Yapo mengi sana ambayo Kikwete ananiudhi lakini kwa hili la.... najisikia hata kukosa nguvu

Dumelambegu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,052
257
Ndugu zangu,

Nimemsikia Kikwete akiwaambia mawaziri kwenye semina elekezi Dodoma kwamba uchaguzi unapoisha unaashiria mwanzo wa uchaguzi unaofuata. Hivi nchi hii itakuja iendelee lini jamani kama mawazo ya kiongozi wetu yanajielekeza kwenye uchaguzi tu?

Halafu kinachoninyima raha ni kwamba kwa CCM maandalizi ya uchaguzi maana yake ni pamoja na kupiga propaganda za kijinga kama anavyowaagiza wasaidizi wake kwamba, waende vijijini wakapeleke habari kuhusu mambo yanayofanywa na serikali yake, kana kwamba hawana macho.

Badala ya kujielekeza katika mipango ya kukuza uchumi aliyowaahidi wananchi ndani ya miaka mitano, yeye anaongelea uchaguzi. Kwa kweli kama ni cha mtema kuni, sasa watanzania tunakipata kweli kweli kwa kumchagua huyu mswahili.
 
Kumekuwa na 'lack of consistency' kwenye message toka kwa Rais Kikwete na hata viongozi kadhaa ndani ya CCM. Mara kadhaa wamenukuliwa wakisema kuwa uchaguzi uliisha na sasa ni muda wa kufanya kazi, sasa anasema kuisha kwa uchaguzi mmoja ni mwanzo wa uchaguzi mwingine.
 
Wamechanganyikiwa hawajui hata wanachokisema.
 
Ana maana waige toka kwa chadema hakuna kulala!ndio maana anakazania eti na mawaziri makatibu wakuu waende vijijini.
 
Ana maana waige toka kwa chadema hakuna kulala!ndio maana anakazania eti na mawaziri makatibu wakuu waende vijijini.

Waende huko vijijini kwa gharama za nani? Hivi mkweere anazo kweli!! Kama yapo mazuri yanayoonekana kwa wananchi kuna haja gani ya mawaziri kwenda vijijini kuwaeleza!? Hizo ndiyo propaganda! Kwa ujumla, kwa miaka sita na mingine minne ijayo, nchi hii hatuna kiongozi.
 
Wamechanganyikiwa hawajui hata wanachokisema.

Yaani badala ya kukimbilia kutekeleza ahadi zao CCM inakimbilia kwa wananchi eti "kuelezea mazuri yaliyofanyika!" Kwa nini hayo yaliyofanyika (kama yapo) yasijieleze menyewe?
 
Ndugu zangu,

Nimemsikia Kikwete akiwaambia mawaziri kwenye semina elekezi Dodoma kwamba uchaguzi unapoisha unaashiria mwanzo wa uchaguzi unaofuata. Hivi nchi hii itakuja iendelee lini jamani kama mawazo ya kiongozi wetu yanajielekeza kwenye uchaguzi tu?

Halafu kinachoninyima raha ni kwamba kwa CCM maandalizi ya uchaguzi maana yake ni pamoja na kupiga propaganda za kijinga kama anavyowaagiza wasaidizi wake kwamba, waende vijijini wakapeleke habari kuhusu mambo yanayofanywa na serikali yake, kana kwamba hawana macho.

Badala ya kujielekeza katika mipango ya kukuza uchumi aliyowaahidi wananchi ndani ya miaka mitano, yeye anaongelea uchaguzi. Kwa kweli kama ni cha mtema kuni, sasa watanzania tunakipata kweli kweli kwa kumchagua huyu mswahili.

Nafikiri hili pia lielekeze kwa watani wa CCM wanaoota kuchukuwa madaraka hata huo muda wa uchaguzi haujafika!
 
Nafikiri hili pia lielekeze kwa watani wa CCM wanaoota kuchukuwa madaraka hata huo muda wa uchaguzi haujafika!

WALIOCHANGANYIKIWA ZAIDI NI CHADEMA AMBAO MARA BAADA YA UCHAGUZI WAMEANZA "KUTEKELEZA" AHADI ZAO KWA WANANCHI WALIOWACHAGUA MAJIMBONI NA KWENYE KATA KWA MAANDAMANO YASIYO NA KICHWA WALA MIGUU!! Tatizo hapa ni Slaa, hana kazi ya kufanya, hivyo anawashinikiza wenzake waache majimbo yao na kuhangaika hovyo na hoja ambazo wangeweza kabisa kuzi-raise Bungeni! Mshaurini Slaa, atulie kumsaidia "mchumba" ajifungue salama kajukuu.
 
Mbona unaandika mambo ya taarabu hapa? Inaonekana Dr. Slaa (PhD) ndiyo main issue kwako. Usituletee chuki binafsi hapa!
 
WALIOCHANGANYIKIWA ZAIDI NI CHADEMA AMBAO MARA BAADA YA UCHAGUZI WAMEANZA "KUTEKELEZA" AHADI ZAO KWA WANANCHI WALIOWACHAGUA MAJIMBONI NA KWENYE KATA KWA MAANDAMANO YASIYO NA KICHWA WALA MIGUU!! Tatizo hapa ni Slaa, hana kazi ya kufanya, hivyo anawashinikiza wenzake waache majimbo yao na kuhangaika hovyo na hoja ambazo wangeweza kabisa kuzi-raise Bungeni! Mshaurini Slaa, atulie kumsaidia "mchumba" ajifungue salama kajukuu.

check hiyo red, wakulaumiwa ni umati wa wananchi wanaojitokeza kwenye hayo maandamano. logic ni kwamba wananchi woooote wale ni wajinga kwa kushiriki maandamano yasiyo na kichwa wala miguu! by the way, naomba tenda ya kuwaandikia na kuwakabidhi barua mapacha watatu maana siku 90 zimeisha.
 
Ndugu zangu,

Nimemsikia Kikwete akiwaambia mawaziri kwenye semina elekezi Dodoma kwamba uchaguzi unapoisha unaashiria mwanzo wa uchaguzi unaofuata...

... kwa CCM maandalizi ya uchaguzi maana yake ni pamoja na kupiga propaganda za kijinga kama anavyowaagiza wasaidizi wake kwamba, waende vijijini wakapeleke habari kuhusu mambo yanayofanywa na serikali yake, kana kwamba hawana macho.

Badala ya kujielekeza katika mipango ya kukuza uchumi aliyowaahidi wananchi ndani ya miaka mitano, yeye anaongelea uchaguzi...

Believe you me tatizo kubwa kuliko vyote kwa JK ni uwezo mdogo sana wa kiuongozi in all wises. Kwa hili huitaji kwenda mbali zaidi ya kufuatilia his many semina elekeza..

Nakubaliana nawe kabisa. ..Imagine semina elekezi ambazo hazigusii mikakati ya ku-address issue zinazowagusa watz kama ajira, nishati, kupanda kwa gharama za maisha etc Kila mara JK ni ku-recite matatizo ya wananchi...

The worst ni kwamba kama waziri hatawajibika the best anachofikiri JK ni kwa waziri kujiondoa na si yy kumwajibisha ... what a weak leader

My take ni kwamba kutokana na uwezo mdogo na kushindwa kutoa leadership JK ameshindwa kabisa hata kutumia institutions za kiserikali zilizopo kuondoa kero za maisha kwa watz.

Nafikiri tumejifunza (unfortunately) the hard way kuwa in future tunahitajika kuchagua viongozi wenye uwezo na tuachane na mtindo wa kuchagua viongozi for convenience tu.
 
Uliyoyasema ni sahihi sana mwana JF. Kiongozi wetu huyu kumbe anatusikitisha wengi sana. Kwa kweli kama ni kupotea hapa tulipotea completely. Huu mtaji wa CCM according to Makamba Sr unatucost sana.

Nadhani tatizo lingine ni kwamba tulichagua mtu ambaye hajui majukumu ya kazi aliyoiomba. Kwa mfano anasema kuwa rushwa imetawala kwenye Wizara, SO WHAT!!!!! Nani mwenye jukumu la kuhakikisha kuwa rushwa inadhibitiwa. Kama imetawala si ina maana Hoseah ameshindwa kazi. Sasa kiongoz mkuu akilalamika hivyo ndo nini sasa. What a weak leader.....!!!!!
 
Kujiepusha na vidonda vya tumbo......mi huyu jamaa siku hizi simsikilizi tena. Nothing good will come out of him anyway.
 
,...Tatizo hapa ni Slaa, hana kazi ya kufanya,...

Ufupi wa akili yako ndio unakuharibu. Kikwete alisema kwenye hotuba yake ya mwisho wa mwezi kwamba uchaguzi umekwisha , sasa tufanye kazi. Sasa anawaambia wenzie kuwa mwisho wa uchaguzi ni mwanzo wa uchaguzi mwingine! Hapo huoni yeye ndio tatizo!? Dr Slaa ndio alimtuma kutuletea hizo staki nataka kama binti anayetongozwa? Nawa uso uone mbele. Huu sio wakati wa mipasho!
 
WALIOCHANGANYIKIWA ZAIDI NI CHADEMA AMBAO MARA BAADA YA UCHAGUZI WAMEANZA "KUTEKELEZA" AHADI ZAO KWA WANANCHI WALIOWACHAGUA MAJIMBONI NA KWENYE KATA KWA MAANDAMANO YASIYO NA KICHWA WALA MIGUU!! Tatizo hapa ni Slaa, hana kazi ya kufanya, hivyo anawashinikiza wenzake waache majimbo yao na kuhangaika hovyo na hoja ambazo wangeweza kabisa kuzi-raise Bungeni! Mshaurini Slaa, atulie kumsaidia "mchumba" ajifungue salama kajukuu.

nauyo nape anafanya nn majukwaani tatizo lenu hamkuchaguliwa 2010 bali mli force 2015 hatukubali
 
Pole sana! sasa kama mnaweza jaribu muone kama hamjapigwa mawe na raia, ujue ccm sasa hvi hata hamtambuliki km mpo nchi hii isipokuwa tunawatambua kama mpo kwa uovu na majeraha mnayozidi kutupa!

Sasa kama hamjipendi sogezeni kwato na rangi zetu mbaya hi mitaa yetu na hivi hakuna umeme uku, tunawamaliza na giza la mawe! Ukweli ni kwamba ccm bila kujua tayari kuipigia campen CHADEMA kwa uovu mnaotutendea!

Naskia mmetangaza giza na kufungwa kwa viwanda sababu ya kukosa umeme mwezi mzima! Hivi mnafikiri nani ataipenda serikali yenu! yani mnashindwa kufikiri namana gani ya kutafuta suruhisho la maana ispokuwa kuzima na kukaa gizani.
 
Acha awatume tena mawaziri kuitangaza ccm km hawajapopolewa mawe.............kikwete anatuma wenzake huku akijua kua yeye mwenyewe tu akipitapita mitaa ya pale mbeya anakula kichapo cha mawe...labda waende huko kwenye mikoa ya ajabuajabu ambao muda wote wanapiga makofi na kuchagua sura
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom