Yasemwayo na hali hali halisi: uchumi awamu za Utawala Tanzania

Mtu Mzima

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
394
124
Mengi yanasemwa na yanaendelea kusemwa kuhusu hali ya uchumi kabla na wakati wa utawala wa awamu ya tano. Hasa kuhusu uvurugaji wa uchumi na mengine kedekede.

Kabla sijatoa maoni kuhusu kampeni hasi inayoendelea hivi sasa hebu tupitie kumbukumbu na takwimu tangu uhuru kisha ndio turudi kwenye mjadala tukiwa tunaongozwa na uhalisia na sio hisia.

1. Utawala wa awamu ya kwanza (1964-1985).

  • Hii ni awamu ambayo kwa kiasi kikubwa uchumi wake ulikuwa unategemea zaidi kilimo (agrarian economy)
  • Pato la Taifa lilikuwa wastani wa Shillingi bilioni 32.7 kwa mwaka
  • Ukuaji wa uchumi (ukuaji wa Pato la Taifa) ulikuwa wastani wa asilimia 3.1 kwa mwaka
  • Mfumuko wa bei ulikuwa kwa wastani wa asilimia 18.6 kwa mwaka
  • Wastani wa kipato cha mtu kwa dola za Marekani ulikuwa USD 190.3 kwa mwaka sawa na TShs. 1,815
  • Kilimo ilitoa mchango wa asilimia 25.2% kwenye uchumi wa nchi ikifuatiwa na uchukuzi na mawasiliano (22.5%), viwanda (18.8%) na sekta ya fedha (13.5%
2. Utawala wa awamu ya pili (1985-1995)

Hii ni awamu ambayo nchi ilikuwa kwenye kipindi cha mpito kuingia soko huria, ni kipindi ambacho watanzania wengi walikuwa na fedha mifukoni. Hiki ni kipindi ambacho ilikuwa ni kama kutaka kuvuka mto kisha unapima kwanza kina cha maji. Ni awamu ambayo iliandaa mazingira ya kazi kwa awamu nyingine zilizofuata. Hata hivyo pamoja na changamoto hizo, mafanikio yalionekana kwa uchumi kuendelea kukua kwa kasi inayoridhisha
  • Pato la Taifa lilikuwa wastani wa shilingi trilioni 1.2 kwa mwaka
  • Ukuaji wa uchumi ulikuwa wastani wa asilimia 3.0 kwa mwaka
  • Mfumuko wa bei ulikuwa kwa wastani wa asilimia 29.7 kwa mwaka
  • Wastani wa kipato cha mtu kwa dola za Marekani ulikuwa USD 205.8 kwa mwaka sawa na TShs. 46,722
  • Mchano wa Sekta ya kilimo uliongezeka na kufikia wastani wa asilimia 62.3% . Michango ya sekta nyingine: Fedha (22.1%) na biashara (13.5%)
3. Utawala wa awamu ya tatu (1955-2005)
Ni kipindi ambacho sekta binafsi ilipewa kipaumbele na viwanda na mashirika mengi ya umma yalibinafsishwa.
  • Pato la Taifa lilikuwa wastani wa shilingi trilioni 9.5 kwa mwaka
  • Ukuaji wa uchumi ulikuwa wastani wa asilimia 5.7 kwa mwaka
  • Mfumuko wa bei ulikuwa kwa wastani wa asilimia 8.8 kwa mwaka
  • Wastani wa kipato cha mtu kwa dola za Marekani ulikuwa USD 311.2 kwa mwaka sawa na Tsh 277,179
  • Kilimo kiliendelea kuongoza katika uchangiaji wa pato la taifa (34.2%). Sekta nyingine: Biashara (17.6%), Viwanda (10.4%), Fedha na Bima (10.3%)
4. Utawala wa awamu ya nne (2005-2015)
  • Pato la Taifa lilikuwa wastani wa shilingi trilioni 52.9 kwa mwaka
  • Ukuaji wa uchumi ulikuwa wastani wa asilimia 6.3 kwa mwaka
  • Mfumuko wa bei ulikuwa kwa wastani wa asilimia 9.2 kwa mwaka
  • Wastani wa kipato cha mtu kwa dola za Marekani ulikuwa USD 622 kwa mwaka sawa na Tsh 979,513
  • Sekta ya Biashara ilichangia zaidi uchumi kwa asilimia 15.7%. Sekta nyingine: Kilimo (12.7%), Ujenzi (12.3%), na viwanda (10.1%)
5. Utawala wa awamu ya tano (2015-2020)

Ni awamu ambayo imedumu kwa kipindi cha miaka mitano tu.

Pia ni awamu ambayo ilijikita zaidi kuboresha miundombinu wezeshi pamoja na uwekezaji wa viwanda.

Ni awamu ambayo imebadilisha sheria na sera ili kuwamilikisha watanzania rasilimali za asili.

Ni awamu ambayo pia ilikumbwa na changamoto za ugonjwa wa korona (uviko 19) mwishoni mwa 2019 hadi 2020 na kutatiza ukuaji wa uchumi.
  • Pato la Taifa (mwaka 2016-2019) lilikuwa kwa wastani wa shilingi trilioni 124.0 kwa mwaka
  • Ukuaji wa uchumi ulikuwa wastani wa asilimia 6.9 kwa mwaka
  • Mfumuko wa bei ulikuwa kwa wastani wa asilimia 4.3 kwa mwaka
  • Wastani wa kipato cha mtu kwa dola za kimarekani ulikuwa USD 1,063.3 kwa mwaka sawa na TShs. 2,386,826
  • Sekta ya Ujenzi iliongoza katika uchangiaji wa uchumi wastani wa asilimia 25.6%. Sekta nyingine: Kilimo (19.4%), Viwanda (9.4%), Mawasiliano na uchukuzi (8.8%).
Chanzo cha takwimu ni Taasisi ya Takwimu ya Taifa na Benki ya Dunia. Kwa taarifa zaidi soma kiambatanisho

MAONI YANGU


Kila awamu ya uongozi ilikuwa na changamoto tofauti na mbinu tofauti lakini zote zililenga kukuza uchumi na kuondoa maadui watatu wa taifa: ujinga,umaskini na maradhi. Jambo la kujifunza: Kila awamu ilijenga msingi kwa awamu nyingine hivyo kupelekea ukuaji wa uchumi awamu hadi awamu na kufanikiwa kuingia uchumi wa kati (lower middle income country).

Kwa mlengo (trend) hii, na iwapo nchi haitaacha misingi yake tutarajie makubwa zaidi siku zijazo.

Si kila MRUZI UNAOPIGWA UNA NIA NJEMA NA TAIFA.


Turudi kwenye swali la msingi: Je yasemwayo kuhusu utawala wa awamu ya tano hasa kuhusu kuvuruga uchumi yana ukweli?.


Akili za kuambiwa changanya na zako....

 

Attachments

  • Taarifa_Fupi_ya_Kitakwimu_Kuhusu_Ukuaji_wa_Uchumi-2020.pdf
    1.2 MB · Views: 3
Back
Top Bottom