Yanga ni bora tusingeshiriki Kagame. Mimi naona kama sisi kuna Kitu tulifanywa tulipokuwa wadogo

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
1,694
3,982
Sisi Yanga kuna kitu tulifanywa kwa kweli. Ni mashabiki wa kipumbavu sana. Yaani week nzima tunahangaika na Manara na Mo.

Hatujiandai Wachezaji wetu wapo muda wote busy na mitandao. Insta na twitter kumuunga mkono Manara na kumsema Mo. Tunatolewa mapema mashindano ambayo yangetupa uzoefu wa mashindano ya kimataifa.

Imeniumiza sana. Huu ni wendawazimu. Tulipaswa kujikita kwenye mambo ya maana ya team yetu. Simba wanatuchuuza sana..sasa tunatolewa kwa aibu kwenye mashindano mapema sana. Halafu tunaji biizisha na manara.

This time Simba wametuweza sana. Tunahangaika na mambo ya kipuuzi sana. Tunaacha ku deal na mambo yetu. Inaumiza. Mi naona kama kuna kitu tulifanywa tulipokuwa wadogo
 
Usitulishe maneno kila mtu mtazamo wake, kwanza huwezi kuwa Yanga wewe, Yanga wanajitambua sana, eti mashindano haya kujiandaa kwaajili ya mechi za kimataifa du poor you, timu zipo kwenye mapumziko na pia zipo kwenye usajili

Yanga tulishiriki kwa malengo 3, kwanza kuwatumia vijana wetu wa U 20 ambao wanatazamiwa kupanda kwenda timu ya wakubwa, pili kuwatumia wachezaji ambao hawakucheza ligi sana ambao yanga wanampango wa kuwatema, na tatu kuwatumia baadhi ya wachezaji ambao kamati ya usajili inataka kujiridhisha na kiwango chao.
 
Bora wewe haukubemendwa wakati mdogo! Wakati wenzenu wako busy kuandaa script ya kuendelea kuwazungumzia huku wakijipanga,nyie mko busy kuwafuatilia.
 
Usitulishe maneno kila mtu mtazamo wake, kwanza huwezi kuwa Yanga wewe, Yanga wanajitambua sana, eti mashindano haya kujiandaa kwaajili ya mechi za kimataifa du poor you, timu zipo kwenye mapumziko na pia zipo kwenye usajili...
Mngechukua ndoo hio ndo ingekuwa timu rasmi msimu ujao. Geez😁
 
Usitulishe maneno kila mtu mtazamo wake, kwanza huwezi kuwa Yanga wewe, Yanga wanajitambua sana, eti mashindano haya kujiandaa kwaajili ya mechi za kimataifa du poor you, timu zipo kwenye mapumziko na pia zipo kwenye usajili

Yanga tulishiriki kwa malengo 3, kwanza kuwatumia vijana wetu wa U 20 ambao wanatazamiwa kupanda kwenda timu ya wakubwa, pili kuwatumia wachezaji ambao hawakucheza ligi sana ambao yanga wanampango wa kuwatema, na tatu kuwatumia baadhi ya wachezaji ambao kamati ya usajili inataka kujiridhisha na kiwango chao.
Naona mpo kwenye mapumziko ya kukesha mitandaoni, mme-draw mbili mkatandikwa moja, mko busy na yule kuwadi Manara.
 
Sisi Yanga kuna kitu tulifanywa kwa kweli. Ni mashabiki wa kipumbavu sana. Yaani week nzima tunahangaika na Manara na Mo.

Hatujiandai. Wachezaji wetu wapo muda wote busy na mitandao. Insta na twitter kumuunga mkono manara na kumsema Mo. Tunatolewa mapema mashindano ambayo yangetupa uzoefu wa mashindano ya kimataifa.

Imeniumiza sana. Huu ni wendawazimu. Tulipaswa kujikita kwenye mambo ya maana ya team yetu. Simba wanatuchuuza sana..sasa tunatolewa kwa aibu kwenye mashindano mapema sana. Halafu tunaji biizisha na manara.

