Yanga SC inabebwa, kwa nini Azam wacheze kiporo chao leo ila Yanga hawajacheza?

barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
32,375
29,732
Habari zenu!
Hii ligi ya VPL inaonyesha inaendeshwa kimagumashi tu. Inakuaje Azam Fc ina viporo kama Yanga, jumamosi wamecheza Mwanza na Yanga walicheza TENA dar es salaam ila leo jumatano Azam wamecheza tena kupunguza kiporo chao ila Yanga hawajacheza. Hii ni wazi kuwa Yanga inabebwa.
Azam wanatakiwa wacheze tena jumapili/ jumapili tena mechi ya kimataifa, Yanga pia wanatakiwa wacheze jumamosi/ jumapili mechi ya kimataifa, KWA NINI AZAM RATIBA YAO IMESEMA WACHEZE LEO NA YANGA WASICHEZE AU KWA NINI AZAM NAO RATIBA YAO INGESEMA WASICHEZE LEO?
Huu upuuzi wa kubebana ni moja ya vigingi vinavyotuzuia kusonga mbele ktk soka.
Asanteni.

P.s: Azam Fc leo wamedroo na Ndanda Fc, waliongoza kwa bao mbili bila kipindi cha kwanza, Ndanda wakasawazisha zote.
Goli za azam: Singano na kavumbagu.
Goli za ndanda: Atupele kwa penati na Aggrey Morris' own goal.
 
Kila mara huwa nasema bila kuing'oa Yanga hapo juu,tutaendelea kichwa cha mwendawazimu.Yanga inaua mpira wa Tanzania,angalia kadi nyekundu zonavyotolewa ovyo pindi yanga akicheza na timu pinzani.
 
Yanga alistahili kulala dhidi ya kagera,kwakua Yanga ndiyo timu ya chama.Hivyo kuchakachia ni tabia yao ya asili.
 
Hizi figisu figisu hizi ndizo zinauwa kandanda letu!
Hii sasa haikubaliki
 
Yanga kubebwa na tff & ccm siyo siri na haijaanza leo. hata jengo lao walijengewa/walipewa bure na Karume
 
Yanga ikishinda imebebwa, ikishindwa poa. walaumuni wanaowafunga, msiilaumu yanga
Yanga inabebwa, KWA NINI LEO HAWAJACHEZA VIPORO VYAO ILHALI AZAM WAMECHEZA?
Mnachotakiwa kujivunia ni mnajua kumshikilia anayewabeba.
 
Umesahau Azam badala ya kucheza ligi waliomba ruhusa kwenda kucheza bonanza nje ya nchi wakati wenzao ligi inaendelea ?
Kwa hiyo na wao wanabebwa?
Kwani Yanga na Azam wana viporo tofauti? Wote ni vilikuwa viwili??
 
TFF walitoa ruhusa viporo vya leo cha Azam na Yanga vitachezwa mbele baada ya mechi zao za kimataifa za wikiendi.
Lakini Azam waliamua kucheza leo kwa sababu taarifa yao ya kuomba mechi hii ya leo na ndanda kuchelewa kupewa majibu. Wamefanya hasira na imekula kwao. Hakuna aliyebebwa Yanga waliamua kutocheza leo ili wajiandae vzr dhidi ya Al Ahly.
 
Kwa hiyo na wao wanabebwa?
Kwani Yanga na Azam wana viporo tofauti? Wote ni vilikuwa viwili??
Kuna tatizo la upangaji wa ratiba ya ligi ya bongo,haiwezekani ligi ina timu 16 inachezwa mwaka mzima halafu timu icheze mechi 4 ndani ya siku 10.Baada ya Azam kufungwa mechi zao ndio mnasema Yanga anabebebwa wakati ule alivyoenda bonanza na kurudi akashinda viporo vyao walikaa kimya
 
Kila mara huwa nasema bila kuing'oa Yanga hapo juu,tutaendelea kichwa cha mwendawazimu.Yanga inaua mpira wa Tanzania,angalia kadi nyekundu zonavyotolewa ovyo pindi yanga akicheza na timu pinzani.
Haya ni mawazo ya watu wa kwenye vijiwe vya kahawa.
 
KILE KIPORO CHA JUZI CHA NDALA A.K.A VYURA FC KILICHACHA PIA ILA MWAMUZI AKAAMUA KUKILA YEYE KWA NIABA YA VYURA FC,

VYURA WANABEBWA NA TFF,

ILA AZAMU NA WENYEWE WAMEANZA KUWA MIDOMO MICHAFU KAMA YA MSEMA OVYO WA VYURA FC ACHA WALIWE!
 
Yanga ya Malinnzi hivyo viongozi wa TFF.
Sasa hyo ligi gani eti kila mwenzio akicheza na we ucheze hebu toa mfano wa jambo hili kufanyika kwa wenzetu maana cjawai sikia na leicester anawazidi mpk mechi tatu
 
Watu hamuishi malalamiko juzi tu mmesema azam wanabebwa leo yanga wanabebwa!! Nyambaf
 
Back
Top Bottom