Yapi nu mazuri na yapi ni mabaya kwenye waraka wa Wakatoliki?

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,621
2,567
Waraka wa Kanisa Katoliki umeungwa mkono na pia umepingwa na watu wa aina mbalimbali. Lakini watu wengi waliweza kusema kwa jumla tu kuwa ni mzuri au mbaya bila kusema ni mambo gani yamewagusa ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi na mambo gani ni mabaya ili yaachwe.

Kwa maana hiyo, inawezekana kabisa kuna watu tumewaacha kwenye giza kabisa. Najaribu kuona kama kuna namna ya kujadili kwa kuchambua: mfano, je tunaweza kuonesha ni mambo gani yameweza kutugusa, ambayo tunaweza kuyatumia au kuyaboresha ili tuwe na maendeleo zaidi kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni? Pili ni mambo gani tunaweza kusema hayatufai?
 
Hii ishu ya Waraka imejadiliwa sana hapa. Mbali ya kutundika nakala ya waraka wenyewe halisi, pia michango mingi sana imewekwa hadharani, fanya marejeo huko nyuma!
 
Back
Top Bottom