Yanga yaanza mchakato wa kujenga uwanja

Nokla

JF-Expert Member
Aug 12, 2012
3,113
1,580
Klabu yanga imeingia mkataba na kampuni Beijing Construction Engeneering Group ya upembuzi akinifu kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa kisasa mitaa ya Jangwani.
Simba mpooo?
 
Story tu za Manji. itaishia kwenye makabrasha.. kesho tu mtasikia ooh ramani bado tunaisubiri toka China
 
Suala la mbu je itakuwaje? Cz jangwani ni wetland pale kuna kiwanda cha mbu

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Story?! Unafikiri Manji ni sawa na mzee wa mogadishu anayefeli kila analofanya?

- Kafeli kwa Mbuyu Twite
- Kafeli kujenga uwanja Bunju kama alivyojinadi, mpk leo anasubiri ramani toka Uturuki
- Alisema amemuuza Okwi Singapore kwa 1bn
- Kaiponza CCmizi Igunga kwa kwenda na bastola akidhani pale ni Mogadishu

Yaani kila kitu yeye ni kufeli tu. Alichoweza ni rufaa CAF mwaka ule na mkaishia kubamizwa na Waydad Casablanca
 
Jangwani mbu kwani tumekwambia tunatengeneza sehemu za kulala pale? Mbona usijiulize mnaishije na NZI wa sokoni?

Hii inashangaza kweli, yaani Club ya Mpira haina hata uwanja wa kupigia dana dana? Mkitaka kumjaribu mchezaji hadi msogeze meza nyuma ndio apige dana dana!!!!

Kaburu:
"Rage sogeza nyanyua miguu kidogo tuone kama kijana ana kontrooo.............."

Rage: "Ok OK, dakika moja tafadhali, ngoja nimalizie hii barua ya rufaa niitume CUF sasa hivi.....sasa hivi....loh, mbona inzi wengi hivi leo, huko sokoni hawajapiga dawa nini?"

Kaburu: "Hamna shaka mkuu" kwa dogo "star we tulia kidogo, sasa hivi tutatoa meza hizi, panatosha tu hapa usijali"

Rage:
"Uuukey! Basi mi nipo chini hapo napata kahawa, mkimaliza utanishtua nije kuwasainia wale jamaa fedha zao"

Kaburu:
"Sawa mkuu, halafu na Bi Fatma wa Zenj unajua bado anadai ile bili ya maharage tuliyokula tulipoenda kwenye kombe la Maulidi"

Rage:
"Sawaaa, tutaongea mida." (Anatoka huku akijisemea mwenyewe 'Hili jamaa sijui samtaim vipi, sasa mambo ya maharage ndio asema mbele ya mgeni. Hivi hivi siku moja atakuja kuropoka kuwa tumetafuna rambi rambi za Mafisango..ah!')
 
mbu wanahusika vipi???
kwani unajengwa ukumbi wa harusi au guest house?
 
Klabu yanga imeingia mkataba na kampuni Beijing Construction Engeneering Group ya upembuzi akinifu kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa kisasa mitaa ya Jangwani.
Simba mpooo?

Tukiacha porojo za hao wapuuzi wachache hapo juu, uongozi wa Yanga Afrika kwa hatua waliyofikia ingawa kuna watu wanabeza.
Cha mno cha kushukuru ni kuwa uongozi haujadanganya umma kuhusu hatua waliyopo, ya upembuzi yakinifu... Ingekuwa sivyo tungeambiwa wale wakandarasi wanakuja kuporomosha uwanja.
Maoni yangu kuhusu huu upembuzi yakinifu yanakinzana kidogo na malengo ya Yanga. Eneo la kaunda ni dogo sana kujenga uwanja wa kuchezea kwa idadi waliyoikusudia huku ukiwa na miundombinu ya msingi (vyumba vya wachezaji, gym, zahanati, media room na kadhalika). Parking pia ni suala muhimu kwa uwanja pamoja na accesibility, yaani kuhakikisha uwanja unafikika toka pande zote kwa barabara.
Ingekuwa kipindi kile kabla ya mradi wa mabasi yaendayo kasi, Yanga ingeweza ku-loby kwa serikali uwanja ukajengwa kwenye viwanja vya Jangwani.
 
chezea Yanga wewe mtaisoma wanamsimbazi aka wazee wa bastola.!
 
Manispaa inawaona mnavyojichanganya pale bondeni. Jengeni tu, utabomolewa na manispaa siku ya uzinduzi
 
Story?! Unafikiri Manji ni sawa na mzee wa mogadishu anayefeli kila analofanya?

- Kafeli kwa Mbuyu Twite
- Kafeli kujenga uwanja Bunju kama alivyojinadi, mpk leo anasubiri ramani toka Uturuki
- Alisema amemuuza Okwi Singapore kwa 1bn
- Kaiponza CCmizi Igunga kwa kwenda na bastola akidhani pale ni Mogadishu

Yaani kila kitu yeye ni kufeli tu. Alichoweza ni rufaa CAF mwaka ule na mkaishia kubamizwa na Waydad Casablanca

Kevin Yondani je, msomali alifaulu?
 
Jangwani mbu kwani tumekwambia tunatengeneza sehemu za kulala pale? Mbona usijiulize mnaishije na NZI wa sokoni?

Hii inashangaza kweli, yaani Club ya Mpira haina hata uwanja wa kupigia dana dana? Mkitaka kumjaribu mchezaji hadi msogeze meza nyuma ndio apige dana dana!!!!

Kaburu:
"Rage sogeza nyanyua miguu kidogo tuone kama kijana ana kontrooo.............."

Rage: "Ok OK, dakika moja tafadhali, ngoja nimalizie hii barua ya rufaa niitume CUF sasa hivi.....sasa hivi....loh, mbona inzi wengi hivi leo, huko sokoni hawajapiga dawa nini?"

Kaburu: "Hamna shaka mkuu" kwa dogo "star we tulia kidogo, sasa hivi tutatoa meza hizi, panatosha tu hapa usijali"

Rage:
"Uuukey! Basi mi nipo chini hapo napata kahawa, mkimaliza utanishtua nije kuwasainia wale jamaa fedha zao"

Kaburu:
"Sawa mkuu, halafu na Bi Fatma wa Zenj unajua bado anadai ile bili ya maharage tuliyokula tulipoenda kwenye kombe la Maulidi"

Rage:
"Sawaaa, tutaongea mida." (Anatoka huku akijisemea mwenyewe 'Hili jamaa sijui samtaim vipi, sasa mambo ya maharage ndio asema mbele ya mgeni. Hivi hivi siku moja atakuja kuropoka kuwa tumetafuna rambi rambi za Mafisango..ah!')

Haaaaaaaa! Kumbe!
 
Yanga wanaweza kufanikiwa katika ujenzi wa uwanja huu. Wameanza na feasibility study ambayo itaonesha mradi huu utekelezwe au la. Simba wameshindwa kuendelea na mradi wao kwa vile walianza na kumpata mkandarasi feki kutoka Uturuki, hii ni hatua ya juu sana. Manji na viongozi wenzako songeni mbele ili tofauti baina yenu na Rage na wenzake ionekane wazi kwa kila mwenye akili timamu.
 
YANGA NI TIMU YA KIZAZI KIPYA ,ITS A TEAM OF NEW GENERATION ,ITS A 21st CENTURY TEAM.HONGERA KWA WANAYANGA WOTE.
 
Akina Thomaso tupo, hatuamini hadi ujenzi uanze, na sio upembuzi yakinifu. Unapembua nini wakati eneo hata kipofu anaona halitoshi kujenda uwanja wa kubeba watu 40,000 ?

Viongozi wa mpira Tanzania ni wababaishaji kupindukia, wanapenda kuwaza makubwa wakati madogo tu shida. Kwa mafano hadi sasa Yanga wanakodi uwanja wa mazoezi, wanashindwaje kutengeneza uwanja wa mazoezi? Simba nao ndio usiseme, sasa hivi hawataki hata kuuzungumizia uwanja wa Uturuki.

Viongozi wameshindwa kuboresha mabenchi ya ufundi, timu za vijana hazina mpangilio unaoeleweka, ni ujanja ujanja kila siku.

Anyway, yangu macho japo naamini Manji uwezo anao akitia nia hakika kuna kitu kizuri kinaweza kutokea.
 
Yanga wanaweza kufanikiwa katika ujenzi wa uwanja huu. Wameanza na feasibility study ambayo itaonesha mradi huu utekelezwe au la. Simba wameshindwa kuendelea na mradi wao kwa vile walianza na kumpata mkandarasi feki kutoka Uturuki, hii ni hatua ya juu sana. Manji na viongozi wenzako songeni mbele ili tofauti baina yenu na Rage na wenzake ionekane wazi kwa kila mwenye akili timamu.

Makoye Matale pamoja sana Mkuu wangu!!!!!!!
 
Manispaa inawaona mnavyojichanganya pale bondeni. Jengeni tu, utabomolewa na manispaa siku ya uzinduzi

Ukimuona Mtoto anamcharaza Baba yake Bakora ujue amebaini huyo si Baba yake,hiyo haitatokea,tumia kichwa kupembua mambo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom