Yanga Yahaha Kusaka Kocha

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,141
13,215


Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi, amesema yupo tayari kuifundisha Yanga kama kocha msaidizi iwapo atahakikishiwa maslahi mazuri.


Mwambusi ambaye amefanikiwa kuipandisha Mbeya City msimu huu na kucheza Ligi Kuu Bara amekuwa akiwindwa na Yanga kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Fred Felix Minziro.



Mwambusi amesema taarifa hizo hajazipata rasmi kutoka kwa viongozi wa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu lakini iwapo watamfuata atawasilikiza na kuwatajia dau ambalo yeye anataka.
Alisema yeye kama kocha, kazi yake ni kufundisha mpira, hivyo yupo tayari kwenda popote iwapo tu atapata maslahi mazuri.
“Taarifa rasmi sijazipata lakini wakinifuata nitaongea nao kwa kuwa tayari watakuwa wameonyesha kuniheshimu kutokana na kazi ninayoifanya kukubalika kwao,” alisema Mwambusi
 
1.jpg
 
Hata hivyo, jana chanzo chetu kingine ndani ya Yanga kililiambia gazeti hili kuwa Bobby Williamson mzaliwa wa Glasgow, Scotland anakotoka aliyekuwa Kocha wa Man United, Sir Alex Ferguson, ndiye atakayerithi mikoba ya Brandts na kwamba uongozi ulifanya naye mazungumzo wakati wa michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika Desemba 12, mwaka huu jijini Nairobi, Kenya.

Kilisema Mscotland huyo atakuwa akisaidiwa na Boniface Mkwasa ambaye naye mazungumzo kati yake na Yanga yanaendelea, huku Felix Minziro siku zake za kuifundisha timu hiyo zikihesabika kabla ya kutupiwa virago.
 


Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi, amesema yupo tayari kuifundisha Yanga kama kocha msaidizi iwapo atahakikishiwa maslahi mazuri.


Mwambusi ambaye amefanikiwa kuipandisha Mbeya City msimu huu na kucheza Ligi Kuu Bara amekuwa akiwindwa na Yanga kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Fred Felix Minziro.



Mwambusi amesema taarifa hizo hajazipata rasmi kutoka kwa viongozi wa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu lakini iwapo watamfuata atawasilikiza na kuwatajia dau ambalo yeye anataka.
Alisema yeye kama kocha, kazi yake ni kufundisha mpira, hivyo yupo tayari kwenda popote iwapo tu atapata maslahi mazuri.
"Taarifa rasmi sijazipata lakini wakinifuata nitaongea nao kwa kuwa tayari watakuwa wameonyesha kuniheshimu kutokana na kazi ninayoifanya kukubalika kwao," alisema Mwambusi

Kwani huyu Mwambusi hata mkataba wowote na Mbeya City?
 
MEI 2004, kocha maarufu nchini Hispania, Jose Antonio Camacho alikabidhiwa jukumu la kuinoa klabu ya Real Madrid ya Hispania.

Ni kocha ambaye alipewa nafasi kubwa ya kuweka mambo sawa katika klabu hiyo hususan baada ya kutimuliwa kwa, Carlos Queiroz.

Hata hivyo katika kipindi kisichozidi miezi minne, Camacho alishindwa kuendelea na kibarua chake baada ya kutangaza kustaafu kuinoa timu hiyo.

Uamuzi wa Camacho uliwashangaza wengi lakini mwenyewe aliamua kuwa mkweli wa nini hasa kilichomfanya atimke baada ya muda mfupi; hakutaka kufa na tai shingoni.

Camacho aliweka bayana kwamba kilichomfanya atimke ni kushindwa kwake kuwaongoza wachezaji nyota wanaolipwa fedha nyingi wa Real Madrid.

Wachezaji hao maarufu Galacticos waliongozwa na kina Zinédine Zidane, Ronaldo, Luis Figo, Roberto Carlos, Raúl, David Beckham na wengineo.

Awali kulikuwa na fikra kwamba kipigo cha mabao 3-0 ambacho Madrid ilikipata kutoka Bayer 04 Leverkusen katika Ligi ya Mabingwa Ulaya ndicho kiini cha kocha huyo kuondoka lakini mwenyewe alisisitiza kuwa alishindwa kuwaongoza mastaa hao.

Baada ya hatua hiyo waandishi kadhaa wa Ulaya walichambua sifa za hao wanaoitwa Magalacticos kwamba ni kutaka kucheza nafasi wanayoipenda.

Kwamba hata kama kocha ataamua kumbadili mchezaji basi kwa Magalacticos jambo hilo ni gumu na zaidi ya hilo wakati wote wanataka kuwa juu ya kocha.

Tunadhani kilichomkuta Camacho katika Real Madrid kwa mbali kinaweza kufanana na alichokutana nacho Ernest Brandts katika Yanga.

Yanga inadaiwa kuwa na wachezaji mastaa au mafaza ambao baadhi yao walianza kuwadharau makocha na kujiona wao ni kila kitu.

Siku kadhaa kabla hata Brandts hajatimuliwa tayari alikuwa na mzozo na baadhi ya wachezaji, wengine wakipinga kutolewa katika mechi, wengine wakitaka kupangwa kila mechi.

 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom