YANGA yafikisha faili la tuhuma za alloyce komba makao makuu ya takukuru

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,249


Uongozi wa Yanga umefanikiwa kukabidhi barua na viambatanishi inavyoamini ni sehemu ya hujuma kwa uongozi huo chini ya Mwenyekiti Yusuf Manji.
Mkuu wa Habari na Mawasiliano ambaye ni Msemaji wa Yanga, Jerry Muro amekabidhi barua na viambatanishi zikiwemo sauti ambazo zinatuhumiwa kuwa za aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Alloyce Komba.
Muro alikabidhi vitu hivyo katika makao makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) Upanga jijini Dar es Salaam.

Takukuru wameahidi kuviingiza kwenye uchunguzi na kuvifanyia kazi na watatoa taarifa uchunguzi wao utakapokamilika
 
Safi
Maana walisema watafuatlia zile ishu za ligi daraja la kwanza halaf waka kausha tu mpaka now.

Kwenye hili ole wao walete uhuni
 
Usichezee Yanga Umoja wa Mataifa...Malinzi kanyoosha mikono juu maana mziki wetu si wa kitoto...Dj wetu ni Manji
 
Back
Top Bottom