Yanga yaachana Rasmi na Kelvin Yondan na Juma Abdul

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,451
29,128
Klabu ya Soka ya Yanga imeamua kuachana rasmi na Walinzi wao Kelvin Yondan na Juma Abdul Jafary baada ya kushindwa kufikia maafikiano.

Screenshot_20200807-193535.png
 
Kuanza upya sio ujinga....Yanga(timu ya wananchi) ni kubwa kuliko mchezaji

Wananchi tumebariki haya mabadiliko wavuta bangi na wahuni lazima tuwaondoe kikosini
 
Kelvin na Juma walishapita muda wao bora. Yondani katusumbua sana msimu miwili iliyopita kuzima simu na utovu mwingine wa nidhamu. Mwishoni alikuwa hana namba kwenye kikosi kile 'kibovu'. Juma Abdul pia alisusa mwaka jana karibu nusu ya msimu! Tulichofanya kuwapa mkataba ilikuwa ni huruma tu lakini wasingekuwa na mchango wowote! Pia wachezaji wakifikia umri huu wanawaza maisha "wanaweza fanya hujuma yeyote " YANGA IMESHAWAHI KUACHA TIMU MZIMA MARA MBILI" Nani anaikumbuka Yanga Yoso? Waliachwa wakina Saidi Mwamba na Mohamedi Hussein! TUACHENI TUJENGE TIMU YETU! Ikiwa tunakosea si ni vizuri kwenu mshinde goli 10?
 
Kelvin na Juma walishapita muda wao bora. Yondani katusumbua sana msimu miwili iliyopita kupima simu na utovu mwingine wa nidhamu. Mwishoni alikuwa hana namba kwenye kikosi kile 'kibovu'. Juma Abdul pia alisusa mwaka jana karibu nusu ya msimu! Tulichofanya kuwapa mkataba ilikuwa ni huruma tu lakini wasingekuwa na mchango wowote! Pia wachezaji wakifikia umri huu wanawaza maisha "wanaweza fanya hujuma yeyote " YANGA IMESHAWAHI KUACHA TIMU MZIMA MARA MBILI" Nani anaikumbuka Yanga Yoso? Waliachwa wakina Saidi Mwamba na Mohamedi Hussein! TUACHHENI TUJENGE TIMU YETU! Ikiwa tunakosea si ni vizuri kwenu mshinde goli 10?
Truth Matters matterJuma Abdul ndio mchezaji mwenye assist nyingi kuliko mchezaji yoyote pale japo mlikuwa na strikers butu hata mwaka Jana pia aliongoza kwa assist.Juma Abdul Ni beki mzuri Sana na wakisasa anaweza kupanda na kushuka umahiri wake upo kwenye kupiga Sana cross zenye macho( Kumwaga maji) watu Kama ngoma kipindi kile na Tabwe walimfaidi Sana Juma Abdul.Kumuacha Yondani na jafari hapo wapo sahihi cos viwango vyao vimeshuka ila sio kumuacha mtu Kama Juma Abdul ambaye kiwango chake kipo vile vile angalau Yanga wangemtafutia backup au mchezaji zaidi ya Juma abdul ila sizani hili litatokea Yanga wamefanya makosa Sana kumuacha huyu Mwamba.
 
Ukweli Juma Abdul ni Beki mzuri wa kulia, krosi zake zimesaidia sana Yanga (assist), ila akija Kwetu atasota benchi, tunae Kapombe
Waliomuacha ndio wajuao namna gani wataziba pengo lake maana si kana kwamba hawajui uwezo wake. Mpira bila nidhamu wakati mwingine ni usumbufu. Mfano timu ina mechi mchezaji haonekani hatoi sababu mbaya zaidi anazima simu yake unategemea nini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom