Yani mpaka sasa wataalam wetu hawajajua ni kitu gani kilianguka Kagera

sisi tulio mbali na kagera tutaaminije mnachokisema?, kama kweli kuna kitu kimeanguka picha ihusike hapa, sio kuishia kusema mliona mwanga, kama ni mwanga watu huwa tunauona sana.

Wekeni picha, atafutwe prof. Muhogo na watu wa anga majibu lazima yatapatikana.
 
Hivi iweli hakuna radar au chombo kingine cha 'kuona' vitu kama hivyo? Yaani ingekuwa ni shambulizi toka nchi jirani hakuna ambaye angejua mpaka vitu vyote vimeshabomolewa? Inatisha !!
 
Kweli sisi bado sana, yani mpaka sasa hakuna taasisi yeyote au msemaji wa taasisi yeyote inayohusika na mambo ya geology au ulinzi au mambo ya anga au majanga ambaye ameweza thibitisha ni kitu gani kimetokea Kagera na kusababisha kishindo na ule mwanga ulioonekana angani.

Nasikia tu wanasema kama kuna mwananchi au wananchi waliokuwa karibu wajitokeze waseme nini kilichotokea.
Ndiyo maana waka MV Bukoba inazama Waingereza walitangulia kupata taarifa kabla vyombo vyetu hata havijapata taarifa ikabidi wavipatie taarifa.

Soma > Kagera: Kimondo chadondoka Bukoba
Usikute alianguka jiwe
 
Si pana Idara ya Jiolojia pale UDSM? Wanashindwaje kuchukua sample ya hicho kitu, kukifanyia uchunguzi, na kutoa majibu kwa wananchi? Anyway, isije ikawa mabaki ya madude ya Kim yalikosea njia! Ee Mola wetu tunusuru!
Wataalamu wa Jeologia kama ni Kimondo kweli hawana msaada hapo, labda kama wanataka kujifunza zaidi, wataalamu wanaotakiwa kulitolea maelezo hili ni kutoka fani ya Astronomy,labda tuwaulize UDSM kama wapo. Hii ni fani inayotawaliwa zaidi na warusi na wamarekani. Kinachoweza kufanyika ni kuwasilina na balozi za nchi hizo mbili ili kwa msaada wa kile kituo cha kimataifa cha angani "ISS" waweze kuangazia anga yetu, aidha kurejea historia ya matukio katika anga yetu ili kubaini kitu kisicho cha kawaida kilichoingia kwenye anga yetu.
 
Hata wataalam wetu wa hali ya hewa wanaiba data za weather focust kwa kuangalia CNN na BBC
Huu ndio wakati wa kufikiria kuweka angani satilaiti yetu itakayoangazia anga yetu na kufuatilia mwenendo wa hali ya hewa. Ikiwa Nigeria walifanikiwa kuwa na yao, bila shaka na sisi tunaweza.
 
Mkuu wa Mkoa alisema kama kuna mtu alisikia au kuona tukio kwa ukaribu zaidi awape taarifa ili wajiolojia wapate pa kuanzia.
Hicho ni kitu kisichojulikana hakitajulikana, tufahamu tu kuwa kuna muungurumo mkubwa na mwanga mkali usioleleweka ulitokea Kagera basi.
Wajiologia wenyewe wanawauliza wananchi ni kitu gani wananchi nao wanawaliza kilikua ni nini.
Ni sawa na daktari kumuuliza mgonjwa" nikupe dawa gani"?
 
Tuache kubashiri kama TMA. Wameshatufikisha mahali sasa tumerudi enzi zetu zilee kuwavizia ndege flan flan. Wakianza kutengeneza viota tunajua kuwa mvua zi karibu. Wengine wakianza kulia wa kwanza asubuhi tunajua mvua ipo leo. Wale wa Kilimanjaro, mkiona barafu imetanda tangu miguuni mwa milima mnajua mvua hiyooo.
Imebidi tufanye hivyo kwa sababu wale sasa hawatoi utabiri bali ubashiri wa mvua. Walisema vuli mwaka huu itakuwa hata zaidi ya wastani. Ati tangu wiki ya pili ya September. Sijui leo ni August au July. Hatujaona hata tone.
Msiwasumbue hao majeolojisti watoke Darisalama hadi Bukoba kwenda kusaka nyota iliyokosea njia ghafla na kujirudia kwenye njia zake mbinguni. Kama kilidondoka, mbona majeshi yasiende kukilinda?
 
Mkuu wa Mkoa alisema kama kuna mtu alisikia au kuona tukio kwa ukaribu zaidi awape taarifa ili wajiolojia wapate pa kuanzia.
Hicho ni kitu kisichojulikana hakitajulikana, tufahamu tu kuwa kuna muungurumo mkubwa na mwanga mkali usioleleweka ulitokea Kagera basi.
Wajiologia wenyewe wanawauliza wananchi ni kitu gani wananchi nao wanawaliza kilikua ni nini.
UNADHANI HATUJUI? TUNAWACHORA TU... MUDA SI MCHACHE KINANGUKIA MAGOGOGNI....
 
Back
Top Bottom