Yanga vs Toto; Simba vs Majimaji - ni mwisho mtamu!

Kama Vigezo ni mechi za mzunguko wa kwanza ulioyozikutanisha timu hizo unaweza kutoa Angalizo.
Tarehe 07 11 2011
Yanga-2 Toto-0 Uwanja wa uhuru, DSM.
Majimaji-1 Simba-2 Uwanja wa majimaji,Songea RVM.
Hapo Simba wakishinda hata 5-0 Ni sawa kwani kama walishinda ugenini idadi hiyo ya mabao tena kipindi hicho ushindani wa ligi ungali ulikuwa mbichi na majimaji hawakuwa katika nafasi mbaya iweje hiyo keshokutwa wameshakuwa na uhakika mwakani hawapo katika VPL Wasipigwe?. Upande wa Mechi ya Toto Walifungwa 0-2 Ugenini na Marudiano wapo CCM Kirumba, Nyumbani kimtazamo wakifungwa zaidi bao. 0-1 inawezekana ila matokeo halisi washinde wao bao 1-0 hata 2-1 au sare yeyote ile itakuwa fair. Kumbukumbu zangu 1987 timu 8 zilipanga matokeo TFF Wakati huo FAT Waliyafuta matokeo ya mechi zote Nne na hivyo basi Biashara fc ya mwanza ilishushwa Baada ya kubebana na RTC Kigoma Kurugenzi Dodoma wakashushwa baada ya kupanga matokeo na Coast union halafu matokeo ya Nyota nyekundu dhidi Tukuyu stars na Reli morogoro dhidi ya Ushirika moshi yakafutwa. Sasa tuangalie TFF wana meno ya kuweza kuyafuta matokeo ya Timu kubwa hizi Yanga na Simba iwapo itabainika zimecheza mchezo mchafu ikiwa Yanga watashinda goli 5-0.Simba wawo italazimika kushinda 8-0 ili watete ubingwa wao huku ikitambua kuwa Mwisho wa siku TFF wakiyafuta matokeo yao yote na ya Yanga basi bila shaka Mpinzani wake anabakia kileleni hivyo kombe litatua Jangwani. Simba walichokosea ni ku concentrate zaidi katika mechi ya TP Mazembe huku wakivurunda kwenye ligi Sare mechi mbili dhidi ya Kagera na JKT walikuwa tayari wameshapoteza pointi Nne leo wangekwisha tangazwa mabingwa mara ya pili mfululizo walishatjuwa kuwa TP Mazembe si SIZE yao ila walitaka tu kuwadanganya wasiodanganyika.

Mtazamo wako ndugu upo kimahesabu zaidi kuliko kisoka.
Simba wakiwa nyumbani walipigwa 4-0 na Mufurila ya Zambia
Wakiwa ugenini wakashinda 5-0

Yanga wakiwa nyumbani walipata sare na Highlander ya Zimbabwe
Wakiwa ugenini wakashinda 2 - 0

Schalke 04 ya Ujerumani wakiwa ugenini wakaisigina Inter Milan 5-2
Kwa hiyo ktk soka, uwanja wa nyumbani au ugenini unaweza usisaidie kukupa ushindi
 
Wakifunga magoli mengi tff itawapiga rungu..

Toto 0 - 4 yanga
simba 3 - 1 majimaji

matokeo yakiwa tofauti ya hayo yataleta shida sana...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom