YANGA yakasirishwa na SIMBA SC, kumsajili BM33, watoa tamko

Tukiacha ushabiki wa Simba na Yanga mimi binafsi nadhani viongozi wa Simba walihitajika kutumia busara tu ya kawaida wangesubiri mpaka jumatatu ndio wamtangaze Morison kuwa mchezaji wao baada ya TFF kutoa uamuzi wake. Sielewi ni kwanini viongozi wa Simba wameshindwa kuwa na subira katika jambo hili dogo . Na ni nini kimewapa jeuri hiyo viongozi wa Simba ili hali mchezaji bado hukumu yake haijatolewa na TFF/ Polisi au hiyo hukumu imeshavuja? Je katika hali ya uswahili kama huu wapenzi wa mpira nchini waendelee kuamini kuwa Simba inaendeshwa kisasa? Viongozi wa Simba wamejiandaaje iwapo hukumu ikitokea kuwa Yanga wameshinda kesi dhidi ya Morison?

Yote kwa yote ukweli lazima usemwe kuwa Morisoni ni bonge la mchezaji ndani ya uwanja lakini nje ya uwanja jamaa ni "comedian" bab kubwa hata "makomediani" wenye fani yao wanazima fegi. Lakini napata mashaka sana na nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa zile komedi zote alizofanya Morison akiwa Yanga ilikuwa tu ni kwa sababu alikuwa ana ugomvi binafsi na viongozi waYanga na si tabia yake. Tabia ni kama ngozi haifichiki je viongozi wa Simba wamejiandaa vipi kukabiliana na vituko vya huyu mchezaji iwapo ataanza "ukomedian" wake pale Simba?

Mwisho nikiangalia kote Morison alikopita kuna sehemu moja au mbili hivi alikuwa na matatizo ya mikataba. Kwa hiyo hii sio kesi ya kwanza kuhusiana na mkataba wake wa kazi. Je GSM hawakuliona hili mapema na iwapo walilijua hili mapema je walichukua hatua gani? Je nao Simba hawalijui hili na kama wanalijua wamechukua tahadhari gani isije wakawa wahanga wa kuingizwa "king" na mtukutu Morison?
Jumatatu sio mbali nadhani ndio muda tutakapoanza kuona mwanga wa hili suala na majibu mengi sana wanaojiuliza wapenzi wa soka nchini yataanza kupata majibu baada ya TFF/ Polisi kutoa taarifa ya uchunguzi na maamuzi ya hili sakata. Na pia itakuwa fursa nzuri sana ya kuanza kumwelewa huyu mwamba wa Ghana maana mpaka sasa sidhani kama kuna mpenda soka nchini anayeweza kusimama mahali na kumwelezea huyu jamaa ni mtu wa nama gani kutoka na vitendo vyake anavyovifanya.
Hii essay ataisoma nani Sir?
 
Ukitaka kumuua adui unapiga kichwani. Mpinzani mkubwa wa simba ni yanga lazima umpige nje ya uwanja.
Wapinzani wa Simba ni
TP mazembe
Mamelodi Sundown
Al Ahly
Zamalek
Espérence de Tunis
Étoile du Sahel
Wydad Casablanca
Raja Casablanca

Waache kubaki na mawazo mgando, yaani viongozi wanajitamba eti tunasajili ili Yanga waumwe mioyo

Shame shame shame

Simba isajili ili ipambane CAF Champions league sio kupambania kombe mechi 38 mshindi wa kwanza anapewa tsh 100 milion
Wakati CAF Champions League
Mshindi 2.5 milion USD mechi 15 (5.625 Bilion tsh apprx.)
Nafasi ya 4 kwa group 550000 USD (1.2375 Billion tsh apprx.)
 
