Yanga SC yaingia mkataba na GSM wa miaka 5 kutengeneza vifaa vya michezo wenye thamani ya bil 9.1

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
=> Tumeingia mkataba mpya wa kutengeneza jezi na vifaa vya michezo kwa miaka 5 na kampuni ya GSM Group Of Companies wenye dhamani ya Tshs Billion 9.1" Rais wa Young Africans SC Hersi Ally Said

=> Mkataba wa pili utakua ni wa udhamini ambapo GSM italipa Tsh. Milioni 300 kwa mwaka, itakayokuwa ikiongezeka kwa asilimia 10 kila mwaka kwa muda wa miaka 5 kuifanya jumla kuwa na Tsh Bilioni 1.83 kwa miaka 5" Rais wa Young Africans SC Hersi Ally Said

=> Akizungumzia makubaliano Rais wa Young Africans SC Eng.Hersi Said alisema “Tunayo furaha kubwa kuingia makubaliano haya mapya na wenzetu wa GSM, moja ya ajenda zangu katika Uongozi wangu ilikuwa ni kuipa klabu uimara wa kiuchumi ili tuweze kujitegemea"

=> Na mikataba kama hii inaiongezea Klabu thamani na kuiimarisha kimapato, na kama tujuavyo uendeshaji wa vilabu vyetu kunahitaji uiamara wa kiuchumi.

=> “Niwapongeze kampuni ya GSM kwa kuendelea kuwekeza katika Klabu yetu kwani uwekezaji wa namna hii sio tu kunaongeza thamani timu yetu bali inasaidia kwa namna nyingine kukuza soka nchini kwetu kwa ujumla” Rais wa Young Africans SC Hersi Ally Said

=> Niwaombe mashabiki, na Wanachama wa Young Africans SC waendelee kuiunga mkono kampuni ya GSM kwa kunununa bidhaa na huduma zao ili waendelee kunufaika na udhamini wao kwetu” Hersi Ally Said, Rais Young Africans SC.
 
Klabu ya Young Africans ya jijini Dar Es Salaam, leo imesaini mkataba mpya wa udhamini na kampuni ya GSM wenye thamani ya jumla ya Tsh Bilioni 10.9 kwa miaka mitano.

Mkataba huo uliogawanyika sehemu mbili utahusisha, mkataba wa kwanza wa uzalishaji na usambazaji wa jezi pamoja na bidhaa mbalimbali za klabu ambapo kila mwaka GSM group itailipa Yanga SC Tsh Bilioni 1.5 ambayo itakua inaongezeka kwa 10% na kufanya jumla ya thamani kuwa Tsh Bilioni 9.15 ndani ya miaka mitano.

Mkataba wa pili utakua ni wa udhamini ambapo GSM italipa Tsh Milioni 300 kwa mwaka itakayokuwa ikiongezeka kwa 10% kila mwaka kwa muda wa miaka 5 kuifanya jumla kuwa na Tsh Bilioni 1.83 kwa miaka mitano

Akizungumzia makubaliano hayo mbele ya waandishi wa habari, Rais wa klabu ya Young Africans EngHersi Said alisema

"Tunayo furaha kubwa kuingia makubaliano haya mapya na wenzetu wa GSM, moja ya ajenda zangu katika uongozi wangu ilikuwa ni kuipa klabu uimara wa kiuchumi ili tuweze kujitegemea. Na mikataba kama hii inaiongezea klabu thamani na kuiimarisha kimapato, na kama tujuavyo uendeshaji wa vilabu vyetu kunahitaji uiamara wa kiuchumi"

"Niwapongeze kampuni ya GSM kwa kuendelea kuwekeza katika klabu yetu uwekezaji wa namna hii sio tu kunaongeza thamani timu yetu bali inasaidia kwa namna nyingine kukuza soka nchini kwetu kwa ujumla"

"Niwaombe na Wanachama wa Young Africans SC waendelee kuiunga mkono kampuni ya GSM kwa kunununa bidhaa na huduma zao ili waendelee kunufaika na udhamini wao kwetu"

Kwa upande wa mdhamini, Mkurugenzi wa Biashara toka GSM Group Bw. Allan Chonjo alisema. "GSM imeona matunda makubwa sana.
 
Umesoma mkataba ukaelewa? Yanga anachukua bil 9.1 kwa miaka mitano. Chukua bil 9.1 gawanya kwa 5 utapata kiasi wanachochukua Yanga kwa mwaka
Wakati simba anapga bil 1 kwa mwaka
Ebu tuambieni nyie vunja bei anawapa ngapi kwa mwaka na alisaini mkataba wa miaka mingapi tuanzie hapo kwanza

Mkataba waliongia simba na vunja bei mwaka jana thamani ni bil 2 kwa miaka miwili
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom