Yanga SC 2-1 Namungo FC | NBC Premier League | Benjamin Mkapa Stadium

Protect

Member
Apr 4, 2020
94
299
FRCrv0YXoAIXt6C.jpg
Leo tarehe 23/04/2022 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, vinara wa ligi Dar Young Africans almaarufu kama Yanga watashuka dimbani kuikaribisha timu ya Namungo FC kwenye mechi la NBC Premier League

Nitakuwa nawe kukuletea yatakayojiri kwenye uwanja huo, mpira utaanza saa moja kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

=====

00' Kabumbu linaanza hapa dimba la Mkapa

01' Feisal Salum anaachia mkwaju kutoka nje ya 18 na unaenda pembeni kidogo mwa lango
03' Feisal Salum tena, almanusura aandike bao la kwanza
04' Kichuya anaangushwa nje kidogo 18 akielekea lango la Yanga, Molinga anashindwa kuutumia vyema mpira wa adhabu ndogo
09' Yanga wanacheza kwa kasi na kulishambulia lango la Namungo
15' Presha ni kubwa Yanga wanatafuta bao la mapema, Fei Toto amekosa nafasi mbili za wazi

17' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Yanga wanapata bao, Fiston Mayele anafunga baada ya beki kuukosa mpira.
23' Mchezo unaendelea kwa kasi, inaonekana Yanga wanataka kumaliza biashara mapema
25' Namungo nao wanasogea karibu na lango la Yanga, upinzani ni mkali na mchezo umechangamka
30' Yanga wanapata kona, inapigwa lakini haina madhara
31' Kipa wa Namungo yupo chini, inaonekana ana majeraha. Mchezo umesimama anatibiwa.

33' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Kichuya anaisawazishia Namungo kwa shuti kali kutoka nje ya eneo la boksi
Kocha Msaidizi wa Namungo, Julio anaenda kushangilia bao mbele ya mashabiki wa Yanga
37' Mchezo umebalansi, timu zote zinashambuliana kwa zamu.
38' Kichuya ambaye anaonekana kuwa hatari kwa Yanga anadhibitiwa na walinzi kwa umakini.

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
39' Feisal Toto anaipatia Yanga bao la pili akimalizia mpira uliopigwa kwa krosi.
43' Kadi za njano zimekuwa nyingi kwa wachezaji wa Namungo
45' Yanga wanashambulia lakini walinzi wa Namungo wanakuwa makini.

MAPUMZIKO

Kipindi cha pili kimeanza.
46' Yanga wanafika langoni kwa Namungo lakini wanaotea.
50' Kasi ya mchezo imepungua kiasi
55' Mwamuzi anawaonya baadhi ya wachezaji wa Namungo ambao wanacheza faulo mara kadhaa.
60' Yanga wanafanya shambulizi la nguvu lakini wanashindwa kutumia nafasi vizuri.
65' Yanga wanaongeza presha sasa kutafuta bao la tatu, wanafika langoni mara kadhaa lakini wanakosa utulivu
70' Kasi ya Namungo imepungua kiasi na wanaruhusu mashambulizi langoni kwao.
77' Yanga wanaendelea kufanya mashambulizi na kutawala mchezo.
78' Namungo wanarejesha majibu kwa kufika langoni kwa Yanga lakini wanashindwa kutumia nafasi.
85' Namungo wanajaribu kutafuta bao la kusawazisha lakini mambo ni magumu kwao
87' Timu zinashambuliana kwa zamu.
90' Zinaogezwa dakika 3 za nyongeza.

FULL TIME: Yanga inapata ushindi wa mabao 2-1.

FRC1q5QXMAY6KzA.jpg


Screenshot_20220423-163248_Instagram.jpg
 
Ukisimama nchale ukikimbia nchale team ya wazee leo inabondwa kwa mara ya kwanza .
 
Back
Top Bottom