Yani mpaka sasa wataalam wetu hawajajua ni kitu gani kilianguka Kagera

itakuwa tyre burst tu!!!! watanzania huwajui??huu mji wa dar watu walijazana buguruni wiki eti mtu kageuka chatu na mpaka leo hata nyumba ya hilo tukio haijulikani
Duh umenikumbusha mbali Sana "Niende buguruni nikanunue viatu, naona ajabu mtu kugeuka chatu" songi hilo !!!
 
Hivi tukijitathmini kama jamii au nchi, na sisi tunaweza kusema tunaishi kweli. Kila jambo linajiendea tu, hatuna ufahamu wala udhibiti wa lolote. Si usalama (watu wanatoweka mpaka Mungu saidia wanarudi wenyewe au), uchumi unaporomoka, mvua zikinyesha, mafuriko mijini miaka nenda miaka rudi, ziwani vyombo cha usafiri havieleweki, barabarani ajali kila kukicha, hatuna uvumbuzi wala werevu wa kutatua matatizo yetu, tupo tupo tu.
 
Back
Top Bottom