Kaka Punguza jazba. Tatizo lenu Yanga mliahadaika na kukubali kukabidhi timu yenu kwa wauza jersey na matapeli maarufu hapa mjini .Simba wapo makini mno "Mwamwedi" hajawahi kuingizwa mkenge kirahisi hivyo subirini Jumatatu mpewe taarifa za usanii uliofanywa na hao matapeli wenu maarufu hapa mjini (Wazee wa Forgery). Na inawezekana wakafungiwa kudhamini Club yenu wasipojiangalia.
Ok inawezekana uko sahihi..lakini Simba watafanyaje usajili wakati suala liko tff?? Je wana watu ndani ya tff ambao waliwadokeza kuwa nyie endeleeni tu kwani mkataba wa Morrison ni wa forgery?
 
Wapinzani wa Simba ni
TP mazembe
Mamelodi Sundown
Al Ahly
Zamalek
Espérence de Tunis
Étoile du Sahel
Wydad Casablanca
Raja Casablanca

Waache kubaki na mawazo mgando, yaani viongozi wanajitamba eti tunasajili ili Yanga waumwe mioyo

Shame shame shame

Simba isajili ili ipambane CAF Champions league sio kupambania kombe mechi 38 mshindi wa kwanza anapewa tsh 100 milion
Wakati CAF Champions League
Mshindi 2.5 milion USD mechi 15 (5.625 Bilion tsh apprx.)
Nafasi ya 4 kwa group 550000 USD (1.2375 Billion tsh apprx.)
Sifa mojawapo ya kushiriki klab bigwa lazima ushinde ligi kuu bara, mshindani mkubwa wa simba ni yanga usisahau hilo mkuu.
 
Yanga walisha peleka mkataba wa Morrison TFF tena mkataba ambao Tff kupitia mtaalamu wao wa TMS wali uidhinisha maana TFF wanaye mtaalamu wa TMS. Yanga wakapeleka malalamiko juu ya mchezaji wao Benard Morrison kurubuniwa na Simba wakati anamkataba wa miaka miwili na wao Tff kimsingi walisha utambua.

Jambo la kushangaza wakati Tff bado hawajatoa maamuzi ya malalamiko ya Yanga, Simba wamemtangaza rasmi kwamba Benard Morrison ni mchezaji waliye msajili. Sasa wapenzi wa mpira tusubiri Tff watachukua uamuzigani juu ya swala hilo.

Endapo timu ikibainika imemrubuni mchezaji pasipo klabu yake kushirikishwa adhabu zake nikama ifuatavyo. Mchezaji atafungiwa miezi 4 au miezi 6.

Klabu iliyo fanya kosa Itapewa moja ya adhabu zifuatazo.

Onyo, fain, kushushwa madaraja mawili, kuzuiwa kufanya usajili. Kwasasa tunawasubiri Tff kwakua picha ndio linaanza.

We muongo sana lini TFF walikiri kupokea mkataba mpya wa BM na Yanga? Hayo maneno ya huyo injinia wenu ndio yanakufanya uandike uongo ? Tshimbimbi jee? Mnajua mlivoji ila mlishindwa kwenye dole gumba sasa subirieni kibao kinavyo wageukia utalia.. hiiiiii vangoshaa
 
Mbona wewe umeumia sana ?why umeumia hivi? Sisi yanga tunafahamu uhuni wa GSM acha yatupate. Wewe unajiita simba na wakati ni yanga mwenzetu na sema tu we ni yanga nyani au mbwa. Luc Eymael. Gsm washenzi wameforge mkataba tunajua sisi tulio ndani
Kamwe sishabikiii rangi ya njano na kijani never
 
Hata kidole gumba walifoji waliweka cha hersi. Hawa jamaa ni manyani kweli kweli.

We muongo sana lini TFF walikiri kupokea mkataba mpya wa BM na Yanga? Hayo maneno ya huyo injinia wenu ndio yanakufanya uandike uongo ? Tshimbimbi jee? Mnajua mlivoji ila mlishindwa kwenye dole gumba sasa subirieni kibao kinavyo wageukia utalia.. hiiiiii vangoshaa
 
Yaani we hapo una akili kuwazidi Simba?

Hata kuandika FIFA tu hujui,uandishi tu unaonesha jinsi ulivyo bogus,leo unawezaje kuisema Simba wewe?
Uyo Morrison kwakua alisha idhinishwa na Tff kimatataifa kama ni mchezaji halali wa Yanga, ina maana inabidi Tff waiandikie barua Fiffa kwamba walikosea kumuidhinisha Morrison kwenda Yanga.
kwakua uyo mchezaji tayari yupo kwenye System za kimataifa kwa mfumo wa kimataifa wausajili kama mchezaji halali wa Yanga,
System haiwezi kukubali tena kumsajili mchezaji mmoja kuchezea timu mbili katika nchi mmoja.
Tff ikitokea waka mwidhinisha Morrison Simba, Yanga wata anzia moja kwa moja Caf au Fiffa. Kitakacho kuja kutokea Simba wataogopa kumchezesha kwakua timu zitamkatia rufaa Caff au Fiffa.Tunaposema Simba ni mbumbumbu fc tunazungumza kwa uhalisia kabisa.
 
Na za uhakika si ajabu hao Simba wakawa wamezipata huko huko TFF na ndio sababu hawana hofu.

Hakika sio wajinga wale.

Washabiki wa hizi timu mbili tumekaa kama washabiki wa kisiasa, tunapelekwa pelekwa sana na viongozi wa hizi timu kama majuha.

Jinsi Yanga wanavyodanganywa na viongozi wao hili sakata la Morrison ni sawa na tulivyowahi kudanganywa kuhusu kupeleka malalamiko FIFA ya kadi ya njano ya Kagera Sugar.
 
Simba wamechungulia kule TFF, kujua kama kuna Mkataba kati ya Yanga na Morison, wamekuta hakuna. Wamesainisha !!!!. Maana Yanga walipeleka Makataba wa Morison TFF na kuusajiri(Kazi ya TFF ni kusajiri Mkataba tu) ambao huyo Morison mwenyewe hautambui na hakuusaini. The contract between parties (Morison and Yanga) is void due to one part (Morison) claim and verification that, those names and signatures on it, is not and never casted by him (Hiyo sheria ya Mikataba iliyovunjika kwa mtu wa upande mmoja wa mkataba kuthibitisha kwamba jina na saini kwenye mkataba sikuiweka mimi), (Non Esto Factum rule). Yanga wanatakiwa kuwa welevu tu, shule muhimu.
 
Kocha wa Yanga alisema mashabiki wa Yanga hawajaenda shule na hawajui lolote kuhusu mpira wanabweka Kama mbwa au nyani. Na Mimi nasisitiza maneno hayo
Uchebe alisema Simba haiwezi kuendelea kwakua kuna watu un educated, Ismail Aden Lage akiwa mweyekiti wa Simba alisema Simba ni Mbumbumbu mimi ninasema Simba bado ni mbumbumbu ila sasa wapo kwenye daraja la pekeyao ni next level .
 
Timu ya YANGA mimi nikiwa mwanachana inpaswa kuwa kali sana kiasi iwe vigumu kwa marefa na TFF kuihijumu. Ref hawezi kukataa goli mbilI au tatu zilizoingia. Na hawezi idhinisha goli la mpinzani lisiloingia. Kuna utatu mchafu kati ya SIMBA, TFF na ...........! No wonder Manara anatamba miaka 10 mfululizo wanachukua! Kwa TFFF hii ni ngumu yanga kuchukua kombe au kupata haki yeyote!
 
Huo mkataba wa miaka 2 ni JANJA JANJA YA GSM.baada ya kuona morrison ameanza kunyatiwa na simba.
Walimsainisha miezi 6 ili kuangalia kipaji chake..
Waambieni GSM watoe mikataba yao na Morrison tuone imesainishwa miaka mingapi?.
Na walimlipa kiasi gani?

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
Mikataba haianikwi hadharani Kama mitumba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom