'Yanga WhatApp Makao Makuu' niombeni Radhi na pia Muuombe Radhi Mtandao wa JamiiForums kwa Kukopi 'Uchambuzi' wangu pasipo kutoa 'Credit' kote kote

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,546
108,876
Wiki mbili zilizopita hapa hapa Uwanja wangu wa 'Kujidai' katika huu Mtandao wangu pendwa kabisa wa JamiiForums nilikuja na 'Uchambuzi' wangu wa Kuwahusu Wachezaji Wawili wa Wapinzani wangu (wetu) ambao ni Yanga SC juu ya Wachezaji Wao wawili mahiri Mshambuliaji Michael Sarpong na Kiungo Mshambuliaji Tuisila Kisinda.

Cha Kushangaza kabisa na tena hata bila 'Aibu' leo na Jioni hii hii katika Ukurasa wa Yanga Whatssap Makao Makuu kwa kudhani kuwa GENTAMYCINE huwa sifuatilii Mambo ya Yanga SC na mengineyo ya Kimichezo nchini wameamua 'Kukopi' ule 'Uchambuzi' wangu wote vile vile kama ulivyo na aliyeuweka Kujifanya kuwa 'Madini' yote yale kayatoa Yeye.

Hata hivyo sina shida sana na 'Kukopiwa' kwa 'Uchambuzi' wangu kwani hawa siyo wa Kwanza kwakuwa 'Mabandiko' yangu mengi tu GENTAMYCINE ninayokuwa 'nayaandika' hapa JamiiForums kuhusu 'Masuala' mbalimbali huwa 'yanakopiwa' na Watu Kujifanya wameandika Wao japo wapo Wastaarabu kama Azam TV na Eatv hadi Redio One huwa 'wakinikopi' hutaja ID yangu na huu Mtandao.

Kilio changu Kikubwa hapa ni kwamba nawaomba sana tena 'chonde chonde' kabisa wale wote ambao huwa wanapenda 'Kunikopi' yale 'Mabandiko' basi wawe wanafanya 'Acknowledging' au 'Credit the Source' kwa kuanzia Kwangu kama GENTAMYCINE na kwa Mtandao wa JamiiForums. Kuwasilisha 'Kitu' cha Mtu halafu humpi 'Heshima' yake ni Kumvunja sana Moyo.
 
Back
Top Bottom