za kuomba msamaha walikuwa wameshafika Mia NNE na ushee... Sasa ili kudhibiti upigaji ikafunguliwa account maalum ya hilo jambo
Hii account signatories hawakuwekwa wazi na KIASI kilichopatikana pia hakikutangazwa... Yaani kukawa hakuna updates... Na hata benki pia nadhani haijulikani kwa wananchi... Na mdhibiti wa account pia... Mambo yakaishia hapo

Ghafla tukiwa tumeshachanganywa sana mara tukaletewa mwarabu wa million saba kwa saa.. Huyu ni mmojawapo aliyekaa rumande kwa miaka mitatu na ushee... Tukaambiwa amekubali yaishe... Hivyo ukaandaliwa utaratibu na makamera....

Sijui zilitumika taratibu gani za kibenki kutoa mahela yote yale kwa haraka na mara moja lakini nina hakika taratibu nyingi zilivunjwa... Cha kushangaza na kujiuliza ni hiki... Kama kulikuwa na account maalum kwa nini kusingefanyika tu bank transfer!? Njia ambayo ni rahisi na salama zaidi? Kwa nini ukatumika utaratibu ule? Zilibebwaje zile hela? Na gari gani? Kutoka wapi mpaka wapi?

Inaendelea....
Kama sikosei ishu ya mwarabu ilitokea kati ya Jumatano na Alhamini... Ikawa ndio habari kubwa mitaani.... Lakini kumbe kulikuwa kuna kitu kinatengenezwa... Kuiba computer zote kwenye ofisi za DPP

Kama tukiweza kuupa jina huu uhalifu /wizi tunaweza kuuita kwa kimombo high profile crime au first grade crime... Kwa vyovyote waliofanya hilo jambo sio watu wa kawaida wala watu wa chini hao ni THE PROFESSIONALS...
Maswali 10 yasiyo na majibu
1. Ni kina nao watu
2. Kiongozi wao ni nani
3. Lengo lao hasa ninini
4. Mipango ya kufanikisha hili jambo waliipangia wapi na lini
5. Wako wangapi
6. Wamefadhiliwa na nani
7. Mhandisi wa mchoro ni nani
8. Nani kawapa mchoro na setup ya ofisi ya DPP
9. Nani kawapa siri za computer kwenye ofisi hiyo nyeti
10. Mpaka sasa wameshafahamu nini

Jumapili nzima ina cha kusimulia.. Kuanzia asubuhi mchana jioni na usiku wa kuamkia Jumatatu
Ofisi ya DPP ina camera za ulinzi... Je hizi ziliondoshwa lini!? Au nani alizi freeze au kuzi disable?
Ofisi ya DPP ina walinzi je walikuwa wapi?
Kwa vyovyote wizi ulifanyika Jumapili usiku kuamkia Jumatatu je ni nani wa kwanza kugundua? Naamini aliripoti kwa wahusika na polisi pia na eneo lote likadhibitiwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi..

Team iliyofanya hii kazi ni kubwa na yenye wahusika wa fani zote... Je wametumiwa na watuhumiwa wa uhujumu uchumi au hii ni inside job? Kama ni watuhumiwa kuna kaunafuu kidogo lakini kama ni inside job hii ni zaidi ya hatari.....

Stay tuned......
 
20191019_170303.jpg

Umeambiwa vimeibiwa vipande vya Computer sio Computer zenyewe, Bro mshana naomba unilipie ada nikasome maana nilidhani nimesoma kumbe bado! Tanzania yangu mbona wanipa pressure!!!
 
View attachment 1238382
Umeambiwa vimeibiwa vipande vya Computer sio Computer zenyewe, Bro mshana naomba unilipie ada nikasome maana nilidhani nimesoma kumbe bado! Tanzania yangu mbona wanipa pressure!!!
Hili ni neno la awali na ni sahihi... Japo hakutakiwa kutoa conclusion haraka... Ni assurance nzuri lakini naogopa asije kuwa outsmarted na kubadili kauli... Kama kuna mtifuano wa ndani kwa ndani lazima tutashuhudia mengi... Home boi kibarua shakani
 
Angalau Leo nimebaini kwanini Mshana ana chuki na serikali, kumbe Mzee wake alikumbwa na Upepo wa Kisurisuri wa Hayati Sokoine kwenye vita dhidi ya wahujumu uchumi???. Pole sana kaka, Piga moyo konde. Unga mkono juhudi za serikali
 
Nimeandika marefu nikafuta...
Kifupi ni kwamba wizi huo ni impossible mission...la sivyo tungekuwa nae mtaani tayari ....najua anajua ila anataka tujue zaidi kuwa mwizi ni yeye.
Lowasa na Rostam ndo wameleta haya ...
 
Hili ni neno la awali na ni sahihi... Japo hakutakiwa kutoa conclusion haraka... Ni assurance nzuri lakini naogopa asije kuwa outsmarted na kubadili kauli... Kama kuna mtifuano wa ndani kwa ndani lazima tutashuhudia mengi... Home boi kibarua shakani
😂😂😂😂😂🤣
 
Back
Top Bottom