Yanga yaingia mkataba wa Tsh Bilioni 34.8 na Azam Media

Mm kuna kitu sijaelewa; huo mkataba unahusu kufungua channel ya Tv yaani YANGA TV kama ilivo LIVERPOOL TV na kuiweka kwenye king'amuzi cha azam au ni Channel za azam kama UTV, Azam sports 1 HD n.k kurusha taarifa mbalimbali za Yanga?

Wenye kufahamu hili naomba ufafanuzi tafadhali.
Ni yanga tv, wao azam ndio watakua wanaandaa hicho kipindi na kukirusha. Mpaka sasa yanga wanakitengeneza wenyewe kisha wanapeleka file kwenye flash disk azam ili irushwe...
 
Ni yanga tv, wao azam ndio watakua wanaandaa hicho kipindi na kukirusha. Mpaka sasa yanga wanakitengeneza wenyewe kisha wanapeleka file kwenye flash disk azam ili irushwe...
Mkuu muwe mnafwatilia bas hivi vitu kabla kuandika kama hivi,,
..huo mkataba sio kuhusu yanga tv tu na sio kua yanga ananda anapeleka,,
Yanga kauza haki zote za matangazo ya television kwa azam tv,,
Azam tv sasa anahaki yakila liloihusu yanga kubrodcast,ni kutoa taarifa t nataka nifanye kitu flani kwa afisa habari wa team hata wakitaka kuanzisha reality show ya yanga,mikutano yote na waandishi wa habari,mahojiano na wachezaji ,mechi za kirafiki,mechi za kimataifa zote izo yanga hawez kuuza tena zote sasa n mali ya azam tv..
Yanga tv ni moja t ya package..
 
Tume ya Ushindani (FCC) imeanza uchunguzi wa mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu ya Simba ambao inawahusu wadaawa watano.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na FCC, wadaawa hao ni Simba Sports Club Holding Company Limited ambaye ni mdaawa wa kwanza, Mo Simba Company Limited (Mdaawa wa pili), Simba Sports Club Company Limited, Simba Sports Club na Mohammed Gulamabbas Hassanali Dewji.

Taarifa ya FCC imesema kuwa mdaawa wa tatu kwa kushirikiana na mdaawa wa kwanza, pili na tano walichukua mali na biashara za mdaawa wanne Tanzania Bara bila kuitaarifa tume hiyo kinyume na sheria ya ushindani kifungu cha 11 (2), 11 (6) (cha mwaka 2018) na kizingiti cha muunganiko wa makampuni cha mwaka 2017.

"Januari 6 mwaka huu, FCC ilifanya maamuzi kwa kutoa matokeo ya awali kuhusiana na tuhuma zinazowakabili wadaawa wote watano.

"Kitendo cha wadaawa wote watano kushindwa kuitaarifu FCC juu ya muunganiko huo wa makampuni kilisababisha kuinyima tume hiyo nafasi ya kutekeleza jukumu lake la kisheria la kufanya tathmini juu ya uhalali wa muunganiko huo unaotuhumiwa kutotaarifiwa kwake kwa mujibu wa sheria," imesema taarifa hiyo.

Tume hiyo pia imetoa nafasi mtu, kampuni, shirika au taasisi kuwasilisha pingamizi kwa kuwa na sababu za kuaminika kuwa muunganiko unaotuhumiwa kutekelezwa na wadaawa wote watano bila kutolewa taarifa kwa FCC kumeathiri au unaweza kuathiri maslahi yake.

Kwa upande wake, mwanasheria wa klabu ya Simba, Mhina M. Mhina alikiri kupokea taarifa hiyo kutoka FCC na wanaandaa taarifa rasmi.

“Tunaandaa taarifa kuhusiana na suala hilo, na msemaji wa klabu ataitangaza kwa mujibu wa utaratibu wetu,” alisema Mhina kwa njia ya simu.

Note: Issue imekwamia hapo FCC wamenusa arufu ya upigaji, MO ni Janja Janja sana, akili zenu mikia mzijuia wenyewe.
Mbona FCC, Bashungwa, Simba, MO washakaa kuweka sawa hili jambo?
 
Hivi Arnold Kashembe anasemaje kuhusu Simba kuuza Maudhui ya Simba TV? Mliosema Simba atapata deal kubwa zaidi ya Yanga kwa sababu Simba ina thamani kubwa kuzidi Yanga, hebu tuelewashane hapa. Ilikuwaje mkakubali 385M kwa mwaka halafu Yanga wapokee zaidi ya 200M kila mwezi? Huku kukiwa na ongezeko la 20M kwenye malipo ya kila mwezi kwa kila mwaka.

Huo ukubwa na weledi wa Simba uko wapi?
 
Klabu kongwe ya Young Africans Sports Club leo inaingia mkataba na Azam Media utakaogharimu jumla ya shilingi Bilioni 34.8 (Bilioni 41 with VAT). Mkataba huu utadumu kwa miaka kumi(10) na utafanyiwa marudio/maboresho baada ya miaka mitano.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Kaimu Katibu mkuu wa klabu ya Yanga Haji Mfikirwa alisema kuwa mkataba huu, utakua ni kichocheo kwa wadau wote wanaotaka kushirikiana na klabu hii ya Yanga. Kwa mfano, wawekezaji, makampuni ya matangazo n.k.

Kabla ya hapo, Katibu Mwenezi wa klabu ya Yanga Hassan Bumbuli alibainisha kuwa Yanga ndiyo klabu ambayo habari zake zinafuatiliwa sana hewani, magazetini (print) na kidijitali kwa ujumla. Akishukuru, CEO wa AZAM MEDIA ndugu Tido Mhando aliahidi kuboresha huduma ya matangazo inayotolewa na Azam Media. kalabu ya Yanga itakuwa inapokea jumla ya Shilingi 200 kwa mwezi, ambazo zitaongezeka kwa jumla ya milioni 20 kila mwaka hadi kufikia milioni 380 kwa mwezi.

Klabu ya Yanga itaweza kupokea hadi shilingi Bilioni 5.9 kwa mwaka kama Media rights ambapo kwa miaka kumi (10), watapokea kiasi cha Shilingi Bilioni 52.4 (jumlisha VAT).

Klabu nyingine pia zinakaribishwa kuingia mkataba na Azam Media.

My Take:
Simba (Vunjabei Sports Club) tunasubiri mkataba wenu.
Mkataba wenu uko wapi? Hayo maneno matupu tumeshawazoe. Kuanzia CAS na kuendelea.
 
Simba inategemea sana mitandao ya kijamii kama vile Instagram na Tweeter. Pia ina viongozi ambao ni kama celebrities, kwa mfano Haji Manara na Mo Dewji. Wana followers wengi, hata Barbara Gonzalez.

Ubovu wa hili kwenye negotiations za Media Partnership ni kuwa itabidi kurasa hizi ziache kuandika na kuonyesha baadhi ya matukio.
Yaani mimi kama AZAM nachukua hizi pages kama competition na itabidi unihakikishie kuwa utaacha kupost mambo ya Simba kabla ya kuniuliza na kuhakikisha hazitaleta migogoro.

This is Negative.
Pia Azam wataangalia siku Yanga ikicheza viewrship ipo vipi na siku Simba ikicheza viewership ipo vipi hasa kwenye TV.
Na mauzo ya Jezi pamoja na merchandise.

Halafu Simba nusu ya mapato yataenda kwa mtu binafsi, anaweza akatumia hizo hela kununua tambuu au kuwapa Simba. Hiyo ni juu yake.

Upende usipende, kwenye hili Yanga wamewapiga bao Simba.
Daaaaaah akili gani hizi utopolo mnazo, gawio kwenye mfumo wa hisa sio mapato ni faida. Uwezi ukanunua hisa Voda afu ukasema kila vocha inayouzwa utakua unachukua % zako. Hakuna kampuni ingesimama. Maana mwisho wa mwaka kila mtu anabaki na fito take
Utopolo acheni kujipotosha
 
Umekaa muda wote huo, ndiyo ukaamua kusema hilo.
 
Tume ya Ushindani (FCC) imeanza uchunguzi wa mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu ya Simba ambao inawahusu wadaawa watano.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na FCC, wadaawa hao ni Simba Sports Club Holding Company Limited ambaye ni mdaawa wa kwanza, Mo Simba Company Limited (Mdaawa wa pili), Simba Sports Club Company Limited, Simba Sports Club na Mohammed Gulamabbas Hassanali Dewji.

Taarifa ya FCC imesema kuwa mdaawa wa tatu kwa kushirikiana na mdaawa wa kwanza, pili na tano walichukua mali na biashara za mdaawa wanne Tanzania Bara bila kuitaarifa tume hiyo kinyume na sheria ya ushindani kifungu cha 11 (2), 11 (6) (cha mwaka 2018) na kizingiti cha muunganiko wa makampuni cha mwaka 2017.

"Januari 6 mwaka huu, FCC ilifanya maamuzi kwa kutoa matokeo ya awali kuhusiana na tuhuma zinazowakabili wadaawa wote watano.

"Kitendo cha wadaawa wote watano kushindwa kuitaarifu FCC juu ya muunganiko huo wa makampuni kilisababisha kuinyima tume hiyo nafasi ya kutekeleza jukumu lake la kisheria la kufanya tathmini juu ya uhalali wa muunganiko huo unaotuhumiwa kutotaarifiwa kwake kwa mujibu wa sheria," imesema taarifa hiyo.

Tume hiyo pia imetoa nafasi mtu, kampuni, shirika au taasisi kuwasilisha pingamizi kwa kuwa na sababu za kuaminika kuwa muunganiko unaotuhumiwa kutekelezwa na wadaawa wote watano bila kutolewa taarifa kwa FCC kumeathiri au unaweza kuathiri maslahi yake.

Kwa upande wake, mwanasheria wa klabu ya Simba, Mhina M. Mhina alikiri kupokea taarifa hiyo kutoka FCC na wanaandaa taarifa rasmi.

“Tunaandaa taarifa kuhusiana na suala hilo, na msemaji wa klabu ataitangaza kwa mujibu wa utaratibu wetu,” alisema Mhina kwa njia ya simu.

Note: Issue imekwamia hapo FCC wamenusa arufu ya upigaji, MO ni Janja Janja sana, akili zenu mikia mzijuia wenyewe.

Hivi inakuwaje mtu mzima tena pengine ni jinsia ya kiume unakuwa muongo kiasi hiki?
 
Mm kuna kitu sijaelewa; huo mkataba unahusu kufungua channel ya Tv yaani YANGA TV kama ilivo LIVERPOOL TV na kuiweka kwenye king'amuzi cha azam au ni Channel za azam kama UTV, Azam sports 1 HD n.k kurusha taarifa mbalimbali za Yanga?

Wenye kufahamu hili naomba ufafanuzi tafadhali.

Wameuza haki za Yanga tv ilioko yutubu
 
Soma soma ujue hisa ni nini, wenzenu tulipewa elimu mapema ndio maana tupo kimya
Elimu ipi hiyo?
Mimi nina hisa, nishanunua, nishauza.
Wewe inatakiwa useme kipi kilichozungumzwa ni upotoshaji. Halafu nitakujibu.
 
Back
Top Bottom