Yanga wanyatia pesa za Azam walizosusa

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,141
13,215
KATIKA hali inayoashiria ni kuyumba kiuchumi, klabu ya Yanga imeandika barua Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikitaka ilipwe malimbikizo ya fedha zake za haki ya matangazo ya Televisheni ya Azam TV, Sh. Milioni 372.

Kwa ujumla Yanga inataka ilipwe Sh. Milioni 422 pamoja na Sh. Milioni 50 za kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Yanga haikupewa zawadi yake ya kutwaa ubingwa wa Kombe la ASFC Mei mwaka huu ikiwafunga Azam FC 3-0 katika fainali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga pia ilisusa kuchukua mgawo wa haki za matangazo ya Televisheni kwa miaka yote mitatu baada ya kutoridhia mkataba wa TFF na Azam TV.
10.jpg

Lakini katika hali ya kustaajabisha ghafla Yanga wameibua na kuiandikia barua bodi ya Ligi ya TFF kuomba malimbikizo ya fedha zake hizo, Sh. Milioni 372.

Habari za ndani ambazo Bin Zubeiry Sports - Online imezipata zimesema kwamba Bodi ya Ligi baada ya kupata barua hiyo ya Yanga waliwajibu wakiitaka klabu hiyo kwanza iandike barua ya kuutambua na kuukubali mkataba huo wa Azam TV ndipo utaratibu wa malipo yao ufanyike.

Bodi ya Ligi bado inasubiri sasa barua kutoka Yanga wakiikubali Azam TV kurusha matangazo ya mechi za Ligi Kuu ili utaratibu wa malipo yao uanze.
Na hatua ya Yanga kudai fedha hizo inakuja katika kipindi ambacho kumekuwa na matatizo hadi ya kulipa mishahara ya wachezaji.

Inadaiwa wachezaji wa Yanga walipitisha miezi mitatu bila kulipwa mishahara kati ya Julai na Septemba na hiyo inatajwa kama sababu ya timu kufanya vibaya kwenye mechi za Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika.
Aidha, wiki iliyopita wachezaji wa Yanga waligoma kwa simu mbili kufanya mazoezi, Jumatatu na Jumanne wakishinikiza kulipwa mishahara yao ya Novemba.

Kwa ujumla hali ya kiuchumi si njema ndani ya Yanga tangu kuondoka kwa waliokuwa wadhamini wakuu, kampuni ya Bia Tanzania (TBL) waliokuwa wakiidhamini klabu hiyo pamoja na mahasimu, Simba kupitia bia ya Kilimanjaro.
Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit alipotafutwa katika simu yake alisema hawezi kuzungumza chochote kwa leo kwa kuwa alikuwa nje ya ofisi.

“Jamani hata siku za sikukuu pia mnatupigia simu?”alihoji Baraka na baada ya kuuliwa kuhusu klabu kuiandikia barua Bodi ya Ligi ya TFF kudai malimbikizo ya fedha za Azam TV, alisema; “We nani kakuambia, kwanza siwezi kuzungumza chochote nipo nje ya ofisi, nipigie kesho nikiwa ofisini,”alisema.
15665735_363497684011101_5618886366820352683_n.jpg

Kuna tetesi lakini za uhakika kwamba hatimaye Yanga wamepewa mzigo ulokua ukielekea kuvunda kule Azam baaada ya ukata wa majuma kadhaa

Pesa hizo zimelipwa baada ya kuzisotea kwani awali walizisusa na sasa hakuna jinsi zaidi ya kuzirudia na kulazimika kuandika barua kupitia TFF ili kupea na hatimaye wamekabidhiwa

hata hivyo bado wingu la ukata linazidi kutanda kwani wana madeni makubwa toka kwa wachezaji waliovunjiwa mikataba yao akina Tegete, Wisdom Ndlovu na Steven Marashi licha ya deni la CAF baada ya Yanga kuruhusu mashabiki kuingia bure
 
BMT walipeni mishahara wachezaji wa Yanga.... Nachukia mizee ukoloni tuu... Ndio maana masikini wa kutupwa
 
Vilabu vyetu vya Tanzania sijui kama vilisha wahi kujiendesha kwa faida.
havina vyanzo vya mapato vya kujiendesha vyenyewe pasipo kumtegemea mtu.
Tanzania Club zinavunja mikataba na wachezaji pasipo sababu za msingi. hata wenzetu walio endelea wana iyeshimu mikataba sana ila sio Tanzania.
Kama mchezaji humuhitaji kwa nini usimuweke sokoni anunuliwe na na timu nyingine. club nayo ipate hela ya mauzo yake kuliko unavunja mkataba alafu unamlipa wewe mchezaji na anasajiliwa na timu nyingine bila gharama yoyote.

Ndiyo mana wenzetu Ulaya kama mchezaji hayupo kwenye mipango ya kocha huwa wanamuweka sokoni na sio kuvunja mkataba.

Soka letu linaendeshwa na watu wasio jua mpira haswa kwenye swala la uwongozi wa club. Wengi wameishia form four na kucheza mpira labda miaka 4 basi anatosha kuendesha timu.

SIMBA na Yanga ni club kubwa sana lakini bado kuto kuendelea kwa club hizi ndiko kutapelejea kudhofisha ligi na timu zingine kuto kuendelea mbele

Natamani sana wajitokeze matajiri wanunue timu kama Mtibwa sugar, kagera sugar au stend Waweke uwekezaji mzuri tuone kama na watalamu wawepo tuone kama hizo timu kubwa hazitabadilika. Viongozi wengi wapo pale kwa ajili ya kujijali tu wao wenyewe na sio kwa mapenzi ya club...
 
Simba na Yanga ndio zinazoua mpira wa Tanzania.
 
Haya wezee wa Yanga wakiongozwa na Akili + BMT tulipieni mishahara, yanga yetu ooih tumeitoa mbali ..mkono mtupu haulambwi, .. All anti Manjis are enemies of progress for our football
 
Simba na Yanga ndio zinazoua mpira wa Tanzania.
Huu mpira wacheni tushangilie tu. ila kimataifa tutabaki kusindikiza tu.
na soka halita endelea
Kocha wa Timu ya Taifa akiwa vizuri achague wachezaji kutoka vilabu vingine.
Wachezaji wengi wana amini kucheza Simba au Yanga ndiyo njia pekee ya kwenda kucheza timu ya taifa mwisho wa siku wakienda wana sugua benchi. Ndoto zao zinakufa
 
Walisahau Kuwa Wenye Akili Walishasema Kwamba "A Beggar Can't Be a Chooser"!
Vyura FC munaanza Kuisoma Namba Taratibu Huku Mnyama Akizidi Kutakata......
 
Hii ndo shida, ya club za wazee na wanachama, haya wazee Wa yanga tangu Uhuru lipieni gharama za timu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom