Yanga yamuongeza kiungo nwingine,ni Rafael Daudi wa Mbeya City!

Wonderful

JF-Expert Member
Apr 8, 2015
7,347
5,980
Kiungo wa Mbeya City, Raphael Daud amethibitisha kusaini mkataba wa miaka mwili wa kuicheza Yanga msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.


Akizungumza kupitia kipindi cha Mshikemshike viwanjani cha Azam Tv, Daud alidokeza kukubaliana kwake na uongozi wa Yanga kwa ajili ya kusaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo.


“Nimefikia makubaliano rasmi na uongozi wa timu ya Yanga kwaajili ya maandalizi ya kuichezea msimu ujao na Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani,” alisema Daudi.


Kiungo huyo alisema taratibu zote za kusaini mkataba na Yanga zimekamilika na zitasimamiwa na kaka yake atakayekuwa na wakili wake.


Daud na Kenny Ally aliyesajiliwa na Singida United walitengeneza kombinesheni nzuri katika safu ya kiungo ya Mbeya City kwa misimu miwili mfululizo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom