Yapi ni Maono ya Taifa la Tanzania huko tuendako?

Gellangi

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
2,756
2,996
Tanzania kama Taifa mojawapo hapa Duniani lazima iwe na Dira na Maono yanayoonyesha jinsi na namna itakavyojiendeleza kitaifa na kimataifa.

Kuna vipindi tumeshuhudia tukiletewa mipango ya muda mfupi,kati na mrefu ya Taifa Letu,tatizo ni maono,dira na mipango gani hiyo tuliyoweka?

Hayo maono yanapangwa na nani na kwa kuzingatia nini?

Tukiambiwa kuwa kuna mipango ya Taifa halafu hadi Leo hatuchimbi kwa ufanisi chuma kiasi tunaagiza mataruma ya sgr kutoka China?

Tuna Coal ambayo karibu inapitwa na muda Wa kutumika Duniani kabla hatujaichimba!

Kuna maono Ama dira ya Taifa wakati kilimo chetu ni cha kusubiri mvua badala ya umwagiliaji?

Kama Tanzania haitaandika Katiba yake upya na kuanza upya,hakika hakutakuwa na maana ya kuwa huru.

Kupitia Katiba Mpya Maono/Dira ya Taifa shirikishi vitawekwa upya.
 
Kwa sasa jambo la msingi ni kufuta ligasi ya mwendazake, mengine yatajua yenyewe.
 
Kwa sasa jambo la msingi ni kufuta ligasi ya mwendazake, mengine yatajua yenyewe.
Hiyo legacy inafutwaje ama inalindwaje katika hali ya kawaida?Sikuwahi kufahamu kwamba legacy ni kitu chenye thamani hivyo kiasi kuwa inatafutwa,inatengenezwa ama inalindwa kwa gharama kubwa hivyo?Hii legacy ni kwa faida au manfaa ya nani hasa?Seriously kwenye mkwamo tuliopo Watanzania,kuna watu wanashughulika kuzilinda na wengine wakibomoa!Hawana kazi za kufanya?
Mada niliyoleta hapa jukwaani lengo lake ni kufungua mjadala wa nini Dira ya Taifa letu?Mbona inaonekana tunatekeleza mawazo,maono,dira za wanasiasa wanaotawala?Huko CCM kwenyewe hakuna vichwa vya kufikiria mambo kwa upana nje ya vipindi vya uchaguzi.Kila anayekuja ana lake.Mwl.Nyerere na Ujamaa na Kujitegemea tuakafeli,Mzee Mwinyi kaja na Rukhsa kila kitu,tukaangukia pua.Ikaja enzi ya Mkapa na Ukweli na Uwazi.Hapo tulikuja kushuhudia usiri mkubwa uliofanywa,vikauzwa kwa mnada wa mali kauli viwanda vyetu,nyumba zetu,ardhi/wanyama kama Twiga na hata sisi almanusra kama hatukuuzwa.
Kila zama na kitabu chake,ikawa zamu ya Kikwete wetu na mbwembwe zake za Ari,kasi na nguvu mpya,tukaaminishwa kuwa tunaandika Katiba Mpya gharama kubwa na hatukuipata.Tanzania kweli kichwa cha mwenda wazimu maana kila kinyozi anakigeza atakavyo.
Dhahma ikatukumba chini ya Bulldozer,vikazinduliwa viwanda usiku na mchana lakini vikayeyuka mchana kweupe.Tanzania ya viwanda haipo ya Magufuli ikatubagaza,ikatunyanyasa ilivyopenda akisaidiwa na Chieftress wetu wa Royal Tour.
Dira ya Taifa la Tanzania ni ipi?Dira ya Taifa inapatikanaje?Utekelezaji wa Dira/maono ya Taifa lazima uwe shirikishi na jumuishi.Dira ya Taifa ndiyo inatakiwa kutuongoza kupata pamoja na viongozi pia ni kuwafanya wananchi wawe sehemu ya maandalizi ya Dira.
Wananchi wa Tanzania lazima waandike Katiba Mpya na kujiwekea Dira itakayowaongoza kufikia kilele cha ustaarabu(maendeleo).
 
Mkuu
Taifa la Tanzania
Litazaliwa upya Baada ya katiba mpya kupatikana na Zama hizi kutokea uhuru zitaaandikwa kama Zama za giza!!!
Duru hapa jukwaani zinatanabaisha katiba mpya itapatikana 2026 na Raisi samia atakuwa Raisi wa mwisho wa Zama za Giza.
Na maono ya taifa yatazaliwa upya wakati huo!
KWA Sasa Taifa halina maono linategemea utashi wa Raisi anayetawala!!
 
Tuna Coal ambayo karibu inapitwa na muda Wa kutumika Duniani kabla hatujaichimba!
Sasa hivi imeanza kuchimbwa na kusafirishwa Nchi jirani kwa kasi ya ajabu kitu ambacho kinatia faraja sana na kuna Ajira nyingi zimetengenezwa.

Naongelea Makaa ya Mawe ya huko Songea.
 
Hatuna Dira, Nchi inaendeshwa na ilani ya vyama siasa na hazitekelezeki, sababu zinabadilika kila baada ya miaka 5 ya uchaguzi, na nyingi ni uongo, sio za kitaalam.
 
Back
Top Bottom