Yanga yasitisha pre-season yao huko Morocco kurejea nchini kwa mafungu

Tripo9

JF-Expert Member
Sep 9, 2009
4,352
3,533
1) Eti sababu wachezaji kama nane wataitwa kwenye nchi zao kwa michezo ya kimataifa hivyo timu itameguka

2) Eti sababu kule kambi iliko joto Sana.

3) Eti tuna mechi wiki ya mwananchi na wale Wanigeria pia.

My take:
Waseme tu pesa imekata.

kwani walipoenda au kupanga kwenda huko hayo mambo hawakuya consider?

Jiisiiem mbona mnawatapeli uto jamani. Wameshaanza kushindwa kabla ya kushindana!
 
Ndo shida ya kulala sebuleni unakuwa wa mwisho kulala na wa kwanza kuamka.

Wanaona aibu kusema kuwa ile Ofa imekwisha.

Yaani wachezaji wachache wanaghairi kuweka kambi..! Mbona Mnyama Mkali ana wachezaji kwenye Timu ya Taifa na bado Timu inajifua mpaka mwisho wa mwezi..Nyieee.
 
Hii ndo shida ya kuishi maisha sio yao, semeni tu ukweli kwanini mmevunja kambi, mnafanya vitu kushindana na Simba hamtatuweza guys hii Simba kufika hapa sio km upepo tu.

Fanyeni kwa uwezo wenu ishini maisha yenu, acheni janjajanja wadanganyeni hao mashabiki zenu wasiojielewa.

Mo akisema anaweka pesa anaweka kweli hao GSM wanawapiga janjajanja tu wachezaji waliitwa mapema team za taifa nadhan ustarabu ilikua nikwenda kuweka kama mapema huko morocco vinginevo mgebaki huku huku bongo au mgeweka hata kambi hapo bagamoyo
 
Kuna tetesi kuwa Waliahidiwa kulipiwa kilakitu na wenyeji wao, sasa walivyofika kule wakahama mji ili kambi isiwe karibu na Simba. Hivyo wenyeji wao wamegoma kuwalipia kambi ya mji mwingine.

Yanga wameshindwa kujilipia wenyewe, wameona Bora warudi Nyumbani.
 
Kuna tetesi kuwa Waliahidiwa kulipiwa kilakitu na wenyeji wao, sasa walivyofika kule wakahama mji ili kambi isiwe karibu na Simba. Hivyo wenyeji wao wamegoma kuwalipia kambi ya mji mwingine.

Yanga wameshindwa kujilipia wenyewe, wameona Bora warudi Nyumbani.
Dah. Sasa si waseme ukweli Tu. Kuiga tembo msamba uko

Sent from my Redmi 7A using JamiiForums mobile app
 
Mbumbumbu wengi hawana reasoning

1.Kilele cha wiki ya mwananchi ni tar.29/8/2021 na leo ni ni tar. 23,kwa hesabu hapo zimebaki siku sita mpaka siku hiyo kufika na timu ipo Morroco na safari yake inachukua siku mbili mpaka kufika Dar es Salaam, kwahyo hapo zinabaki siku nne pia kuna uchovu wa safari na kuendelea na mazoezi kwa ajili ya mtanange wa wiki hiyo ya mwananchi
Tupo mule mule tu.

Wachezaji wanatakiwa timu ya Taifa
1.Kabwili
2.Feisal
3.Mauya
4.Job
5.Mwamnyeto
6.Yacouba
7.Mokoko Tonombe
8.Djagui Diarra

Kimsingi hapo kwa tuliosomea coaching hasa ukiwa kambi ya maandalizi ya msimu bila kuwa key players wako, hapo huwa tunahesabu hakuna maana ya kuwa na kambi hiyo, automatically kuna mbinu ulikuwa uzitoe lakini utashindwa kutokana na kukosekana kwa baadhi ya wachezaji wako muhimu

Na isitoshe wiki ya mwananchi ipo ukingoni sina shaka kumuelewa Coach Nabi na Eng. Hersi said
 
Hata huku kwa watani kinachowapa nguvu ni kwamba mechi zao za kimataifa zitaanza mwezi wa 10 na mechi yao ya kwanza kimashindano itakuwa itakuwa September mwishoni kabisa ikiwa ni ya Ngao ya hisani wakicheza na wapinzani wao Yanga, hivyo wana faida kubwa kimaandalizi

Na ndio maana hata simba day wamesogeza mbele na hii ni kutokana na urafiki wa ratiba walio nayo na hilo halina shaka

Hii ni tofauti kwa watani wao Yanga ambapo kabla ya kukutana kwenye ngao ya hisani watakuwa wamesha cheza almost mechi mbili tena za kimataifa tena zenye kuamua hatima hatma yao kwenye yao kwenye CAF Champions league

Hivyo basi kama usipokuwa mbumbumbu utakuwa unaelewa nini Yanga wanakifanya
 
Mbumbumbu wengi hawana reasoning

1.Kilele cha wiki ya mwananchi ni tar.29/8/2021 na leo ni ni tar. 23,kwa hesabu hapo zimebaki siku sita mpaka siku hiyo kufika na timu ipo Morroco na safari yake inachukua siku mbili mpaka kufika Dar es Salaam
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano wa klabu ya Yanga Sc Eng Hersi Said amethibitisha kuwa timu hiyo imesitisha kambi nchini Morocco 🇲🇦 na sasa itarejea nchini kwa mafungu mawili tayari kwa kumalizia maandalizi ya msimu mpya kabla ya kuanza msimu rasmi

Eng amesema sababu za kuvunja kambi hiyo ni timu kumeguka kutokana na wachezaji nane kuitwa timu zao za Taifa lakini pia ukaribu wa mechi zao ikiwemo ile ya Siku ya Mwananchi pamoja na mechi ya kwanza ya Kimataifa ambazo zote zitapigwa jijini Dar Es Salaam

Hersi ameongeza kuwa hali ya joto ya Morocco ni kubwa sana tofauti na ya jiji la Dar Es Salaam hivyo kwasasa ni wakati sahihi kwa wachezaji wao kuzoea hali ya joto la nyumbani kuelekea kwenye mchezo wa kwanza wa Kimataifa

Chanzo: Mwanaspoti

Tatizo nikurud mafungu mafungu hapa ndo wasi wasi unazid inatufanye tuamin mpunga umekata afu machezaji walingwazwa week 3 zilizo pita kama mantiki hiyo kulikua na haja gani ya kwenda kuweka kambi siku5 si bora mgebaki bongo tu
 
Hizo mbinu angetoa kwa wachezaji 22 waliobaki
Kumbuka na kilele cha wananchi kipo mwisho wa wiki hii yaani Jumapili, Je utasafiri lini na kufika Dar es Salaam na pia uzinduzi wa jezi za wananchi lazima ufanyike Dar es Salaam kwa wachezaji wote

Kubali au kataa, Ratiba kwa timu ya wananchi ipo very tight, ukisema uendelee kukaa Morroco kuna mambo yaliyopo kwenye ratiba utaharibu

Tafadhali msiendeleee kubeba laana ya UMBUMBUMBU kwenye vichwa na maisha yenu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom