Yanga SC wamefanikiwa 100% kwa hii 'Unbeaten Record' yao na 'Propaganda' madhubuti

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,542
108,856
Akina GENTAMYCINE tukiwa tunasema kuwa kwa sasa Klabu ya Yanga imejipanga vyema hasa kwa upande wa Propaganda muwe mnaelewa/mnatuelewa.

Ukweli ni kwamba Yanga SC siyo wapumbavu kama labda ambavyo tunaweza kudhani kwa wao kuikuza hii 'Unbeaten Record' yao katika Ligi Kuu ya NBC nchini Tanzania.

Yanga SC ambao GENTAMYCINE kama mwamba na mbobezi wa propaganda nawapongeza kwa hili, kwani ili kuonyesha kuwa wamedhamiria lengo lao litimie, hivi karibuni walikuja na kampeni ya kumpongeza Kocha wao Mkuu Nabi dakika ya 43 na kesho wakiwa pale CCM Kirumba Mwanza wakicheza na Geita Gold FC ikifika dakika ya 44 watasimama safari hii kuwapongeza wachezaji wao.

Ukweli ni kwamba kwa Yanga SC kuikuza hii 'Unbeaten Record' yao wameshafanikiwa kwa mafanikio ya kimatokeo ya uwanjani. Kwani tayari hata waamuzi wote watakaowachezesha katika mechi zao za Ligi Kuu wameshaingiwa na uwoga na wao hii 'Unbeaten Record' ipo vichwani mwao.

Hivyo iwe isiwe hawatathubutu kuruhusu Yanga SC ipoteze mechi (ifungwe) mbele yao na watakachokifanya ni kuhakikisha wanaibeba ishinde na kama ikishindikana basi watoke (itoke) sare/suluhu, ila siyo kufungwa ili kujiepusha na lawama ya kuharibu rekodi yao.

Kuna siku hapa hapa GENTAMYCINE nilisema kuwa, Klabu ya Simba imelala na imepwaya mno katika kufanya propaganda na hakina kitengo thabiti cha propaganda (hasa kwa mpira wa Tanzania), lakini kama kawaida sikueleweka. Ila ipo siku tu mtakuwa mnanielewa na kuungana nami kifikra, kimawazo na kimtizamo.

Kwa ambao mnadhani na kujidanganya kuwa ndani ya hii NBC Premier League Klabu ya Yanga itafungwa (itapoteza), mnapoteza muda. Ila kushindwa kwa Yanga SC ni kutoka tu sare/suluhu na kama ni kufungwa basi watafungwa katika Michuano ya CAFCC (ya kimataifa) ambayo huko propaganda yake bado hawajaiwezea/hawajaimudu.

Ila hata huko pia wakipaweza watakuja kuwa imara kuliko hata Simba SC ambao wana uzoefu mkubwa huko (kimataifa).
 
Kwahiyo kumbe tunakubaliana Yanga inapata matokeo kupitia propaganda na sio uwezo ktk pitch?, basi tunasafari ndefu sana kisoka hadi tuje kufikia level ya watani zetu Simba.
 
Na Siku zako pia za Kudumu na Ugonjwa wa Akili mkubwa huo ( huu ) ulionao hadi leo huwa unazikumbuka vile vile?
, Genta kama Genta
1664834935810.jpg
 
Back
Top Bottom