This time Simba wametuweza sana.tunahangaika na mambo ya kipuuzi sana. Tunaacha ku deal na mambo yetu. Inaumiza. Mi naona kama kuna kitu tulifanywa tulipokuwa wadogo
timu mbovu hyo
 
Waziri Junior, Juma Mahadhi, yule Konde Boy wao wanayetaka kumsajili, nk. Hawa wote ni average players!
Wapewe mkono wa kwa heri, wakajitafutie ridhiki mahali pengine.

Ninja apelekwe kwa mkopo hata Geita Gold huko ili akaongeze uzoefu, na pia kushauriwa matumizi ya akili zaidi kuliko nguvu awapo uwanjani.

Golikipa Metacha Mnata arejeshwe kundini! Kukosea kwa binadamu ni jambo la kawaida. Sidhani kama angeweza kuonesha ile ishara ya matusi iwapo asingechokozwa na wale mashabiki.

Mwisho kabisa nataka niweke wazi! Binafsi nawaunga mkono viongozi na benchi la ufundi kwa kuwajaribisha wachezaji waliokosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza, lakini pia kuwapa nafasi wale wachezaji wa U20! Lakini utekelezaji wa hatua ufuate mara moja! Masuala ya kuendelea kuwalipa watu mishahara huku wakiwa hawana tija inayotakiwa uwanjani, ni matumizi mabaya ya fedha za klabu.

Viongozi walione hili.
 
Hakuna tofauti mkuu tatizo la yanga lipo kwenye chemestry ya team kila siku wachezaji wapya na makocha wapya duu kwa hili utoaji wataishia kuwa wa majaribio tu
 
Wewe ulifanywa kitu kibaya ukiwa mdogo. Sikulaumu.
Usitulishe maneno kila mtu mtazamo wake, kwanza huwezi kuwa Yanga wewe, Yanga wanajitambua sana, eti mashindano haya kujiandaa kwaajili ya mechi za kimataifa du poor you, timu zipo kwenye mapumziko na pia zipo kwenye usajili

Yanga tulishiriki kwa malengo 3, kwanza kuwatumia vijana wetu wa U 20 ambao wanatazamiwa kupanda kwenda timu ya wakubwa, pili kuwatumia wachezaji ambao hawakucheza ligi sana ambao yanga wanampango wa kuwatema, na tatu kuwatumia baadhi ya wachezaji ambao kamati ya usajili inataka kujiridhisha na kiwango chao.
 
Mchezaji Mpira tunamwita Ninja. Unategemea atakuwa na Akili Uwanjani? Hii inatokea tu Tanzania kwa team yetu. Mchezaji mpira hawezi itwa Ninja. We angalia miaka yetu ya nyuma kulikuwa na Mabeki. Anaitwa beki mstaarabu. Hao walikuwa wanacheza mpira

Waziri Junior, Juma Mahadhi, yule Konde Boy wao wanayetaka kumsajili, nk. Hawa wote ni average players!
Wapewe mkono wa kwa heri, wakajitafutie ridhiki mahali pengine.

Ninja apelekwe kwa mkopo hata Geita Gold huko ili akaongeze uzoefu, na pia kushauriwa matumizi ya akili zaidi kuliko nguvu awapo uwanjani.

Golikipa Metacha Mnata arejeshwe kundini! Kukosea kwa binadamu ni jambo la kawaida. Sidhani kama angeweza kuonesha ile ishara ya matusi iwapo asingechokozwa na wale mashabiki.

Mwisho kabisa nataka niweke wazi! Binafsi nawaunga mkono viongozi na benchi la ufundi kwa kuwajaribisha wachezaji waliokosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza, lakini pia kuwapa nafasi wale wachezaji wa U20! Lakini utekelezaji wa hatua ufuate mara moja! Masuala ya kuendelea kuwalipa watu mishahara huku wakiwa hawana tija inayotakiwa uwanjani, ni matumizi mabaya ya fedha za klabu.

Viongozi walione hili.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom